Mwana Mtoka Pabaya
JF-Expert Member
- Apr 22, 2012
- 15,118
- 16,470
Pumba nyingi nazozisikia ma ProPesa wetu wa chuo kikuu wakiziongea kwenye media huwa wanaongea Kiswahili. Hata neno 'jalalani' ni la Kiswahili.
Mmmmmmmmh! Ndio.
Mtoa maada sijui amekula nini leo. Engineering au Health sciencies zilivyo ngumu kwa kiingereza eti uje utumie kiswahili. Acheni ujinga.Wanangu siwezi wafundisha kiswahili Mimi sijaona faida take! Kalugha ka kuunga unga kako kwa ajili ya kujazana ubishi tu. Hivi taaluma za kuunda meli, ndege, udaktari nk utatumua kiswahili gani kuwaelewesha wanafunzi? Hebu tuache ujinga basi!
Kwani sasa tunapata fursa gani kwa kufundishwa kwa kiingereza? Maana pamoja na kufundishwa kwa kiingereza bado kiingereza hatujui si wasomi wala wasio wasomi.Acha Alinacha zako. Kuna Watanzania wengi tu ambao ni wazalendo hawakusoma kwa Kiswahili. Au unataka kutuambia kuwa Mwalimu Nyerere alikuwa na kasumba ya ukoloni?
Kama hujui English wewe jitahidi tu kujifunza. Hakuna sababu ya kutaka kila mtu akose fursa ili tu mlingane.
Sasa wewe na mchina mko sawa? Veta wanafundishwa kiswahili ukitajiwa components za engine ya gari na mwalimu wa VETA hutawahi kukitamani hicho kiswahili unachokisifia.mb
mbona wewe huna akili kabisa kwani technolojia haiwezi fundishwa kwa kiswahili jinga kweli wachina wanajua kiingereza? mbona wameenda mwezini
hakuna utumwa mbaya kama wa fikra afadhali wa kipato
Tatizo mnataka kila neno kwenye techonology basi ulitafutie neno lake la kiswahili tena mara nyingi linakuwa gumu.wewe ndo mjinga mkubwa usiye elewa maana ya kufundisha kwa kiswahili watanzania wote tunaongea kiswahili alafu lugha yenye kuongelewa na wale waliopata bahati ya kusoma iwe lugha ya kufundisha. Huu ni unyanyasaji watoto wetu wangefaulu na kuelewa masomo vizuri
Na huenda una wadhifa katika serikali hii wewe mzigo mkubwa sana
wewe ndo mjinga mkubwa usiye elewa maana ya kufundisha kwa kiswahili watanzania wote tunaongea kiswahili alafu lugha yenye kuongelewa na wale waliopata bahati ya kusoma iwe lugha ya kufundisha. Huu ni unyanyasaji watoto wetu wangefaulu na kuelewa masomo vizuri
Na huenda una wadhifa katika serikali hii wewe mzigo mkubwa sana
Haita kaa itokee hata siku moja asilani abadani watanzania milioni 55 wote waje kuishi huko uliko wewe na wenzio wachache mnaopata tabu kuongea kiingereza ! Idadi kubwa tutabaki Tanzania tukiwasiliana kwa lugha yetu tamu ya kiswahili !
Sasa waswahili wanataka maneno ya kilatini wayaweke kwa lugha ya kisukuma halafu hiyo lugha ndo tufundishie. Aiseee hebu tuwe serious.China hadi leo hii haitaki kuitwa first world (developed) country. Na ina vyuo vingi tu vinavyotoa kozi zao kwa Kiingereza. Unadhani ni kwa nini?
Unadhani ni kwa nini nchi nyingi duniani hadi leo zinatumia terminologies za Kilatini kwenye legal matters?
Can you explain that?