Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,060
- 43,477
hizo ndio best laptop duniani kwa wafanyabiashara, hazina feature za kimauzo ila zina vitu muhimu wafanyabiashara kamaHivi mkuu laptop za lenovo thinkpad zina kitu gani cha ziada mbona ghali sana?
-processor zenye nguvu
-battery zinazokaa sana na charge (hadi masaa 24)
-keypads nzuri zinazobonyezeka kirahisi
-warranty za miaka 3
-ni rahisi kuzi upgrade vitu kama ram, hdd nk
-zinadumu kwa muda mrefu na thinkpad nyingi zinakuwa na layer ya magnesium alloy kulinda vitu vya ndani visiharibike
-zinakuwa na bios maalum kwa ajili ya wafanyabiashara na zinasuport encryption mbali mbali kama AES inayopatikana kwenye ssd
pia thinkpad ni brand maarufu toka kipindi ipo IBM hadi ilivyokuja kununuliwa na Lenovo