Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe

Paul Chizzi amuumbua Mwakyembe

Mtu kama Chizi siwezi kamwe kumuonea huruma. Tumeoneana huruma vyakutosha.
 
Chizi anafahamu sana anachokifanya, ameharibu akubali, aondoke akapumzike.Mwakyembe amezungumzia gharama ya uniforms ni $49,900, tena amesama wazi. lakini chizi kwa usanii wake na huyo mwandishi wanazungumzia bei ya uniform ni $18,000. bei na gharama ni vitu viwili tofauti, sasa sitegemei CEO apindishe tafsiri kati ya bei na gharama.
hao precision air walinunua uniform kwa bei kati ya $ 200 na $ 600 kwa kila mmoja. ATCL hata kama wangenunua kwa bai kama ya precision air, gharama ya ATCL kwa uniform zao bado ni juu , kwani wao (ATCL) walituma wafanyakazi wao kwenda kununua na walitumia siku 45 huko, so maisha yao huko yanaingia ktk gharama ya uniform.je precision air nao walituma watu china kwa siku 45?, kama wangefanya hivyo, si precision air ingeshakufa?. chizi ni mtu mzima ameharibu akubali. baadhi ya waandishi wetu nao ni waandishi uchwara, wana ripoti bila kuchunguza na kutafsiri wanacho ripoti
Mkuu mwalimu wako wa kiingereza ana laana, yaani maelezo yanajitosheleza na hadi gharama ya unit imeelezwa bado hujaelewa na unabisha...

Ninashauri sio lazima kuchangia mada kama hujaelewa, haya mambo ya aviation ni ya kitaalam, nyie mliotokea shule za kata kaeni pembeni wataalam walumbane.
Nenda jukwaa la lugha kajifunze kiingereza au hire a translator
 
Kuna watu huwa hawapendi kusikia taarifa kutoka pande zote, wanapenda kutoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja tu. wanamlaumu Chizi kusema kuwa angekaa kimya, jambo ambalo halipaswi kuwa hivyo kwani inahitajika waseme sana hadi watu watambue usahihi wa habari ukoje.

Chizi kafatwa na mwandishi wa bahari, ambaye nampongeza sana kwani aliona haipaswi kusikia habari ya upande mmoja na kujiridhisha kuwa ndo usahihi wenyewe hivyo akafanya jitihada za kutafuta taarifa za upande wa pili.

Na kuna asilimia ya watu humu ndani pia wanakimbilia kutoa maoni hata bila kusoma taarifa yote ya mwandishi kwa kutumia yale ambayo walikuwa wanayafahamu kabla, jambo ambalo pia si sahihi kwa watu wanaojiita magreat thinkers.

Chizi anasema uchunguzi wa suala hili ulishafanyika na ripoti ikaandikwa juu ya tuhuma kama hizi tunazozitoa, suala ni Je, Mwakyembe katoa maamuzi kutokana na hii report, au report hii haiamini na ndo maana anachunguza upya suala hili linalosemekana kuwa lishafanyiwa uchunguzi?

Waandishi wa habari endeleeni kuwachokonoa hawa wadau wa habari hii hadi taarifa zote ziwe wazi ili umma ujue kwa ufasaha, na ikiwezekana muitafute hiyo report na itundikwe hadharani tuone inavyomfunga Chizi na pia tuangalie kama ilichakachuliwa ili impendelee Chizi.
 
Kama aliyekanusha ana ushahidi basi Mwakyembe shule haijamsaidia au nitaamini kuwa hata ukiwa msomi na intergrity yako ukiingia CCM unakuwa juha .

Kwa wataalamu wa manunuzi huyu bwana alijuaje kama procurement from china ilkuwa ni cheap? je anaweza kutuambia ilikuwa ni ghari kulinganisha na kununua sehemu nyingine km Dubai, uk, US na etc? kama haikuwa local procurement International biding ilitawngazwa wapi? kama ni china peke yake ilipendekezwa ni makampuni mangapi kutoka china yalituma yalituma quotation? JE kununua kutoka china si kuangusha uchumi wa nchi? hata k tungenunua hapa hapa bongo pesa si ingebaki hapa bongo kwa Mtanzania?

Hivi mpaka bwn Chizi akumbushwe na mkuu wake kuwa pesa ile ya insurance ingeweza kununua ndege nyingie? basi nafai ile haikuwa sahihi kwake, km hawezi kutoka nje ya box kujua mambo kuliko kawaida.
 
