Mkuu mkwawa kuna generation ngapi kwan?
amd ni bristol ridge ni zipi
kwa intel processor zao maarufu kuna generation sita mpaka sasa na ya saba itatoka baadae mwaka huu
-1st generation inaitwa nehalem/westemere
-2nd generation inaitwa sandy bridge
-3rd generation inaitwa ivy bridge
-4th generation inaitwa haswell
-5th generation inaitwa broadwell
-6th generation inaitwa skylake
baadae mwaka huu na mwakani itatoka
-7th generation itakayoitwa kabylake
-8th generation itakayoitwa canonlake
kama nilivyosema hapo juu hizo generation ni kwa ajili ya processor maarufu tu kama i5/i3/i7 na core m na baadhi ya pentium na celeron kwa umaarufu tunasema "core series"
intel pia ana series nyengine za processor ndogo maarufu kama atom hizi haziingiliani na hizo generation hapo juu huku unakuta generation kama baytrail, cherry trail, braswell na apolo lake. hizi huwa zinatumia umeme mdogo sana na perfomance pia ni ndogo na celeron na pentium za sasa zinatumia atom inabidi uwe makini sana kama unanunua laptop ya celeron au pentium ili ujue kama inatoka kwenye core au atom.
kuhusu amd pia ana series zake nae zipo bulldozer, kaveri, godavari, bristol ridge, carrizo etc sema amd amekuwa outdated sana wana architechture yao mpya inaitwa zen itakuja 2017 nafkiri wengi wanasema itakuwa nzuri huwenda ikacompete na intel.
hakuna tofauti sana kwenye generation kama 4 hivi za amd karibia zote zinafanana.
na cpu za bristol ridge zitaingia sokoni hivi karibuni hivyo nyingi bado hazijajulikana ni leaks tu ndio zipo