Paul Makonda bado ni kijana mdogo na asitumike vibaya kama Sabaya

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
13,824
18,568
Makonda bado ni kijana mdogo na bado hana utashi uliokamilika, bado anafanya mambo kwa kufuata hulka, hisia za kiujana na kutegemea watu wanamwona vipi.

Hulka hizi hutumika sana na wakubwa kuwatafuta watu wa kushirikiana nao katika jambo fulani kwa manufaa yao. Wanajua vyema mtu kama Makonda anapenda nini na humpatia anachopenda kwa maagano ya kufanya jambo flani.

Wakubwa hawa hujificha nyuma ya vijana hawa kwa kuwapa nguvu kubwa ya kufanya kama itakavyowafurahisha ili kufananisha jambo flani.

Sabaya alitumika kwa mtindo huo huo na baadaye kutupwa jalalani kwani ukweli ni kwamba hakuna anayewapenda watu hawa ambao kimsingi ni vibaraka wa mkubwa flani.

Iwe iwavyo huo ni mtego mbaya kwa Makonda na kwa bahati mbaya yeye kwasasa anajiona mbarikiwa sana. Siasa za Tanzania ni mchezo unaohitaji mtu kutoka kwa Mungu kuja kurekebisha siasa hizi la sivyo tutaendelea kuwatumikia wanasiasa kwa muda mrefu ujao.
 
Back
Top Bottom