Napata shida sana Kutamka Jina na huyu Mkurugenzi aliyefukuzwa, Nashindwa pia kushangaa hata aliye mpa hiyo nafasi ndiyo maana hata haliyoyafanya sishangai sana coz jina lake speeks more Than words......
Hata wewe unatetea upuuzi wa Mwakyembe!!! Kweli nchi yetu ina safari ndefu sana kufikia maendeleo maana asilimia kubwa mnahitaji heater za kuchemsha akili. Chizi ameact professionally, Mwakyembe ame act ki layman, halafu mwakyembe ndio shujaa kwenu. Stupid.
 
kwani hizo dola 18,000 ni kidogo? wakati shirika halina hata ndege moja? Tusiwaonee haya wahalifu kama hawa ni hatari kwa nchi yetu

Hiyo ni kama Tzs.28,800,000/= ,ki ukweli wazingeweza kufanya kazi bila uniform sasa kinachotakiwa ni tujue hii hela ilinunua uniform ngapi? vilie vile na kama PPRA walishafanya uchunguzi na kugundua deal ilikuwa fair kwa maana ya (VFM) sasa haya ya Mwakwyembe yanatokana na uchunguzi upi na ulifanywa lini?
 
Si ajabu anaitwa chizi....utatumiaje dola 18,000 kushona nguo ambazo zaweza shonwa kwa batiki za hapa hapa na hata Millioni 2 isifike.....

Kwanza soma gazeti uone hoja zake before jumping into a Band Wagon. Mlishangilia sana Mwakyembe alivyopiga siasa kwenye vyombo vya habari kwenye jambo la kiadministrative sasa mnakuwa wakali.
 
Hate wewe mkuu bado shule inakusumbua, hapa kuna taaluma zaidi ya aviation, kuna maswala ya uchumi, uhasibu na ugavi. mfano huwezi kufanya international procurement bila kutangaza kimataifa local ukalinganisha. je tangazo la zabuni lilitangzwa kwenye gazeti gani hapa nyumbani km PPRA inavyotaka?

Hhivi kwa akili ya kawaida huwezi kujua kuwa pesa ya gari lililopata ajari ikilipwa na bima inakupa gari jipya km bima yako ni Comprehensiv? bwana chizi hakujua km pesa ya bima ingeweza kusaidia kupata ndege nyingine? na hii ya kukodi ikajipa yenyewe? huu ni upuuzi na utetezi usiokuwa na tija. kama china huyu bwana tungemsahau. lkn kwa kuwa bongo ni kulindana ndiyo maana hata huyu chizi anapata nafasi ya kuongea bila wasi wasi.
 
Hata wewe unatetea upuuzi wa Mwakyembe!!! Kweli nchi yetu ina safari ndefu sana kufikia maendeleo maana asilimia kubwa mnahitaji heater za kuchemsha akili. Chizi ameact professionally, Mwakyembe ame act ki layman, halafu mwakyembe ndio shujaa kwenu. Stupid.

Mkuu am not side with none of the names mentioned.Sorry!
 
Sijasoma yote nitasoma baadaye lakini huu ni wizi na uhuni. Amekansha nini sasa hapo kihusu uniform? Anasema hela zingine zilitumika kununua other materials; yapi? Uhuni tu. Hivi angekuwa mbunifu si angewapa wanamitimdo wetu washone nguo zinazofanana fanana na Tanzania badala ya kukimbilia China. Ati CEO hivyo ana mandate; mandate y wizi?
Ukisoma kati ya mistali inaonesha walifuata taratibu na sheria za manunuzi hivyo tatizo kubwa linalotutesa ni hiyo sheria ya manunuzi PPRA.
 
Aliyekuwa mtendaji mkuu wa ATCL ameibuka na kusema kwamba Dr Mwakyembe alidanganya umma kutokana taarifa alizopewa kuwa ni za uongo na zisizokuwa na ukweli wowote.

Kwa mfano uniform ziligharimu dola 18,000 tu na sio dola 50,000 kama alivyosema mwakiembe, Bwana Chizi alisema pia tatizo ni kwamba kuna watu hawajui chochote kuhusu sekta ya anga lakini wanajidanganya kuwa wanajua mbele ya umma.

