Paypal: Upotevu wa mapato na ajira Tanzania

Genius one

Senior Member
Jul 11, 2015
134
69
Ni wazi wale wote tunaofuatilia mambo ya technology; especially E-Commerce(biashara kwa njia ya internet) mtakubaliana na mimi nchi yetu imepoteza mapato mengi sana na ajira nyingi sana kwa watanzania hasa vijana wasomi.Kwa nini ?

Nitoe mifano michache then wenzangu mtaongezea zaidi.Kuna mitandao maarufu kama EBAY na AMAZON (E-commerce platforms).Hizi sites zimetoa ajira kubwa sana kwa vijana na makampuni kwa Marekani,China,Kenya na nchi nyingine nyingi duniani.

Utajiuliza hapa kwanini watanzania hawauzi na kunufaika na haya masoko makubwa duniani EBAY,AMAZON and the like?

JIBU: Ni mfumo wa malipo. Ukiwa Tanzania huwezi kupokea malipo toka nchi nyingine kwa kutumia Paypal.Kwa kifupi ni kwamba nchi yetu bado haijaruhusu kupokea fedha kwa njia ya PAYPAL kutoka nchi nyingine duniani.Hivyo,ukiwa Tanzania Unaruhusiwa tuu KUTUMA(one way) kwa njia ya Paypal.

Kwanini PAYPAL? Ninakubali kuna njia nyingi za kupokea malipo, taja njia yoyote ile lakini hakuna inayoifikia Paypal(Security & number of Customers).Hivyo,Paypal inaaminika zaidi duniania kuliko njia nyinginezo tunazozifahamu.Nilishawahi kupata a number of customers on Ebay kikwazo ikawa kwenye suala la malipo.Wateja wengi wanaimani zaidi na Paypal.So far I am grateful kwamba ninajua baadhi ya bidhaa ambazo foreign customers wanazihitaji sana(kutokana na inquiries) nilizozipata baada ya ku-list online some of the products made in Tanzania.

Kuna watanzania wengi tu mikoani huko wanazalisha na kutengeneza products nyingi na nzuri ambazo mataifa ya kigeni yanazihitaji lakini kikwazo kikubwa(Opportunity here!) ni kukosa access ya international market.

Kuna tabia ya watanzania kupuuza technology,kugopa technology,na wengine may be inatokana na kukosa taarifa na uelewa wa fursa zitokanazo na technology(Computer & Internet ….) au kubweteka na old model of doing things(Business as usual)

Pia viongozi wetu wengi wanasisitiza kilimo pekee.Bila kuangalia upanuzi wa masoko.Tunahitaji vyote kulima,kufuga,viwanda na kupanua masoko hasa mosoko ya nje(kimataifa).Technology imekua,Dunia imebadilika nasi tubadilike.

Sio kila mmoja lazima aishie kulima na kufuga pekee; japo kulima na kufuga ni muhimu,tunahitaji kufikiria mbali na mbele zaidi.

Nina imani serikali hii ni sikivu,pia nina imani itasikia na kutenda.Zaidi ni imani yangu kwa Mr. President Dr. Magufuli. Tusikubali kuendelea kupoteza fedha na ajira huku majirani zetu Kenya ,Mozambique wakiendelea kuneemeka na kunufaika na hii fursa.

Niseme tu kwamba mimi na vijana wenzangu(wanaojitambua) tupo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote,wakati wowote,kwa taasisi/shirika lolote na kwa wakati wowote ili kuhakikisha nchi yetu inanufaika na hii fursa(E-commerce) ambayo itakuawa ni mkombozi wa ajira kwa vijana wengi zaidi na kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Kenya Wameweza na wanafanya,Mozambique wameweza na wanafanya.WHY NOT US, WHY NOT NOW?

