Masalu Jacob
JF-Expert Member
- Jul 26, 2017
- 1,339
- 1,493
Habari Tanzania !
Napenda kuleta wazo hasa kwa Serikali Tanzania na Vijana wa Tanzania endapo ikiwapendeza.
Tuanzishe taasisi ya Vijana Ujenzi Taifa; waajiriwe vijana wenye nia na kutumika kwenye sekta ya ujenzi Taifa.
Itungwe Sheria ya usimamizi miundombinu na ujenzi majengo Taifa. Pia pawepo na Sera ya Ujenzi Taifa kuhusu Shirika hili la Vijana.
Naomba mapendekezo yafuatayo yatumike kwenye hii taasisi;
1. Ujenzi wowote kuanzia wa miundombinu na ujenzi ngazi ya kijiji/ mtaa, Kata, Wilaya, Mkoa; itasimamiwa na hii taasisi kuanzia ngazi ya upimaji udongo, usanifu wa miundombinu na majengo; ujenzi wa jengo husika na utunzaji wa jengo aidha la mtu binafsi au taasisi hapa nchini.
2. Tenda zote za Taifa hasa miradi ya ujenzi yote hili shirikia lipewe kipaombele na ndio watakuwa wasanifuu wakuu wa miundombinu yote inayohusu ujenzi.
3. Kila mwananchi awe na "UJENZI CARD". Hii kadi itakuwa maalumu kwa kila mwenye uhitaji wa ujenzi. Hata taasisi Binafsi na Umma lazima wawe nayo hii kadi.
Atapaswa kuchangia kiasi kidogo kidogo kutokana na mahitaji yake ya ujenzi na atapewa huduma moja kwa moja juu ya uhitaji wake hata kama hajakamilisha ada yake ya hitaji. Uzuri atapewa ukadiliaji mzuri wa gharama za hitaji lake.
(Ujenzi - Card itaunganishwa moja kwa moja na mifumo mingine kama Banks, NIDA, TRA,POLISI, JWTZ nk).
Angalizo
1. Hii taasisi inauwezo wa kuajiri vijana 5,000,000 kwa mkupuo (moja kwa moja) nchi nzima.
2. Ujenzi ndio sekta pekee yenye utatuzi wa kiuchumi hasa mzunguko wa pesa na ajira kwa jamii.
3. Tutachochea uundwaji wa miundombinu bora na tutazuia ujenzi holela hapa nchini.
4. Serikali ikiwapendeza mnaweza sasa mkawatafutia michongo ya ujenzi nchi za ng'ambo huko vijana wakaleta fedha za kigeni hapa nvhini kukuza Taifa letu.
5. NHC (Shirika la Nyumba Taifa), Suma JKT na TBA (Wakala wa Ujenzi Tanzania) hizi taasisi zisihusike na hiyo taasisis ya Ujenzi Taifa yaani wao waendelee na majukumu yao hivyo hivyo wakae mbali.