Pauline Gekul anastahili kuvuliwa uanachama na kufikishwa mahakamani haraka sana. Amekichafua na kukipaka matope chama

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,311
9,739
Ndugu zangu Watanzania,

Kwanza nianze kwa kumpongeza mh Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama samia suluhu Hasssan kwa kutengua uteuzi wa Pauline Gekul. kwa Vitendo vya aibu na udhalilishaji alivyovifanya kama mbunge na naibu waziri wa katiba na sheria.

Kiukweli ametia aibu sana,amekitia aibu chama cha mapinduzi,amekipaka matope chama,ameleta hasira kwa wananchi. Binafsi nashangaa roho mbaya namna hiyo anaipata wapi Gekul? Hivi yeye si ni mwanamke? Hivi Alikuwa Hajisikii wala kuhisi uchungu kwa hayo aliyoyatenda? Tumbo lake lilikuwa halimtetemi kwa maumivu wakati anatekeleza unyama huo? Ameanzia wapi na kupata wapi ujasiri wa kufanya hayo ilihari yeye ndiye anasimamia wizara inayopaswa kusimamia sheria na utekelezaji wake kwa haki?

Nini kilimpa kiburi cha kufanya hayo? Tangia lini yeye akawa polisi yeye mwenyewe, mpelelezi yeye mwenyewe,mtesaji yeye mwenyewe, mahakama yeye mwenyewe na mtoa hukumu yeye mwenyewe?

Anatuma ujumbe gani kwa kauli yake ya kwamba atamuua huyo mtoto na kumtupa ziwani? Je ameua wangapi? Amewatupia ziwani wangapi? Amepoteza roho za wasio na hatia wangapi? Ametesaa wangapi? Amejeruhi wangapi? Amewaharibu watu wasio na hatia wangapi? Amedhalilisha wangapi? Amewashushia heshima watu wangapi? Emefanya maovu mangapi gizani? Ametoa maelekezo kwa jeshi la polisi kutesa wabaya wake wangapi na Mara ngapi? Amewaacha watu na vilema gizani wangapi?

Yafuatayo yafanyike kwa huyu mbunge.

Kwanza ,chama cha mapinduzi yaani CCM kijitenga na matendo yake hayo maovu kwa kulaani hadharani kitendo hicho na kumlazimisha muhusika kutoka hadharani kuomba msamaha.

Pili ,avuliwe uanachama au awajibishwe kwa namna yoyote ile. Lakini pia hata akibaki ndani ya chama basi asipewe nafasi ya aina yoyote ile ya uongozi ndani ya chama na hata serikalini.kwa sababu kila mtu anafahamu kuwa CCM huwatetea na kuwapigania wanyonge,huwafuta machozi watu na kuwapatia faraja na matumaini na siyo kuwabubujisha machozi watu wala kuwatesa wala kuwaonea wala kuwadhulumu haki zao wala kuwaumiza wala kuwapa vilema au kuuwa watu.

Tatu,afunguliwe mashtaka na kufikishwa mahakamani kama ambavyo wengine wamekuwa wakifikishwa ili kuonyesha kuwa sheria ni msumeno.kukaa kimya pasipo kumchukulia hatua ni kujenga picha mbaya sana kwa jamii kuwa wanaokwenda mahakama na jera au mahabusu ni maskini pekee na walala hoi na siyo kwa wenye vyeo au waheshimiwa au wenye pesa zao.

Nne ,upelelezi ufanyike ili askari waliofanya utesaji kwa maelekezo ya Gekul wachukuliwe hatua za kisheria na kinidhamu. Kwa sababu wao wanapaswa kufanya na kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa sheria na siyo kauli ya kiongozi au mbunge kwa hisia zake binafsi..

Tano ,yule mtoto apewe msaada wa kisaikolojia na matibabu kwa kuwa kitendo hicho kimemuathiri, lakini pia alipwe fidia na kama alikuwa kuna hela anamdai boss wake Basi alipwe haraka sana.

Sita ,nashauri mbunge huyo apokonywe bastola yake, maana naamini hakupewa kwa ajili ya kutishia watu kuwaua bila sababu na kuwatupia ziwani.kuendelea kumuachia Bastola hiyo inaweza kuja kuleta madhara makubwa, kwa kuwa muhusika hafahamu matumizi yake na wapi itumike.