GOD BLESS TANZANIA not Lema only-LOL!(hapa nimechomekea tu)
 
Attachments

  • Paypal -Mozambique.png
    Paypal -Mozambique.png
    101.8 KB · Views: 184
  • Paypal-TZ.png
    Paypal-TZ.png
    88.4 KB · Views: 157
  • Paypal-kenya.png
    Paypal-kenya.png
    97.3 KB · Views: 180
Awali sikujua Kuwa Tanzania sio member wa paypal, nikafungua duka Zuri Sana eBay, nikaanza kupokea lawama kwa wateja Na meseji nyingi wanahitaji kulipia Na mm nikaona njia rahisi Ni PayPal. Kumbe Tanzania haimo kabisa lkn Kenya Na Uganda wenzetu wanafanya mambo makubwa kupitia hiya maduka ya kimataifa. Kiukweli eBay, emazon kuna Ajira ambazo Kama Serikali itakua sirias itasaidia vijana wengi sana. Nchi itauza bidhaa nyingi sana duniani Na Itakuwa inaingiza Dola nyingi.
 
Hii serikali yetu sijui ikoje,wakishauriwa juu ya jambo kama hilo utanaona watakavyoanza kuleta ujuaji wao....'ooh tunafanya hivyo kwasababu za kiusalama...sijui nini....'.Nasikia pia hata matangazo ya television yameruhusiwa mwisho ukanda huu wa Afrika Mashariki na si zaidi ya hapo,hatujui fursa tunazozipoteza kutokana na sera hizi zilizopitwa na wakati.Duo citizenship ni janga lingine kwa nchi hii.
 
Ni kweli kabisa,kuna fursa kubwa sana.Nchi yetu ikifungua mlango huu,hakika itakuwa imetengeneza ajira kubwa sana kwa vijana & next-multi-millionaires & billionaires.
 
Kutokana kwa kukua kwa Tecnoloji haya maduka ya eBay, emazon yanaweza kusaidia vijana wengi sana hapa nchini, tunaiomba serikali ilipe kipaumbele hili la PayPal kuweza kuuza bidhaa Na kupokea Pesa kupitia paypal. Ni rahisi kufanya biashara kimataifa lkn Nina wasiwasi wa kiwango cha uaminifu walionao watanzania. Hapa ndipo panapotakiwa kujadiliwa kwa kina.
 
Hii serikali yetu sijui ikoje,wakishauriwa juu ya jambo kama hilo utanaona watakavyoanza kuleta ujuaji wao....'ooh tunafanya hivyo kwasababu za kiusalama...sijui nini....'.Nasikia pia hata matangazo ya television yameruhusiwa mwisho ukanda huu wa Afrika Mashariki na si zaidi ya hapo,hatujui fursa tunazozipoteza kutokana na sera hizi zilizopitwa na wakati.Duo citizenship ni janga lingine kwa nchi hii.

Tusikate tamaa,tuendelee kupaza sauti. I belive there better days ahead.Siku moja wataelewa tusemayo na kutekeleza.
 
Maoni yangu Kuhusu Ebay/PayPal:
EBay wana policy ya refund kama bidhaa uliouziwa kupitia mtandao wao either haijakufikia au imeharibika Na mmeshindwa kufikia muafaka Na Seller.

Sasa kwa kesi ya Tanzania ni ngumu kwa sababu address haziko tracked. Itakuwa ni vigumu kwa eBay kuthibitisha kama bidhaa ulionunua imefikufikia au la. Halafu wa Nigeria waliwatapeli sana wazungu Na watumiaji wengine wa EBay.
Mfano: unauza simu kwa $100, mtu anabid Na kuwin, kisha anakutumia fake email kutoka PayPal kusema umepokea $400. Kisha Yule mtu anakuandikia email kusema kakosea amekutumia pesa nyingi kwa hiyo anaomba umrudishie $300 kwenye PayPal account yake.
Ziko njia nyingi Ambazo fraudsters wanazitumia kuibia watu via PayPal/EBay. Ndio maana wanaweza sanctions kama hizo.