Chanzo: The Guardian on Sunday



Kuna watu 10 % walizozoe ziliwapita ndio maana wana hasira,we unafikiria ukiweka ka 10% kwenye mkataba wa kukodisha ndege ni hela ngapi? ndio maana wizarani wanataka kila kitu kipitie hapo wakamue chao. Hii nchi ukiwa msafi tabu sana haufiki mbali mafisadi ndio wanakumbatiwa.
 
Ukisoma kati ya mistali inaonesha walifuata taratibu na sheria za manunuzi hivyo tatizo kubwa linalotutesa ni hiyo sheria ya manunuzi PPRA.

Aliwatuma akina mama wawili waliokaa China siku 45 wakisubiri hizo uniform ($400x2x45days=$36,000). Hili hajalizungumzia
 
Mkuu Kichuguu sijui kama unachochangia unakielewa. Kashfa ya Airbus imezungumzwa sana hapa miaka ya nyuma. Sasa inakuaje unamuhusisha Chizi?
Kuna taarifa za kutosha kabisa kuwa ndege ile ni bomu; ukitaka zaidi wewe google ATCL+Liberia+Airbus. Ingawa ni kweli kuwa deal lile lilianza zamani wakati wa Makatta, huyu mheshimiwa angekuwa ni mtaalamu na mwenye nia njema na shilika, ni wazi kuwa asingesukumiza dili hilo liendelee, angelilipiga stop. Kuna kila dalili za kutia shaka kuwa huenda kabla ya kustaafu kwake, alikuwa ni mmoja waliokoleza dili hilo, na alipopewa mwanya tu basi akalisukumiza kwa nguvu zote lifanikiwa.
 
Kama ni hivi Chizi anachemka kwa kujitetea kwenye magazeti. Naanza kuwa na wasiwasi naye coz naona waandishi wengi wanakimbilia kumtetea badala ya kusubiria akajitetee pale Kisutu mahakamani..

Kuna uwezekano mkubwa mahakamani akashinda, dalili zimeshaanza kuonekana kuwa ameondolewa kwa zengwe la CCM na mafisadi wake.
 
Aliyekuwa mtendaji mkuu wa ATCL ameibuka na kusema kwamba Dr Mwakyembe alidanganya umma kutokana taarifa alizopewa kuwa ni za uongo na zisizokuwa na ukweli wowote.

Kwa mfano uniform ziligharimu dola 18,000 tu na sio dola 50,000 kama alivyosema mwakiembe, Bwana Chizi alisema pia tatizo ni kwamba kuna watu hawajui chochote kuhusu sekta ya anga lakini wanajidanganya kuwa wanajua mbele ya umma.

Chanzo: The Guardian on Sunday




Anasema nini huyo sasa? kama $18,000 ndio za nguo, ok tufanya staff wawili walikwenda kuzisubiri kwa siku 45, fanya wawe wameripwa per ya chini kabisa serikarini kwa safari za nje ambayo ni $320 X 2 X45 ni $28,800 +$18,00=$46,800


Kwa mchanganuo huu bado anabisha?
 
Huyu bwana asijitetee amefanya hujuma dhidi ya shirika la ndege. kwanini alituma watu kununua sare ulaya badala ya kutangaza tenda?taratibu za manunuzi za umma zinajulikana ,kwanini alizikiuka? hafu zile nguo zina thamani hiyo kweli? hao aliowatuma aliwalipa fedha shs ngapi?shaka yangu ni kwa watu wanao mtetea,kuna nini nyuma ya pazia wakati madudu aliyo ya fanya yako wazi?watanzania bwana!!!!!

Soma gazeti upya uone kama tender haikutangazwa halafu urudi JF.
 
Mwakyembe kama kweli ni muungwana na mpenda nchi yako. Hapa imekupuruchuka OMBA RADHI kwa Chizzi na jamii nzima ya waTz kwa yaliyotokea.
 
Mbona anaye kanusha ana zungumzia TUMBONI...! aite press achambue hizo hayo madai sio mwandishi amfuate amuombe kuelezea!.... BIG UP MWAKYEMBE
 
majina mengine siyo ya kuwaita watoto. yani watu wanaenda kula maisha kwa siku 45 huko hong kong, kisa wanatafuta jezi?? Duh, mbona hata magari tunaagiza tukiwa hapa hapa bongo na yanatufikia bila mtu kwenda japan?? huyu Paul Chizzzi naye ni chizi kweli kumbe
 
Back
Top Bottom