Paul mabuga- Tuongee asubuhi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Paul mabuga- Tuongee asubuhi.

Discussion in 'Celebrities Forum' started by samirnasri, Mar 11, 2011.

 1. samirnasri

  samirnasri JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 1,377
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Naomba kutoa dukuduku langu kuhusu huyu mtangazaji wa star tv ambaye mara kadhaa hutangaza kipindi cha tuongee asubuhi kinachorushwa na star tv kila siku kuanzia sa moja na nusu asubuhi hadi sa tatu kamili. Binafsi mtangazaji huyu nimekuwa sipindezwi naye kwa namna anavyoendesha kipindi cha tuongee asubuhi. Nina sababu kuu tatu zinazonifanya nisipendezwe na namna jamaa huyu anvyoendesha kipindi hicho. Mosi, paul mabuga amekuwa na tabia ya kuegemea upande moja hasa ule unaotetea serikali kitu ambacho hatakiwi kukionesha waziwazi yeye akiwa kama mtangazaji.(hapa nazungumzia mada zinazohusisha ukosoaji wa serikali). Katika hili paul mabuga amejipambanua waziwazi kwamba yeye ni kada wa chama cha kijani. Yeye kama mtangazaji anapaswa kusimama katikati pasi kuegemea upande wowote. Pili, paul mabuga amekuwa na tabia ya kuwakatisha wazungumzaji walioalikwa studio mara kwa mara kwa kupachika vijimaswali vya ajabu ajabu kabla hawajamaliza kuzungumza kile walichokuwa wanakieleza. Kwa sababu hiyo amekuwa akipoteza mwelekeo wao wa kuchangia hasa pale wanapokua wanaibana serikali. Nambuka wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu mwaka jana mabuga alimualika dr slaa studio kwenye kipindi hicho ambapo hakutaka kumpa nafasi dr slaa kuzungumza kwa kina na mara nyingi alikua akimkatisha mara kwa mara na kumuuliza vijimaswali visivyo na tija, nakumbuka ilifika wakati dr slaa aliishiwa uvumilivu akamwambi kama hutaki nijieleze ni bora usingenialika hapa studio.. Sababu ya tatu ni kutokana na tabia yake ya kubana muda wa kupiga simu kwa wachangiaji wanaofuatilia kipindi hicho. Mara nyingi anapoendesha kipindi utakuta anaruhusu simu zikiwa zimesalia dakika 20 au 15 kabla ya kipindi kumalizika natokeo yake wanapiga simu watu wawili au watatu kipindi kinamalizika. Hii inaondoa zana ya tuongee asubuhi. Namshauri paul mabuga aige mfano wa watangazaji wenzake samadu hassan na rymond nyamwihula ambao wamekua wakiendesha kipindi hicho kwa uhodari mkubwa na kuwapa waalikwa uhuru wa kuzungumza bila kukatishwa mara kwa mara Nawasilisha.. .
   
 2. howard

  howard Senior Member

  #2
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 188
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Watangazaji wengine ni wapuuzi ukishaona station either ya TV au radio cha kufanya ni kubadilisha tu kama ninavyofanya mimi kwa watu wa clouds kipindi cha jahazi. Maana huwa nasilkiliza vyote kuanzia asubuhi ikifika saa kumi nakwenda channel nyingine nikiona miyeyusho nagonga cd za kwaya tu.
   
 3. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mabuga ni nini?
   
 4. Ba Martha

  Ba Martha JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2011
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  TRUE MKUU..HAIWEZI HIYO FANI..:tongue:
   
 5. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #5
  Mar 11, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Nakubalilia na mtoa mada hasa hili la kumzuia mchangiaji asimalizie hoja anayoitoa huku akiwa yeye ndiyo aliyemuuliza swali

  Kipindi cha leo kikikuwa kizuri lakini nasikitika mtangazaji amekiharibu hatamgeni waliyemualika hata ukiacha mwanza mgeni aliyealikwa dar hakuwa na upeo wa uchambuzi wa mambo nafikiri walisagula pale mlimani kwakuwa ni lecture basi wakamleta studio
  Yahya Mohamed ,Baruni, Angelo mwaleko ninawakubali sana
   
 6. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #6
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Yes pale ingekuwa bora kabisa angewaachia wale jamaa wa mwelekeo wetu wajinome na sisi watazamaji tupate mambo. yeye alikuwa anauliza na yale maswali mabaya, anaulizia hoja ya mikopo ya magari! wapi na wapi! Mbaya sana.
   