Update:
Ebay na PayPal wametengana sasa, mwanzo walikuwa pamoja, japokuwa bado unaweza kulipia bidhaa ulionunua EBay kwa PayPal.

Ebay wameanzisha "Click & Collect" kwa UK. Unanunua bidhaa online kisha unaenda kuchukua kwenye Click & Collect shop jirani Na wewe.

Way Forward:
Fanya research,tafuta wadhamini contact EBay uanzishe click & Collect service Tanzania.
Tatizo la hiyo itakuwa kwenye kuwalipa kodi TRA. Maana mtu atanunua simu kwa $10 atalipakodi shs 50,000.
 
Kweli kabisa, we need to establish paypal payments in Tanzania. Dunia ya sasa imebadilika na kila kitu kina involve mitandao. Inabidi Tanzania iwe technological country.. Malipo ya mitandao yatawezesha fursa za kibiashara kwa vijana na pia yatapunguza rushwa serikalini

Ni kweli kabisa.Ni vizuri sisi vijana wenye uelewa na hili swala tuendelee kupaza sauti zetu bila kurudi nyuma wala kukata tamaa.
 
Ni wazi wale wote tunaofuatilia mambo ya technology; especially E-Commerce(biashara kwa njia ya internet) mtakubaliana na mimi nchi yetu imepoteza mapato mengi sana na ajira nyingi sana kwa watanzania hasa vijana wasomi.Kwa nini ?

Nitoe mifano michache then wenzangu mtaongezea zaidi.Kuna mitandao maarufu kama EBAY na AMAZON (E-commerce platforms).Hizi sites zimetoa ajira kubwa sana kwa vijana na makampuni kwa Marekani,China,Kenya na nchi nyingine nyingi duniani.

Utajiuliza hapa kwanini watanzania hawauzi na kunufaika na haya masoko makubwa duniani EBAY,AMAZON and the like?

JIBU: Ni mfumo wa malipo. Ukiwa Tanzania huwezi kupokea malipo toka nchi nyingine kwa kutumia Paypal.Kwa kifupi ni kwamba nchi yetu bado haijaruhusu kupokea fedha kwa njia ya PAYPAL kutoka nchi nyingine duniani.Hivyo,ukiwa Tanzania Unaruhusiwa tuu KUTUMA(one way) kwa njia ya Paypal.

Kwanini PAYPAL? Ninakubali kuna njia nyingi za kupokea malipo, taja njia yoyote ile lakini hakuna inayoifikia Paypal(Security & number of Customers).Hivyo,Paypal inaaminika zaidi duniania kuliko njia nyinginezo tunazozifahamu.Nilishawahi kupata a number of customers on Ebay kikwazo ikawa kwenye suala la malipo.Wateja wengi wanaimani zaidi na Paypal.So far I am grateful kwamba ninajua baadhi ya bidhaa ambazo foreign customers wanazihitaji sana(kutokana na inquiries) nilizozipata baada ya ku-list online some of the products made in Tanzania.

Kuna watanzania wengi tu mikoani huko wanazalisha na kutengeneza products nyingi na nzuri ambazo mataifa ya kigeni yanazihitaji lakini kikwazo kikubwa(Opportunity here!) ni kukosa access ya international market.

Kuna tabia ya watanzania kupuuza technology,kuugopa technology,na wengine may be inatokana na kukosa taarifa na uelewa wa fursa zitokanazo na technology(Computer & Internet ….) au kubweteka na old model of doing things(Business as usual)

Pia viongozi wetu wengi wanasisitiza kilimo pekee.Bila kuangalia upanuzi wa masoko.Tunahitaji vyote kulima,kufuga,viwanda na kupanua masoko hasa mosoko ya nje(kimataifa).Technology imekua,Dunia imebadilika nasi tubadilike.

Sio kila mmoja lazima aishie kulima na kufuga pekee; japo kulima na kufuga ni muhimu,tunahitaji kufikiria mbali na mbele zaidi.

