Paul Makonda anaisisimua CCM na kuwazindua watendaji mazoea chamani na Serikalini

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
8,170
11,572
Katibu wa NEC Itikadi na uenezi Taifa, Paul Makonda kwa hakika anaisisimua CCM vilivyo na ana wasanua wananchi hali halisi ya upinzani nchini. Ni kama vile hawapo tu, watoa taarrifa hawa nchini.

Anawazindua watendaji mazoea chamani na serikalini. Ama kwa hakika watendaji wote mazoea wataongeza bidii na maarifa kiutendaji na matokeo yataonekana dhahiri punde kwa wanainchi kufaidika na maendeleo, la sivyo watatetemeka sana.

Waungwana, kwa vibe na vibration hizi za muenezi huyu, ni dhahiri katika muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ujao kuanzia sasa,
matarajio ni kwamba tengua teua zinanukia sana kwa watendaji mazoea chamani na serikalini, lakini pia mabadiliko Baraza la mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya, wakurugenzi na wakuu wa mashirika ya umma hayakwepeki.

Spidi ya Mwenezi ni kimbunga ni hatari kwa watendaji dhaifu, wasio na mipango, ubunifu, wasiowajibika kwa wananchi na wasio na matokeo.

Ilani ya uchaguzi ya 2020-2025 Lazima itekelezwe vilivyo katika ukamilifu wake.
Waziri mkubwa must be very carefully, responsible and visionary, he might be the first victim and second political target giant to fall after Job as we are approaching general elections within near future. Makonda waves are hot to him than any other politician within the gov.This is my political opinion.

Anyway,
Ndugu zangu, mwakani 2024 tunao uchaguzi muhimu sana wa serikali za mitaa, tafadhali sana, tujitokeze kwa wingi kujiandikisha kwajili ya uchaguzi huo wa maana sana kwa mustakabali wa maendeleo mitaani mwetu.
Na mwaka 2025 tujiandae pia kwa uchaguzi mkuu na hatimae baadae mwaka 2026, tuanze upya mchakato wa katiba mpya.

Kwasasa kazi iendelee......
 
Back
Top Bottom