PC nzuri ina sifa zipi?

TEK

Senior Member
Jul 13, 2015
184
34
Heshima kwenu wandugu.

Kutokana na hali ilivyosasa mahitaji ya pc yamekuwa makubwa sana. Mimi ni mmoja kati ya wahitaji wakubwa wa kompyuta (PC).

Kwa kuwa nina uhitaji ila siyo mtaalam wa hivi vitu naomba mnisaidie kujua uzuri wake unategemea vitu gani hasa kwenye PC hadi iwe na uwezo mkubwa wa kuprocess mambo hasa upande wa kwenye mtandao
 
mkuu ukichagua generation ya kisasa automatic mambo mengine nayo yanakuwa mazuri, kwa intel generation ya 6 yaani skylake na kwa amd ni bristol ridge japo narecomend zaidi intel.

kuzijua kama hii ni generation ya 6 angalia namba ya kwanza ya processor itaanziwa na namba 6 na itakuwa na namba 4 kwa ujumla. mfano wa processor za generation ya 6 ni kama

i7 6700
i5 6500
i3 6100

ukiwa na generation mpya inamaana automatic
-ram zitakuwa za kisasa (ddr4)
-hdd itakuwa na speed kidogo
-adapter za wifi na component nyengine za ndani zitakuwa nzuri

hapo ndio kiurahisi kadri nilivyoweza kuelezea ila kama unataka maelezo zaidi inabidi tuingie deep kila kifaa ndani ya pc kuanzia processor, ram, hdd, mobo, gpu etc
 
Mkuu mkwawa kuna generation ngapi kwan?

amd ni bristol ridge ni zipi

kwa intel processor zao maarufu kuna generation sita mpaka sasa na ya saba itatoka baadae mwaka huu

-1st generation inaitwa nehalem/westemere
-2nd generation inaitwa sandy bridge
-3rd generation inaitwa ivy bridge
-4th generation inaitwa haswell
-5th generation inaitwa broadwell
-6th generation inaitwa skylake

baadae mwaka huu na mwakani itatoka
-7th generation itakayoitwa kabylake
-8th generation itakayoitwa canonlake

kama nilivyosema hapo juu hizo generation ni kwa ajili ya processor maarufu tu kama i5/i3/i7 na core m na baadhi ya pentium na celeron kwa umaarufu tunasema "core series"

intel pia ana series nyengine za processor ndogo maarufu kama atom hizi haziingiliani na hizo generation hapo juu huku unakuta generation kama baytrail, cherry trail, braswell na apolo lake. hizi huwa zinatumia umeme mdogo sana na perfomance pia ni ndogo na celeron na pentium za sasa zinatumia atom inabidi uwe makini sana kama unanunua laptop ya celeron au pentium ili ujue kama inatoka kwenye core au atom.

kuhusu amd pia ana series zake nae zipo bulldozer, kaveri, godavari, bristol ridge, carrizo etc sema amd amekuwa outdated sana wana architechture yao mpya inaitwa zen itakuja 2017 nafkiri wengi wanasema itakuwa nzuri huwenda ikacompete na intel.

hakuna tofauti sana kwenye generation kama 4 hivi za amd karibia zote zinafanana.

na cpu za bristol ridge zitaingia sokoni hivi karibuni hivyo nyingi bado hazijajulikana ni leaks tu ndio zipo
 
mkuu shukran kwa maelezo mazuri ila sasa naomba utupe na mifano ya hizo pc ili tukienda kununua tujue ni aina zipi hasa zinatufaa
 
pc zipo tofauti sana aina moja tu ya pc inaweza kuwa na aina ndogo ndogo karibia 20 ambazo zinakidhi mahitaji tofauti tofauti hivyo siwezi kukwambia kanunue pc fulani bila kujua unaenda ifanyia nini na una budget kiasi gani.

mfano mzuri angalia dell xps 13 zipo version za core m, i3, i5, i7 na hizo version hapo zipo za broadwell na skylake na zipo za 4gb, 8gb na 16gb na zipo zenye touch na zisizo na touch na zipo zenye resolution full hd na QHD hivyo ukifanya hesabu hapo unapata aina 96 (makisio tu)

laptop moja inaitwa dell xps 13 lakini ina aina tofauti tofauti kibao
 
mkuu hii sanaa ya pc ni hobby tu sidhani hata kama humo mashuleni inafundishwa, kila mtu anaweza kuijua akitaka si lazima uwe umesomea It.
mkuu kweli upo deep/lakin kwa mtu kama mkuu aliyeiomba ushauri,hii ni overkill.nadhani muomba usahuri(hata mimi) angependa/ningependa kujua vtu basic kama brand nzuri,uimara,ukubwa wa ram,storage,labda swala la upatikanaji wa hardware za kureplace kwa brand flani,na muhimu bei kwa makadirio tuu,na vingine basic unavyovijua mkuu.nadhani mkuu(mleta uzi)atakuwa ni mtumiaji wa kawaida kama matumizi ya mwanafunzi wa chuo hv,yani vitu common ni kujaza movies kibao miziki picha,kufanya kaz ndogondogo kama kutype,kutumia internet/kudownload nk.natanguliza shukrani.
 
