Paypal: Upotevu wa mapato na ajira Tanzania

Paypal: Upotevu wa mapato na ajira Tanzania

Awali sikujua Kuwa Tanzania sio member wa paypal, nikafungua duka Zuri Sana eBay, nikaanza kupokea lawama kwa wateja Na meseji nyingi wanahitaji kulipia Na mm nikaona njia rahisi Ni PayPal. Kumbe Tanzania haimo kabisa lkn Kenya Na Uganda wenzetu wanafanya mambo makubwa kupitia hiya maduka ya kimataifa. Kiukweli eBay, emazon kuna Ajira ambazo Kama Serikali itakua sirias itasaidia vijana wengi sana. Nchi itauza bidhaa nyingi sana duniani Na Itakuwa inaingiza Dola nyingi.
Bidhaa Gani Mkuu Tutaziuza Kwa Wingi ..... Wakat Viwanda Hatuna Na Ss Tunalangua China .. au Mambo ya Kutoa Ndizi Moshi Unapeleka kuuza Bukoba
 
Acheni kurusha watu stimu nyie. Watu wenyewe hamzalishi kitu zaidi ya umbea. Sasa hata hiyo PayPal hata ikianzishwa, wabongo mna kitu gani cha kuuza? Stori za Wema Sepetu labda.

Punguza ulimbukeni mama.
 
Bidhaa Gani Mkuu Tutaziuza Kwa Wingi ..... Wakat Viwanda Hatuna Na Ss Tunalangua China .. au Mambo ya Kutoa Ndizi Moshi Unapeleka kuuza Bukoba

Bidhaa nyingi za utamaduni unaweza kuuza nje ya Tanzania, wateja wapo wengi sana.
Au ingia ebay angalia categories ya vitu ambavyo vipo pale. Ndo utajua tunaweza kuuza nini.
 
Bidhaa nyingi za utamaduni unaweza kuuza nje ya Tanzania, wateja wapo wengi sana.
Au ingia ebay angalia categories ya vitu ambavyo vipo pale. Ndo utajua tunaweza kuuza nini.
Sasa Unadhani Kila Mtu Atauza Vitu Hivyo Na Unadhani Kila Mtu atataka kuuza Vitu vya Utamaduni.... Ebay

Vipi nikitaka Kuuza Simu... Maana Nalangua China Kwa Bei Poa Then Namuuzia Mmarekani au
 
Ni wazi wale wote tunaofuatilia mambo ya technology; especially E-Commerce(biashara kwa njia ya internet) mtakubaliana na mimi nchi yetu imepoteza mapato mengi sana na ajira nyingi sana kwa watanzania hasa vijana wasomi.Kwa nini ?

Nitoe mifano michache then wenzangu mtaongezea zaidi.Kuna mitandao maarufu kama EBAY na AMAZON (E-commerce platforms).Hizi sites zimetoa ajira kubwa sana kwa vijana na makampuni kwa Marekani,China,Kenya na nchi nyingine nyingi duniani.

Utajiuliza hapa kwanini watanzania hawauzi na kunufaika na haya masoko makubwa duniani EBAY,AMAZON and the like?

JIBU: Ni mfumo wa malipo. Ukiwa Tanzania huwezi kupokea malipo toka nchi nyingine kwa kutumia Paypal.Kwa kifupi ni kwamba nchi yetu bado haijaruhusu kupokea fedha kwa njia ya PAYPAL kutoka nchi nyingine duniani.Hivyo,ukiwa Tanzania Unaruhusiwa tuu KUTUMA(one way) kwa njia ya Paypal.

Kwanini PAYPAL? Ninakubali kuna njia nyingi za kupokea malipo, taja njia yoyote ile lakini hakuna inayoifikia Paypal(Security & number of Customers).Hivyo,Paypal inaaminika zaidi duniania kuliko njia nyinginezo tunazozifahamu.Nilishawahi kupata a number of customers on Ebay kikwazo ikawa kwenye suala la malipo.Wateja wengi wanaimani zaidi na Paypal.So far I am grateful kwamba ninajua baadhi ya bidhaa ambazo foreign customers wanazihitaji sana(kutokana na inquiries) nilizozipata baada ya ku-list online some of the products made in Tanzania.

