Huyu siyo wa kumpa uhuru wa kufanya anayoyataka, hakawii kurudi kwenye mambo yake ya kuua watu, kuteka na kupora mali za watu. Huyu ni shetani ambaye hakustahili kupewa nafasi hata ya ubalozi wa nyumba 10. Wenye akili wote na wenye hekima wanamshangaa aliyemteua na kumpa nafasi ya uongozi mtu aliyetakiwa kufikishwa kwenye vyombo vya sheria kujibu tuhuma mbalimbali.

Akiendelea kumkumbatia, anaweza kuondoka naye siku umma ukiamka.

Kisasi cha damu alizozimwaga, tunaomba zikawe juu yake na kizazi chake muovu huyu.

RIP Sanane, RIP Azory. Mungu muweza wa yote uwapunguzie majonzi wanafamilia wa hawa ndugu zetu ambao shetani aliwapoteza.
Hakuna kipindi umma utaamka,acha kuota mzee!!!
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
Wameshampa onyo Kali kabla hawajamsikiliza
 
Makonda alirudishwa katikati ya uwanja wa kisiasa na mama Samia.
Mama aliamua kusahau madudu aliyofanya wakati wa Magufuli.
Makonda hakumbuki kuwa aliumiza watu kwa kauli na vitendo.
Tukumbuke alidiriki kumwita hadi Ridhiwani Kikwete kuwa ni don la madawa ya kulevya, wakati hana ushahidi.

Sasa hili la kuwatyhumu viongizi wenzake hadharani, as if yeye Makonda yuko juu yao matokeo yake sasa tunaysona.

Viongozi wenzake sasa wanamfunga kengele shingoni.
Na hili linaweza kuwa tukio la mwanzo wa mwisho wa Makonda.
CCM ikimpiga pini, hata mama Samia hatamsaidia.
Kwani ni uongo. Idiot kabisa. Wauza unga wanajulikana
 
nadhani hii ni alart kwa mama, ajue makonda ana hasara kwa chama chake na uongozi wake kuliko faida. hivyo yeye mwenyewe achague, abaki na makonda apoteze sapoti ya watanzania wengi, au apoteze makonda abaki na watanzania.
Nani kakuambia atapoteza sapoti ya watanzania? Watanzania wengi tunamuelewa Makonda, na tunampa sapoti km ilivyokuwa kwa Magufuli.
 
Umeanzisha thread kuhusu maandamano na hii,

Nadhani unaona ipi imepata wachangiaji wengi,

Ndomana Huwa tunakwambia, unafanya KAZI ya CCM Kwa kujua au kutojua .

Anyway MAGAMBA MATATU naona Bado ameshikilia mkeka wake.
 
Walikuwa wapi kumuita akiwa ktk mikutano ya chama wakati ana sikiliza wananchi na kero zao?

Na mama akasema kuwa amekiamsha chama, pamoja na kuonekana alikuwa ana dhalilisha watu majukwaani na alikuwa anafanya majukumu ya kipolisi, mahakama, serikali nk
Alikuwa hajatenda kosa la kushutuma mawaziri na kuwatishia 😀.

Sasa wanataka kumuonesha namna ya kuwa na staha. Chama kimeshika hatamu.
 
Nani kakuambia atapoteza sapoti ya watanzania? Watanzania wengi tunamuelewa Makonda, na tunampa sapoti km ilivyokuwa kwa Magufuli.
Sema Vyawa wengi mnamuelewa, mngebahatisha kumilika japo punje ndogo ya akili msingejipiga vifua.
 
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ndugu Paulo Makonda ameitwa kwenye Kamati ya Maadili ya Chama cha Mapinduzi.

Ameelekezwa kufika kwenye Kamati hiyo tarehe 22/04/2024.

=====

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimemuita Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda kwenye Kamati ya Maadili.

Makonda anatarajiwa kufika mbele ya Kamati hiyo Jumatatu, Aprili 22, 2024 asubuhi na kukutana na wajumbe wa kamati hiyo.

Hata hivyo, Mwananchi inafahamu kuwa Makonda alitakiwa kufika mbele ya kamati hiyo Aprili 20, 2024 majira ya asubuhi, lakini haikuelezwa sababu za kusogezwa mbele.

Barua ya wito wa CCM kwa Makonda haikueleza sababu za kumuita huku ikieleza kwamba, kuna masuala mbalimbali kati yake na wajumbe wanakwenda kujadili.

Lakini, wito huo huenda unahusishwa na kauli ya Makonda aliyoitoa wakati wa kumbukumbu ya miaka 40 ya kifo cha Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine iliyofanyika Monduli, Arusha ambako Makonda alidai kuwa viongozi wakiwemo mawaziri wamekuwa wakilipa watu kumtukana Rais Samia Suluhu Hassan kwenye mitandao ya kijamii.

Makonda alitoa onyo kwa viongozi hao akisema kama wakiendelea atawataja hadharani na kwamba, hayuko tayari kuona Rais Samia akitukanwa.

Chanzo: Mwananchi online

Pia soma:
IMG_1762.jpeg
 
Back
Top Bottom