mkuu post ya kwanza nimerahisisha kabisa chagua generation ya kisasa then probability ya hio computer kuwa nzuri nayo ni kubwa.

mfano laptop za i3 6100u na i5 6200u zote zinapatikana around 600,000 hadi milioni 1 hizi automatic zinakuwa laptop nzuri kwa matumizi ya kawaida na ukicheki specs zake utakuta automatic ni nzuri ram itakuwa 4gb kupanda na ni ddr4 au ikiwa ddr3 basi speed itakuwa nzuri, hdd itakuwa na ukubwa wa kutosha na mambo mengi yatakuwa mazuri.
 
Naomba nikusahihishe mkuu hapo kwenye version ya RAM...m,i ddr3 na sio ddr4
NOTE: labda kwa watumiaji wa apple products
mkuu ukichagua generation ya kisasa automatic mambo mengine nayo yanakuwa mazuri, kwa intel generation ya 6 yaani skylake na kwa amd ni bristol ridge japo narecomend zaidi intel.

kuzijua kama hii ni generation ya 6 angalia namba ya kwanza ya processor itaanziwa na namba 6 na itakuwa na namba 4 kwa ujumla. mfano wa processor za generation ya 6 ni kama

i7 6700
i5 6500
i3 6100

ukiwa na generation mpya inamaana automatic
-ram zitakuwa za kisasa (ddr4)
-hdd itakuwa na speed kidogo
-adapter za wifi na component nyengine za ndani zitakuwa nzuri

hapo ndio kiurahisi kadri nilivyoweza kuelezea ila kama unataka maelezo zaidi inabidi tuingie deep kila kifaa ndani ya pc kuanzia processor, ram, hdd, mobo, gpu etc
 
kwa intel processor zao maarufu kuna generation sita mpaka sasa na ya saba itatoka baadae mwaka huu

-1st generation inaitwa nehalem/westemere
-2nd generation inaitwa sandy bridge
-3rd generation inaitwa ivy bridge
-4th generation inaitwa haswell
-5th generation inaitwa broadwell
-6th generation inaitwa skylake

baadae mwaka huu na mwakani itatoka
-7th generation itakayoitwa kabylake
-8th generation itakayoitwa canonlake

kama nilivyosema hapo juu hizo generation ni kwa ajili ya processor maarufu tu kama i5/i3/i7 na core m na baadhi ya pentium na celeron kwa umaarufu tunasema "core series"

intel pia ana series nyengine za processor ndogo maarufu kama atom hizi haziingiliani na hizo generation hapo juu huku unakuta generation kama baytrail, cherry trail, braswell na apolo lake. hizi huwa zinatumia umeme mdogo sana na perfomance pia ni ndogo na celeron na pentium za sasa zinatumia atom inabidi uwe makini sana kama unanunua laptop ya celeron au pentium ili ujue kama inatoka kwenye core au atom.

kuhusu amd pia ana series zake nae zipo bulldozer, kaveri, godavari, bristol ridge, carrizo etc sema amd amekuwa outdated sana wana architechture yao mpya inaitwa zen itakuja 2017 nafkiri wengi wanasema itakuwa nzuri huwenda ikacompete na intel.

hakuna tofauti sana kwenye generation kama 4 hivi za amd karibia zote zinafanana.

na cpu za bristol ridge zitaingia sokoni hivi karibuni hivyo nyingi bado hazijajulikana ni leaks tu ndio zipo
Nimependa hapo kwenye kutambua processor za Celeron na Pentium za atom na ambazo si atom lakni haujapaelezea, kwa faida ya wote nini kitafanya kuzitambua hizo processor?

Kati ya processor ya Pentium na celeron ipi ina nguvu kushinda nyingine kwa matoleo yote?
 
Nadhani Kwanza ingekuwa vizuri kuelewa unataka PC kwa ajili ya Matumizi gani unaweza nunua Pc yenye uwezo mkubwa halafu Matumizi yako kumbe ni kuchapa barua ,kuangalia Movie na ku peruzi mtandaoni. Ukifanya hvyoo hutakuwa na tofauti na mtu alienunua Transit kwa ajili ya kupeleka Mtoto shule.