 7. m

  msambaru JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 242
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 45
  Ndugu yangu uko sawa kabisa, huyu jamaa mpaka hua natamani nimtumie radi imfanye hakuna, mwingine mwenye tabia za kipuuzi kama hizo ni JANE SHIRIMA wa TBC yani bora kaenda loliondo kwa mchungaji.
   
 8. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #8
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimekiona kipindi, lakini , je usalama wa mtangazaji unakuwa wapi ikiwa mgeni anakaribia kuzunguza jambo ambalo linaweza kuwa kashfa ama tusi kwa namna fulani, lakini mbona nimeona wageni walikuwa wanapewa kauhoja za kuchokozwa ili waongee ... lakini bado licha ya kipindi kuegemea upande mmoja lakini bado tumepata hoja za upande mwingine... maanake vingine kingekuwa kipindi cha kwa ajili ya Cdm kama baadhi ya watu wanavyotaka.

  Ufafanuzi ulikuwa mrefu, nafikiri kama hatujui kazi za watu tusijisemee kama vile tunabishana kwenye matapu tapu
   
 9. MFUKUZI

  MFUKUZI JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 1, 2011
  Messages: 932
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Nasri nakuunga mkono. Huyu Paul Mabuga kiukweli anakera, hajui hata taratibu za kuendesha mahojiano. kweli kabisa huyu ni kada wa CCM na isitoshe akiwa na hoja yake basi hataki kupata mawazo tofuati na anayofikiri yeye. Hafai kuwe kwenye kipindi kile. Mimi nawakubali sana
  Yahya Mohamed ,Baruni muhuza na Angelo mwaleko. Hawa jamaa wanajua kazi zao, huwezi kujua wameegemea wapi wao wanachojali ni kuendesha mjadala kwa mujibu wa taaluma.


  Nawaomba Sta TV huyu jamaa msimweke tena anawaharibia kipindi. akaendeshe Jarida Maridhawa. PAUL MABUGA naomba upumzike tu kwa lengo la kukinusuru kituo chako cha TV
   
 10. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #10
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi kwa nini malalamiko haya yanatokea pale tu huyu jamaa anapoendesha kipindi ambacho kinaihusu CHADEMA sijasikia akilalamikiwa katika mada nyingine! Aanauwauzi nini Wana Nzengo na hasa wale ambao wanatarajia kugombe ubunge kwa tiketi ya CDM 2015?
   
 11. Q

  Quick Senior Member

  #11
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mimi nikimsikia huwa napata kichefuchefu,anafaa kufanya mijadala kilabuni..na hiyo TV station nilishaacha kufatilia habari habari zake.,
   
 12. P

  Paul Mabuga Verified User

  #12
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nachoamini ni kuwa changamoto ni jambo la kawaida kwa binadamu! Kwangu mimi hakuna hoja ya kipuuzi. Lakini pia binadamu kutofautiana katika fikra ni jambo la kawaida, fikra zinajengwa na misingi minigi, baadhi ni pamoja na Imani, utashi na uelewa. Siwezi kuhukumu kipi kinawasukuma baadhi kutoa hoja na maoni waliyonayo, lakini ni mara chache misingi hii ikafanya katika hali ya usawa na kwa pamoja,lazima msingi mmoja utakuwa juu zaidi ya mingine. Kama binadamu pia kuna hatua za kujifunza katika jambo, kwanza naona, Napata uzoefu, maarifa mapya kama yapo na kisha napambanua, na hii ni lazima.
  Kuibuka na fikra na kushtumu ama kulalamikia jambo ambalo una uewlewa nalo ama huna pia siyo dhambi, lakini uendeshaji na utayarishaji wa vipindi vya majadiliano una misingi na maadili yake. Unaweza kufanya kama wengine wanavyotaka uwafurahishe, nap engine fikiria ukifanya kuegemea upande mwingie kuwauzi hali itakuwaje. Lakini fikiria ukaendesha mjadala ambao wageni wako wengi wa upande mmoja, lakini unatakiwa kuwa na muungwana akilalamika kwa sababu umeuliza jambo ambalo yeye linamkirihisha.
  Najua kwa nini zinakuwepo hoja kama zinazotolewa, lakini naziheshimu na nachukua kama changamoto.
  Pengine ni nadra kwa mtu kujibu wazi malalamiko kama hivi, lakini nawapeni hongera mnaotoa malalamiko, wengine nawafahamu na wengine siwajui lakini Shukurani na Kwaresma njema.
   