Nina imani serikali hii ni sikivu,pia nina imani itasikia na kutenda.Zaidi ni imani yangu kwa Mr. President Dr. Magufuli. Tusikubali kuendelea kupoteza fedha na ajira huku majirani zetu Kenya ,Mozambique wakiendelea kuneemeka na kunufaika na hii fursa.

Niseme tu kwamba mimi na vijana wenzangu(wanaojitambua) tupo tayari kutoa ushirikiano wa aina yoyote,wakati wotote,kwa taasisi/shirika lolote na kwa wakati wowote ili kuhakikisha nchi yetu inanufaika na hii fursa(E-commerce) ambayo itakuawa ni mkombozi wa ajira kwa vijana wengi zaidi na kuliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Kenya Wameweza na wanafanya,Mozambique wameweza na wanafanya.WHY NOT US WHY NOT NOW?

GOD BLESS TANZANIA not Lema only-LOL!(hapa nimechomekea tu)
Mkuu uko vizuri sana.
Sijui kama wanauelewa lkn Unaweza kumuandikia hata rais barua kama wadau mbalimbali humu wenye Mawazo chanya japo wanalalamika Kuwa kuna huwa hazimfikii.

Nimepitia kwenye forums za wanigeria sio wachoyo Wa maarifa. Hivyo vitu ulivyovisema nakushauri pia ulete kama somo. Kuna mapesa mengi mitandaoni lkn wachache tu Nigeria,Kenya,SA na baadhi ya nchi za Africa Ila weñgi hasa sisi tuko slow sana na Viongozi wetu weñgi wanatakiwa kuanza kufikili kidigital. Naona weñgi wako deep kwenye negative effects za mitandao.
 
Nakuunga mkono, na nitashiriki katika juhudi hizi za kuwafahamisha vijana juu ya hivi vitu.
Nimeona.
pia kuna site kibao zinalipa tu hata kwa kuandika makala na ikakubaliwa. Hapo silaa yako ni kuwa na mawazo na kujua muingeleza vizuri cha kuandika.
Mfano:www.listverse.com
 
Maoni yangu Kuhusu Ebay/PayPal:
EBay wana policy ya refund kama bidhaa uliouziwa kupitia mtandao wao either haijakufikia au imeharibika Na mmeshindwa kufikia muafaka Na Seller.

Sasa kwa kesi ya Tanzania ni ngumu kwa sababu address haziko tracked. Itakuwa ni vigumu kwa eBay kuthibitisha kama bidhaa ulionunua imefikufikia au la. Halafu wa Nigeria waliwatapeli sana wazungu Na watumiaji wengine wa EBay.
Mfano: unauza simu kwa $100, mtu anabid Na kuwin, kisha anakutumia fake email kutoka PayPal kusema umepokea $400. Kisha Yule mtu anakuandikia email kusema kakosea amekutumia pesa nyingi kwa hiyo anaomba umrudishie $300 kwenye PayPal account yake.
Ziko njia nyingi Ambazo fraudsters wanazitumia kuibia watu via PayPal/EBay. Ndio maana wanaweza sanctions kama hizo.

Update:
Ebay na PayPal wametengana sasa, mwanzo walikuwa pamoja, japokuwa bado unaweza kulipia bidhaa ulionunua EBay kwa PayPal.

Ebay wameanzisha "Click & Collect" kwa UK. Unanunua bidhaa online kisha unaenda kuchukua kwenye Click & Collect shop jirani Na wewe.

Way Forward:
Fanya research,tafuta wadhamini contact EBay uanzishe click & Collect service Tanzania.
Tatizo la hiyo itakuwa kwenye kuwalipa kodi TRA. Maana mtu atanunua simu kwa $10 atalipakodi shs 50,000.
Tunashukuru kwa mchango wako.Lakini sio kweli kwamba swala la utapeli ndio limeifanya Tanzania isipate hiyo huduma. Kuna nchi ambazo baadhi wananchi wake wana PHD za kutapeli watu mtandaoni lakini bado wanapata Full paypal services.So,there more than fraud issues.
 
