Mateja M.G Yango,
Hilo jambo ni muhimu sana na mimi binafsi niliwahi kulivalia njuga. Kwa mujibu wa PayPal ambao niliwasiliana nao, tatizo sio moja kwa moja toka kwao bali kuna some administrative issues (may be some regulations or something like that) vile vile zinahitajika kutoka kwetu (serikalini).
Kilicho wazi ni kwamba PayPal hawatuhitaji sana sisi kama tunavyowahitaji wao; kwa maana nyingine sidhani kama kuna economic factors zinazoweza kuwashawishi PayPal kutufuata sisi badala ya sisi kuwafuata wao. Kutokana na ukweli huo, binafsi nilikuwa nasubiria tu hii serikali ya Magufuri ikae sawa ili niliibue hili suala. Nilikusudia kufungua petition vile vile but not directly to PayPal but to the government at least ku-create awareness. Lazima tukubali kwamba haya mambo ni mageni sana kwahiyo hata huko serikalini kwenyewe wengi hawafahamu lolote! Na ndio maana ilikuwa hata ukienda kwenye benki zetu ambako wengi ni vijana na wasomi, lakini bado unakuta wengi hawafahamu.
So, wakati unaendelea na hizo harakati zako, nami soon nina mpango huo huo lakini kwanza nitajaribu ku-create awareness kabla ya ku-file petition. Lakini kwavile issue yenyewe kwa PayPal nilituma query muda mrefu, nitaanza kwa kutuma fresh query ili kutafuta jibu lao kwa sasa ni lipi!