Ushauri wangu : Uzuri wa Pc unategemeana na Matumizi yako
Nawasilisha
Babu Kifimbo Cheza
 
huko ddr3 tumeshahama mkuu kuanzia skylake watu wamehamia ddr4 ambazo zina speed na bandwidth kubwa zaidi ya ddr3
Nime edit post yangu mkuu...ila kwa ndo ipo mbioni kuhamia makampuni mengine yanayozalisha kompyuta
Kwa sasa hv wanafaidika wateja wa apple toleo la Latina ambayo bei yake bora ukanunue shamba tu litakusaidia baadae uzeeni
 
Nimependa hapo kwenye kutambua processor za Celeron na Pentium za atom na ambazo si atom lakni haujapaelezea, kwa faida ya wote nini kitafanya kuzitambua hizo processor?

Kati ya processor ya Pentium na celeron ipi ina nguvu kushinda nyingine kwa matoleo yote?

mkuu kama zote zipo generation moja ujue speed yake inatokana na ghz, yenye ghz kubwa ndio itakayokuwa na speed zaidi, na zote zinakuwa na core mbili (dual core)

mfumo wa processor za celeron na pentium unafanania na i3/i5/i7 ikiwa hizo processor zipo kwenye core family. kwa laptop inamaana either itaishiwa na m kwa mbele au U

-zinazoishiwa na M mbele TDP (umeme) ni watt 35
-zinazoishiwa na U mbele TDP yake ni watt 15

hizo za M zinatumia umeme mkubwa na perfomance ni kubwa na hizo na hizo za U zinatumia umeme mdogo na perfomance ya kawaida,

mfano wa pentium na celeron za M ni kama
-pentium 3550M
-pentium 3560M
-pentium 2020M
-Celeron 2950M
-Celeron 2970M

mfano wa pentium na celeron za U ni kama
-celeron 3205U
-celeron 3215U
-pentium 3805U
-Pentium 3825U

kiufupi celeron na pentium za core zinakuwa ni kama i3/i5 na i7 sema hazina tu hyperthread (kasoro pentium 3825u)

hizi zina nguvu kufanya mambo mengi hata games zinahimili kiasi.

ukija kwenye pentium na celeron ambazo zinatokana na atom hizi zinakuja na computer zote mpya za bei rahisi kwa sasa. ukienda madukani kununua pc za laki 5 ujue asilimia 99% zitakuwa ni hizi. perfomance yake ni ndogo kama simu vile ila hukaa sana na charge na zipo nyengine zina hadi memory za simu (emmc) badala ya HDD. mimi ninayo moja inakaa na chaji masaa 17 kama unasomea tu bila kuingia online, na inakaa hadi masaa 10 kama unakuwa online.

hizi huanziwa na herufi N mfano kama
-celeron N3050
-pentium N3700

hivyo kuconclude hapo Ukiona processor ya celeron au pentium kwa mbele inaishiwa na U au M ujue ni family ya core sawa na i3/i5 na i7 na ukiona imeanza na N ujue ni atom

kama unataka computer ya bei rahisi inayokaa na charge nunua inayoanza na N ila itakuwa haina nguvu hio computer na kama unataka laptop nzuri ya bei rahisi yenye nguvu tafuta Pentium inayoishiwa na M
 
Nime edit post yangu mkuu...ila kwa ndo ipo mbioni kuhamia makampuni mengine yanayozalisha kompyuta
Kwa sasa hv wanafaidika wateja wa apple toleo la Latina ambayo bei yake bora ukanunue shamba tu litakusaidia baadae uzeeni
sijakuelewa mkuu unamaanisha hizo processor mpya zinapatikana kwenye computer za apple ambazo bei zake ni sawa na shamba?

zipo pia processor za skylake ambazo zinapatikana kwenye computer za bei za kawaida kama i3 6100u
 
Heshima kwenu wandugu.

Kutokana na hali ilivyosasa mahitaji ya pc yamekuwa makubwa sana. Mimi ni mmoja kati ya wahitaji wakubwa wa kompyuta (PC).

Kwa kuwa nina uhitaji ila siyo mtaalam wa hivi vitu naomba mnisaidie kujua uzuri wake unategemea vitu gani hasa kwenye PC hadi iwe na uwezo mkubwa wa kuprocess mambo hasa upande wa kwenye mtandao
PC nzuri ni ile ambayo itakidhi mahitaji yako kwa wakati huo unaohitaji na miaka kadhaa mbele, lakini kikubwa ni bajeti yako.
 
Daaaah mkuu kwa maelezo uliompa anaweza ishia nunua PC iliyo pigwa msasa tuuuu... hayo maelezo ungetoa kwa ambaye ni Pro or Expert tayari ila sio kwa #Beginner
 
Back
Top Bottom