Sawa mkuu. Huwezi kuielewa point yangu kwa sasa, Ila IPO siku utaelewa.

Angalia hii

07837bdb9c4e4ce3276af1bcedb4d88d.jpg

Sasa hizo fees wanacharge za nini wakati hawana service Tanzania?
 
Nilishawah kupoteza Pound 247 kisa tu Tz haimo. Nilinunua bidhaa the ile order ikawa cancelled ikabid waniambie wananirudishia hela after negotiation. Kuzirudisha sasa kwa Paypal ndio balaa. Kama mtu anafanya E purchasing atumie CBA, hii bank ni ya wakenya so ukitumiwa hela kwa paypal huwa zinakuja. I have tried this and it works
 
Nakuunga mkono, na nitashiriki katika juhudi hizi za kuwafahamisha vijana juu ya hivi vitu.
Nimeona.
pia kuna site kibao zinalipa tu hata kwa kuandika makala na ikakubaliwa. Hapo silaa yako ni kuwa na mawazo na kujua muingeleza vizuri cha kuandika.
Mfano:www.listverse.com
Ahsante ndugu,tushirikiane kufikisha ujumbe bila kuchoka.Ukiingia kwenye sites nyingi zinazolipa utakuta profiles za wengi wakenya, then south Africa,Mozambique,...Vijana wenzetu wamekamata fursa sisi.....? Mpaka roho yaniuma kwa kweli.
 
Maoni yangu Kuhusu Ebay/PayPal:
EBay wana policy ya refund kama bidhaa uliouziwa kupitia mtandao wao either haijakufikia au imeharibika Na mmeshindwa kufikia muafaka Na Seller.

Sasa kwa kesi ya Tanzania ni ngumu kwa sababu address haziko tracked. Itakuwa ni vigumu kwa eBay kuthibitisha kama bidhaa ulionunua imefikufikia au la. Halafu wa Nigeria waliwatapeli sana wazungu Na watumiaji wengine wa EBay.
Mfano: unauza simu kwa $100, mtu anabid Na kuwin, kisha anakutumia fake email kutoka PayPal kusema umepokea $400. Kisha Yule mtu anakuandikia email kusema kakosea amekutumia pesa nyingi kwa hiyo anaomba umrudishie $300 kwenye PayPal account yake.
Ziko njia nyingi Ambazo fraudsters wanazitumia kuibia watu via PayPal/EBay. Ndio maana wanaweza sanctions kama hizo.

Update:
Ebay na PayPal wametengana sasa, mwanzo walikuwa pamoja, japokuwa bado unaweza kulipia bidhaa ulionunua EBay kwa PayPal.

Ebay wameanzisha "Click & Collect" kwa UK. Unanunua bidhaa online kisha unaenda kuchukua kwenye Click & Collect shop jirani Na wewe.

Way Forward:
Fanya research,tafuta wadhamini contact EBay uanzishe click & Collect service Tanzania.
Tatizo la hiyo itakuwa kwenye kuwalipa kodi TRA. Maana mtu atanunua simu kwa $10 atalipakodi shs 50,000.
Unajua malipo ya PayPal kweli? Labda useme mtu asitume mzigo na hapo ndani ya siku 45 ukifungua kesi ,unarudishiwa chako.

Ndio maana PayPal ipo trusted worldwide.
 
Sawa mkuu. Huwezi kuielewa point yangu kwa sasa, Ila IPO siku utaelewa.

Angalia hii

07837bdb9c4e4ce3276af1bcedb4d88d.jpg

Sasa hizo fees wanacharge za nini wakati hawana service Tanzania?

Hizo fees nami nilishaziona,but in reality Tanzania haipo kwenye nchi zinazo-receive payment via Paypal.Ili uweze ku-confirm ninachosema hapa,check attachments za hii post nilizoziweka.Linganisha attachment ya Kenya,Mozambique Vs Tanzania.
 
Back
Top Bottom