Kuna watanzania wengi tu mikoani huko wanazalisha na kutengeneza products nyingi na nzuri ambazo mataifa ya kigeni yanazihitaji lakini kikwazo kikubwa(Opportunity here!) ni kukosa access ya international market.

Kuna tabia ya watanzania kupuuza technology,kugopa technology,na wengine may be inatokana na kukosa taarifa na uelewa wa fursa zitokanazo na technology(Computer & Internet ….) au kubweteka na old model of doing things(Business as usual)

Pia viongozi wetu wengi wanasisitiza kilimo pekee.Bila kuangalia upanuzi wa masoko.Tunahitaji vyote kulima,kufuga,viwanda na kupanua masoko hasa mosoko ya nje(kimataifa).Technology imekua,Dunia imebadilika nasi tubadilike.

Sio kila mmoja lazima aishie kulima na kufuga pekee; japo kulima na kufuga ni muhimu,tunahitaji kufikiria mbali na mbele zaidi.

Nina imani serikali hii ni sikivu,pia nina imani itasikia na kutenda.Zaidi ni imani yangu kwa Mr. President Dr. Magufuli. Tusikubali kuendelea kupoteza fedha na ajira huku majirani zetu Kenya ,Mozambique wakiendelea kuneemeka na kunufaika na hii fursa.

Niseme tu kwamba mimi na vijana wenzangu(wanaojitambua) tupo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote,wakati wowote,kwa taasisi/shirika lolote na kwa wakati wowote ili kuhakikisha nchi yetu inanufaika na hii fursa(E-commerce) ambayo itakuawa ni mkombozi wa ajira kwa vijana wengi zaidi na kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Kenya Wameweza na wanafanya,Mozambique wameweza na wanafanya.WHY NOT US, WHY NOT NOW?

GOD BLESS TANZANIA not Lema only-LOL!(hapa nimechomekea tu)
Ukitoka nje ndo utajuwa pia uzembe wa serikali.

Mfano, nipo diaspora, leseni ya udereva ya Kenya inatambulika yaani wakenya wakitaka leseni ni kitendo cha kuwasilisha ya Kenya kwenye mamlaka na kupewa ya huku.

Tanzania sasa, mtu unalazimika kulipia euro kibao kwa ajili ya mtihani na majaribio barabarani kisa, Tanzania haijasign moja kati ya mikataba inayohusiana na usalama barabarani.

Ukilinganisha idadi ya wabongo tuliopo diaspora na mataifa mengine tupo wachache mnoo. Hii ni changamoto.

Juzi kati hata kwa kutumia worldremit nilishindwa wakati ni njia rahisi na flexible pia.

Tanzania bado tutaburuzwa sana
 
Sasa Unadhani Kila Mtu Atauza Vitu Hivyo Na Unadhani Kila Mtu atataka kuuza Vitu vya Utamaduni.... Ebay

Vipi nikitaka Kuuza Simu... Maana Nalangua China Kwa Bei Poa Then Namuuzia Mmarekani au
kwa hiyo unataka kuuza marekani simu feki?
 
Ni kweli kabisa ndugu,nchi yetu bado imelala sana ktk mambo mengi.Tunahitaji nguvu ya pamoja kuondoka hapa tulipo.Wanasiasa wengi wanafurahia umasikini wa watanzania kwani ndio mtaji wao.Sasa tuseme NOO!
 
Sasa Unadhani Kila Mtu Atauza Vitu Hivyo Na Unadhani Kila Mtu atataka kuuza Vitu vya Utamaduni.... Ebay

Vipi nikitaka Kuuza Simu... Maana Nalangua China Kwa Bei Poa Then Namuuzia Mmarekani au

Huwezi kuuza simu. You will not offer competitive price.
China haijawa na bei ya chini kuliko marekani kwasababu wanatengenezewa huko na kuletewa kwa bei ya chini.
Isitoshe Marekani wananunua simu kwa mfumo wa contract kati ya mteja na kampuni ya simu.
 