 13. M

  Mutakyamirwa JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 4,873
  Likes Received: 334
  Trophy Points: 180

  Ndugu,

  Let's be realistic. Napenda watu wanaoongea 'ukweli'. Na-support mtoa mada. Analysis yangu kwa mtangazaji huyo ni kama hii:

  1) Yeye uanzisha swali na kisha utakarijibiwe anavyotaka yeye
  2) Uingilia muongeaji kabla ya kumaliza hoja/points zake
  3) Uteka mjadala-yaani uongea yeye mda mlefu badala ya walioalikwa kuongea
  4) Ufanya reference nyingi za wanasiasa wakati mwingine zisilenge mada yenyewe.

  Nahisi ni mmoja wa wanaoona kuwa mambo yanaenda vizuri nchini-yaani watanzania wanamaisha bora kama ilivyotangazwa/ilivyo-slogan ya JK.

  Kwa ujumla nachukia watangazaji vibaraka na wenye uwezo mdogo wa kuuliza maswali. Na zaidi nawaogopa watangazaji kama hawa kwa sababu nia zao sionzuri kwa taifa.
   
 14. m

  mbeshere Member

  #14
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 66
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Makanjanja sijui alisomea wapi huo uwandishi is not competent on what is doing!!
   
 15. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #15
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nimefuatilia mjadala huu, lakini hapa nachoona ni ushabiki wa kichama! Aanacholaumiwa huyo mtangazaji ndicho ambacho baadhi yenu mnakifanya. Inaelekea uchadema umewakolea. lakini pia ukanjanja nauona hata katika kuchambua mambo. Mimi namjua huyu mtangazaji ni mweledi na kazi yake wananchi wengi wanaiukubali kwamba inaelimisha mno. Lakini nimepitia pia mijadala ya awali lakini pia inaelekea walalamikaji ni wanachadem,a damu yaani hawajifichi. Hebu fikiria mtu anakaribia kutukana eti kwa sababu tu hoja anayoiwazia imepimwa katika hoja za mtangazaji. Mimi nimekiona kipindi na kwa kweli kilikuwa cha manufaa sana, Sheria ya uhaini imejadiliwa na inaonekana CDM siyo wahaini hali kadhalika uchochezi nao ikaonekana siyo na mambo mengi tu. lakini hakuishia hapo akahoji dhdmira ya cdm kuhusu kutetea maslahi ya wananchi wakati wanalamba za mili.

  Nimefuatilia na sasa naoma kama badala ya hoja kinacholetwa ni chuki binafsi, hata wachangiaji wenyewe ukiona wanachozungumza utawajua ..hata kiwango chao cha kutafakari mambo.

  Kuweni wakweli
   
 16. Tumaini Jipya

  Tumaini Jipya JF-Expert Member

  #16
  Mar 11, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  <br />  MABUGA PAUL,HAPA SWALA SIO WEWE KUULIZA MASWALI KUFURAHISHA AUDIENCE FULANI,WALA HAPA ISSUE SI TU WELEDI WA UANAHABARI LAKINI HATA STADI ZA MAWASILIANO HAUNA!!
  KWA KAWAIDA HAUWEZI KUMKATIZA MTU WAKATI ANAJIBU SWALI ULILOMUULIZA WEWE MWENYEWE!!
  KAMA MWANAHABARI UPO HURU KUUNGA MKONO CHAMA CHA SIASA UNACHOKIPENDA WEWE LAKINI UNAPOKUWA KAZINI HAKIKISHA UNAKUWA NEUTRAL!!
  Az for u,upo biased kiasi hata mtu mwenye akili nzito anaweza kutambua kirahisi kabisa!!
  Mimi ni mtazamaji wa kipindi hichi mzuri sana,kwa mfano leo Umemkatishakatisha sana Bwana Greyson,it was very obvious!!

