Payoneer ni mbadala halisi wa PayPal!

Na kama ukinunua kitu online kupitia wao, bahati kitu hakijakufikia, wanaweza kuhakikisha pesa yako inarudi?
 
Mimi sina a/c ya bank hata moja sasa nifanyeje na jee naweka pesa kupitia m-pesa ama
 
Inawezekana Mkuu! Kwa Ku transfer hiyo 500,000 kwenda kwenye Payoneer account yako! Na ukafanya manunuzi mtandaoni!

Kumbuka Payoneer ni sawa na Bank account nyingine, utofauti ni kuwa hii ni online banking!

Na kwa vile ni free unaweza kufanya registration na uka apply card yako! Inaweza kutokea siku unahitaji kununua kitu mtandaoni ikakurahisishia!

Au uko na friend nje ya nchi akakutumia pesa kupitia Payoneer!
Tatizo huelewi swali hata trasfer vipi Atatuma Kwenye Ndege Pesa Mpaka Marekani Kwenye Benki Husika Ili Aweke Au Elezea kwa Ufasaha Anaenda wapi Au Benk gani Au anatumia system ipi Ku trasfer?
 
Na kama ukinunua kitu online kupitia wao, bahati kitu hakijakufikia, wanaweza kuhakikisha pesa yako inarudi?
Wana refund pesa yako Mkuu! Ila kwa Websites ambazo Wao wana makubaliano nayo, zipo nyingi but pia hutegemea na issue yenyewe!

Check hapo chini juu ya refund policy zao!

Refund Policy for Payoneer
 
tatizo huelewi swali hata trasfer vipi Atatuma Kwenye Ndege Pesa Mpaka Marekani Kwenye Benki Husika Ili Aweke Au Elezea kwa Ufasaha Anaenda wapi Au Benk gani Au anatumia system ipi Ku trasfer?
Tatizo la watu Kama wewe huwa hamfatilii comment, swali lako nimejibu Mara kadhaa huko juu!

Ni hivi, unataka kununua kwa payoneer au master card ya payoneer, ni lazima uwe na local bank account, hivyo utatoa pesa toka local bank kwenda payoneer then utaendelea na mambo mengine.
 
Inachukua mda mpaka uipate ukisha apply online?
After registration na ku appy Card, huchukua Week 2 mpaka 3 mpaka Card yako kufika, Wao wenyewe watakutumia email wakikwambia lini Card yako itafika.
 
Habari Wakuu!
Binafsi ni mtu ambaye niliathiliwa na kutokubaliwa kwa PayPal Tanzania, kwa wale wenzangu na Mimi ambao tumekua tukiuza kazi zetu online, watakubaliana nami kuwa Clients wengi wanajisikia salama wakilipa kwa PayPal, Clients wengi hawataki kusikia Western Union, Moneygrams na hata Bank Transfer.

Ilipelekea wengi kupata shida namna kupokea malipo Yao, hapa jf Kuna thread kadhaa za members wakitoa malalamiko Yao.

Kwa wale wote waliokua wanakwazwa na kutokuwepo PayPal, sasa wanaweza kutumia Payoneer Master Card, uta apply Card yako toka America na ndani ya week 2 au 3 utatumiwa Master card ya Payoneer ambayo itakuwezesha Ku withdraw pesa yako kwenye ATM yoyote inayo support Master card Worldwide, pia unaweza Kuhamisha pesa yako toka Payoneer kwenda kwenye account yako ya bank!

Binafsi Mimi ndo naitumia, mpaka sasa nimesha withdraw pesa zaidi ya Mara 3.

Nakuwekea link hapo chini, huduma zote ikiwemo Card ni bure.

Una swali au chochote Karibu.

https://share.payoneer.com/nav/1IYl...XyTobBfQIlfYwJKEZGoAAd7S9xVGy2c5HvirbrcC8syA2

Unaposema paypal haijaruhusiwa tanzania unamaanisha nn?.
Nikiwa tz siruhusiwi kumiliki account ya paypal? Au siruhusiwi kufanya any bank transfer via paypal? Siruhusiwi ku-link my card(visa,MasterCard..etc) na paypal account?
Au kwa namna gani yoyote ile siwezi tumia paypal!..
 
After registration na ku appy Card, huchukua Week 2 mpaka 3 mpaka Card yako kufika, Wao wenyewe watakutumia email wakikwambia lini Card yako itafika.
Ku register na Ku apply card how much does it cost au ni bure???
 
Nime apply io payoneer na wameshanbia wananitumia lakini naona ni tatizo katika matangazo na maelezo yao yote wanaeleza hio ni account ya kulipwa toka kwa wateja, sijaona popote wakisema na mimi naweza lipia bidhaa pengine.

Ebu tupatie ufafanuzi maana inaonesha ipo tofauti na paypal. Paypal una shop, hii unapokea tu malipo ma kutoa
 
Nime apply io payoneer na wameshanbia wananitumia lakini naona ni tatizo katika matangazo na maelezo yao yote wanaeleza hio ni account ya kulipwa toka kwa wateja, sijaona popote wakisema na mimi naweza lipia bidhaa pengine. Ebu tupatie ufafanuzi maana inaonesha ipo tofauti na paypal. Paypal una shop, hii unapokea tu malipo ma kutoa
Hilo ndo lengo haswa pale walipoanzisha hii huduma.

Mkuu bila shaka ushawahi kuona kwenye website mbalimbali kuwa unaweza kulipia kwa Master card, Visa Card n.k, hivyo ukiwa Na Payoneer account utakua na Master card ya Payoneer, so utaweza kununua chochote mtandaoni Ni sawa na Kama ungekua na Master card ya Local bank.

Pia Seller wengi sasa nao wana Payoneer account, so unaweza kulipa/kununua direct toka kwa Payoneer account yako, kwenda kwa Payoneer account ya Seller.
 
Mkuu unajaza nini sehemu ya zip code nimekwama hapo na je kadi yangu watantumia ktk sanduku LA posta ntakalojza au naipokelea WAP?
 
Back
Top Bottom