Chama cha Mapinduzi kiwaite wabunge wake wote na kuwakumbusha dhamani kubwa na heshima kubwa waliyo nayo katika jamii ,na kwamba hawapaswi kutumia madaraka yao kuwaumiza au kuwatesa watu,kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanakichafua chama mbele ya macho ya watanzania.na kwamba chama ndicho kilichowapa mdhamana wa kugombea na kwamba kinaweza au hakitasita kuondoa mdhamana huo wakati wowote ule kitakapoona inafaa kufanya hivyo.

Mwisho ni kwamba hakuna atakayekwenda mbinguni na cheo chake.viongozi kuweni na hofu na Mwenyezi Mungu.muogopeni Mungu.Duniani tunapita tu.leo ni kiongozi kesho siyo kiongozi au kesho jina linabadilika na kuitwa marehemu. tendeni haki na wema kwa kadri muwezavyo. Kuweni na huruma .Hivyo vyeo ni vya kupita tu na wala siyo vya kudumu.hata uwe nani wewe si chochote mbele za Mungu akiamua kukushusha . Usione na kuringia walinzi wanaokuwa wamekuzunguka ulipokaa na unapowapa amri ,maana Mungu akiamua kukuchukua hakuna hata mmoja wao awezaye kukuokoa na hilo .Mungu akitaka pia kukushusha hata uweje huwezi kuzuia anguko lako.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.

===

Pia soma:

Rais Samia Suluhu atengua uteuzi wa Pauline Gekul saa chache baada ya kutuhumiwa kufanya unyanyasaji

Pauline Gekul ajibu tuhuma za kumdhuru na kumdhalilisha kijana
 
Wazee wa kwenda na Biti hamjambo!!

Hapa mama Samia angeongea kwa kumtetea huyu Gakul ungeibuka na uzi mrefu kuliko huu kumsifia Gekul anyways tumeshawazoea hamtusumbui

Sema nini, Rais Samia hongera sana kwa hili ulilofanya la kumtosa Gakul
Urais wa Kifalme
 
Kwani zile ahadi zenu za kichama zina semaje tena,kwa kukumbusha tu ,Binadamu wote ni sawa na Africa ni moja,nyingine Fitina kwanu ni mwiko, pia zipo ahadi za uadilifu ila ukweli ni kuwa kwenu yote hayo ni sifuri🤪
 
ccm haiwezi kujitenga naye, hakuna mtu amewafanyia watu unyama kama Sabaya na makonda na bado wanapeta...ccm ni ghala la wezi waporaji na wauaji....hiyo ndo imetoka
CCM Ni mtetezi wa wanyonge kwa hiyo hakiwezi kumkumbatia mtu anayekipaka matope na kukichafua kwa matendo yake ya kinyama na kishetani namna hiyo tena mwanamke ambaye anajuwa na kufahamu uchungu wa kuzaa.
 
Hakika, kitendo tu cha kutuhumiwa inafaa kusema hafai. Kwa kiongozi awe amefanya ama hajafanya basi busara inasema "yatosha kusadiki". Kisiasa hii ni ajali na kitakachofuata atateuliwa mwingine kama ambavyo wahenga waliwahi kusema kufa kufaana
 
Wewe lucas unaandika haya umewasiliana na ccm wenzio?
Kesho wakimtetea na kumsafisha utaficha wapi uso wako?

Usije ukarudi utadanganye hapa.!!
CCM Ni mtetezi wa wanyonge na siyo watesaji na wanyanyasaji.kazi ya CCM Ni kuwafuta watu machozi na siyo kuwabubujisha machozi
 
Chama cha Mapinduzi kiwaite wabunge wake wote na kuwakumbusha dhamani kubwa waliyo nayo katika jamii na kwamba hawapaswi kutumia madaraka yao kuwaumiza au kuwatesa watu,kwa kuwa kwa kufanya hivyo wanakichafua chama mbele ya macho ya watanzania.na kwamba chama ndicho kilichowapa mdhamana wa kugombea na kwamba kinaweza kuondoa mdhamana huo wakati wowote ule.
Hio ni tone kati ya mabaya viongozi wa CCM wanayo yatenda Kwa wananchi wasio na hatia. Viongozi wa CCM 99% wananuka damu zisizo na hatia
 
Naona bado alikua na hulka na tabia za alikotoka kabla ya kujiunga CCM.

Baada ya vyombo vingine vya dola kufanya kazi zake dhidi yake, asaidiwe pia kisaikolojia, asiachwe hivi hivi
 
Back
Top Bottom