  Sisemi kwamba uwaachie wachangiaji hata pale wanapotukana,No,lakini usizue mchangiaji kama anavyofanya Ana Makinda!!
  Nafikiri haitoshi kujibu kisiasa kwamba u take it as a challenge,kimsingi unahitaji kubadilika or otherwise itakuwa busara urudu darasani ujifunze MAADILI YA UANAHABARI!!
  Mwambie Yahaya,Mwaleko au hao waandeshaji wengine huwa wanatumia mbinu gani kuhakikisha mapenzi yao kwa chama fulani doesnt get in the way of their running the show!!
  U are such a COWARD and CHEAP!!!
   
 17. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #17
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Siyo kweli kabisa Tumaini Jipya! Una ushabiki naona! Mimi nimeona hiki kipindi baada ya kupigiwa simu na jama yangu nisikose kukiangalia. Mambo mapya nay a ufafanuzi yamezungumziwa vema hata yale ambayo nilikuwa siyajui na nilishuhudia &#8211; effective communication. Niliona pia hata wakati anamkatiza mshiriki aliyekuwa akianza kujadili hoja --- ilikuwa dhahiri mshiriki alipotoka na kuanza kuzungumzia personality akimzunguza Kikwete kama mtu binafsi badala ya hoja, sikusumbuka sana kwenye hilo. Kuna rafiki yangu mmoja aliwahi kuniambia endapo mahojiano yangekuwa yanaendeshwa namna ile na mtangazaji kuhoji katika namna inayojibu maswali ya wananchi ikiwepmo hoja za pande mbili ingekuwa shwari. Tatizo tumaini jipya na wenzako ni ushabikiiii.
   
 18. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #18
  Mar 11, 2011
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...hivi hujishangai kuwa mpaka sasa ni wewe peke yako humu ndani ya nyumba unayemtetea huyu Kanjanja?? Ama ni Wewe?? Ni aina ya watu kama nyinyi msioona ukweli mnaotufanya tushindwe kuondoa takataka zinazokwamisha maendeleo ya nchi yetu.Tafakari.
   
 19. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #19
  Mar 11, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  BabaDesi angalia hoja ziwe na msingi, kwa sababu nifikiri hutafakari! kama unafanya hivyo basi kuna ukanjanja katika ubongo wako. Taizo ni ushabiki ambao mnaulalamikia dhidi ya mtangazaji wakati na ninyi ikiguswa CDM mnang'aka na kuwapaka majina ya ajabu watu wenye maoni tofauti na yenu. Jukwaa hili badala ya kuwa huru sasa inaelekea linatumika kujipambanua kitu ambacho hakikuwa hivyo miaka mitatu minne iliyopita. Hivi peleleza tangua imeanza thread hii --- dhana ya Great Thinkers -- imejitokeza kweli. sasa kimekuwa kijiwe cha majungu na kusukuma ajenda za watu kama wewe!
  hata na mimi unataka kunivanmia. Kama mmempania huyo jamaa. Basi naomba niishia hapa maana inaelekea hii ni vita na mimi nijiingiza kichwa kichwa.
   
 20. chuki

  chuki JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,691
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Paul Mabuga anaheshimika sana kwa wasikilizaji na wtazamaji wa vipindi anavyoendesha.
  wanaochukizwa na Mabuga ni wale ambao wanapenda kubebwa na kupata cheap populality kupitia vipindi kwenye redio,TV,na magazeti.
  na hao ni wale wenye mlengwa wa maandamano, tunawajua,hatuwashangai kwani hata huko kwenye "movements" zao wakiona watu wamejaa wanaita "nguvu ya umma" bila kujali hizo picha zitasambaa mitandao yoote as if 'hiyo' ndio Tanzania nzima.
  Mabuga piga kazi ndugu yangu,tunapenda vipindi vyako,vinachangamoto sana.
  kumbuka hakuna Msema ukweli asiyepitia Changamoto.
  BIG UP MABUGA.keep it up.
  Mtazamo wangu JF inageuzwa kuwa uwanja wa matapu tapu,
  nahofia GREAT THINKERS tumebaki wachache sana ndani ya JF,WENGI wanatumika,na kutumiwa na WAJASILIAMALI wa siasa.
   
Loading...