Ukitoka nje ndo utajuwa pia uzembe wa serikali.

Mfano, nipo diaspora, leseni ya udereva ya Kenya inatambulika yaani wakenya wakitaka leseni ni kitendo cha kuwasilisha ya Kenya kwenye mamlaka na kupewa ya huku.

Tanzania sasa, mtu unalazimika kulipia euro kibao kwa ajili ya mtihani na majaribio barabarani kisa, Tanzania haijasign moja kati ya mikataba inayohusiana na usalama barabarani.

Ukilinganisha idadi ya wabongo tuliopo diaspora na mataifa mengine tupo wachache mnoo. Hii ni changamoto.

Juzi kati hata kwa kutumia worldremit nilishindwa wakati ni njia rahisi na flexible pia.

Tanzania bado tutaburuzwa sana

Hatuna viongozi wenye vision kabisa. Wanachojua ni kwenda kazini na kurudishwa nyumbani.
 
Harpo TE="Nguvu sio Pesa, post: 16460518, member: 187031"]Wewe Jane Lowassa.. Amka...hivi hizi products kama nguo za batiki....vinyago... Viatu vya kimasai... Urembo...mazao... Majanai ya mchachai... Nk.. Hizi ni products ambazo ni big deal kwa inchi za ulaya na marekani na middle east.... Na kama mfumo wa paypal ungekua unaruhusiwa na serikali kama moja ya official transactions.. Ningekua millionaire[/QUOTE]
Hapo kwenye mazao inakuwaje? Unaweza kuuza gunia 100 za mbaazi kwa mteja aliyepo Saudi Arabia?
 
Bulldog said:
Kama sio mfanyabiashara huwezi kuona fursa. Shirikisha ubongo wako.
Mbona husemi hizo fursa? Naona hapo juu eti umetaja batiki. Yaani kwa akili zako, sister duu wa kizungu avae hiyo mibatiki yenu isiyokuwa na kiwango chochote. Batiki unafua siku mbili imeshachuja.
 
Huwezi kuuza simu. You will not offer competitive price.
China haijawa na bei ya chini kuliko marekani kwasababu wanatengenezewa huko na kuletewa kwa bei ya chini.
Isitoshe Marekani wananunua simu kwa mfumo wa contract kati ya mteja na kampuni ya simu.
Kwahiyo haina Haja Sasa Ya Kulalamika Paypal Tanzania haipo Wakati Mna Bidhaa Moja Tu Mtakayouza Zingine Hamuuzi.....

Halafu Si Wote Wana Contacts na Makampuni
 
Hili swala ni muhimu sana , tupaze sauti mm ni mhanga wa hili
 
Mbona husemi hizo fursa? Naona hapo juu eti umetaja batiki. Yaani kwa akili zako, sister duu wa kizungu avae hiyo mibatiki yenu isiyokuwa na kiwango chochote. Batiki unafua siku mbili imeshachuja.
we ndio kenge kweli wazungu wengi tena mabinti wadogo wanaongoza kwa kununua mashuka ya kimasai hapa ngorongoro tembea uone
 
Mbona husemi hizo fursa? Naona hapo juu eti umetaja batiki. Yaani kwa akili zako, sister duu wa kizungu avae hiyo mibatiki yenu isiyokuwa na kiwango chochote. Batiki unafua siku mbili imeshachuja.
Bangili za kimasai..shanga za kimasai..vinyago wazungu wananunua sana we endelea kujiuza maana ndio biashara pekee unayoiweza
 
He...[emoji15]
Hivi kupata michongo wa kwenda UK ni dili eeehhh..[emoji47]
Alafu.....[emoji5]
Kumbe ukifanikia kwenda UK, maana yake unauhakika wa kua milionea.....[emoji12]
soma post uelewe mkuu acha kukurupuka.. nilipata mchongo from my friend yupo UK nikashindwa kuufanikisha coz PayPal ilizingua haipo Tz so business ikafa.. next time soma uelewe acha mapepe bado asubuhi
 
Back
Top Bottom