Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

Mimi ni mangi orijino, najua inavyouma kulipa deni...huyu mangi mwenzangu yataweza yakafumuka Mengi zaidi. Dola mil.8 waungwana sio kitu kidogo, kwa alivyoanza sidhan Kama kuna Benk iliyokuwa tayari kumpa hizo dola mil.4. Huyu mangi alitumika. Time will tell.
No hio usd 4mil ilikua ni mfano kuonyesha jinsi gani isivyo rahisi kulipa madeni
 
Hivi kwanini watanzania wanapenda kuona mtu anafail.!?hii pia nmeiona kwenye hotuba za raisi pale anaposemaga matajiri atawashusha wawe kama raia wengine huwa watu wanashangilia sana..huku mitaani ndo balaa ukifanikiwa watu kidogo tu figisufigisu kibao na kashfa za kijingajinga.

Sidhani kama watu wanachukia watu kufanikiwa.Kwako kufanikiwa ni kupi maishani? Ni ile kufanya lolote ili mradi malengo yanafikiwa? Wachangiaji wanajiuliza tu imekuwaje kwa hatua aliyofikiwa haya yakajitokeza? Sio kama watu wanashangilia kuanguka kwake.Hivi Chukulia mfano wa Masamaki wa Bandarini.Unafikiria isingekuwa Magufuli labda watu tungekuwa tunajua kuwa jamaa pamoja na ajira yake lakini ana biashara nyingine nzuri inayomlipa.Kumbe hali ni tofauti.Biashara ina mambo mengi sana.
 
Amekuwa akialikwa kwenye makongamano mbalimbali ya vijana kama kijana aliyefanikiwa Sana. Yale mabilioni yote tunayoambiwa anayo yameyeyuka? Yaan mpaka bank wakuweke kwenye list ya defaulters ujue umeshindwa kulipa kwa Muda mrefu na efforts nyingi zimetumika lakini umeshindwa. Kuna jambo la kujifunza hapa, Nini kimepata huyu ndugu?
Kama alipata hela kwa kufunga mitambo kwenye kambi ya wakimbizi ujue hiyo hela imeshuka sana kwani asipopata tender nyingine ndiyo kwishneyi. Mi nilifikiri anatengeneza vifaa vya solar
 
Uongo mtupu labda kama unamaanisha NBC lkn kwa STANBIC ni uongo

Kweli nimeongopa,haikua STANBIC Bank ilikua ni NBC kama ulivyosema,Bahati mbaya nilikurupuka sikusoma hilo tangazo,mimi nilisoma tittle ya thread na niliangalia hiyo rangi ya tangazo nilivyoona ni bluu na nyekundu nikaunganisha kichwani mwangu kuwa ni NBC.Sorry for that,Lakini benki ilikua ni NBC mwishoni mwa miaka ya tisini.
 
mods bana tangu asubuhi uzi huu ulipoanzishwa hamuoni kama hii heading ya mtoa post imekosewa?au mko busy kuunganisha threads na kuedit maneno tunauopost kwenye posts zetu?
STAFF ONLINE NOW
 
Kama madeni anashindwa kulipa vipi kuhusu KODI?
Madeni ni tofauti na kodi,kwani kwenye kodi huku kuna namna nyingi za kufanya na kupata msamaha hasa kwa kipindi cha awamu ya serikali ilyopita ukizingatia kulikua na sheria nyingi zinazotoa misamaha ya kodi na kuna maafisa wa mamlaka ya kodi wasio waaminifu ambao mfanyabiashara anaweza kula njama nao na akakwepa kodi na mambo yakawa poa tu ,vilevile kuna mchangiaji hapo juu alizungumzia kuwa huyo bwana aliwahi kufanya biashara na UN nao ulikuwa ni mwanya mzuri kwa mfanyabiashara kuweza kukwepa kodi,tofauti na mkopo wa benki,kwani mkopo ni obligation unayotakiwa kuitimiza kwa utii na unyenyekevu mkubwakusudi usije kujiharibia in the future,kama ilivyotokea kwao sasani kwamba walishindwa kutii masharti yaliyomo kwenye mkopo,still anaweza kwenda creditor wake wakaongea na yakawapoa tu,wengi tu waliingia kwenye hali kama hiyo na wakaweza toka salama,japo waliingia kwenye fedheha ya kutaka kunadiwa dhamana zao.
 
Kweli nimeongopa,haikua STANBIC Bank ilikua ni NBC kama ulivyosema,Bahati mbaya nilikurupuka sikusoma hilo tangazo,mimi nilisoma tittle ya thread na niliangalia hiyo rangi ya tangazo nilivyoona ni bluu na nyekundu nikaunganisha kichwani mwangu kuwa ni NBC.Sorry for that,Lakini benki ilikua ni NBC mwishoni mwa miaka ya tisini.
Usijali Mkuu, sorry pia kama nimetumia lugha kali kwako. Ile inshu ya mkopo wa NBC sijui mzee aliimalizaje huko juu kwa juu.
 
Km kipindi cha kikwete ulikuwa unaweza kukopa na ukarudisha deni ki ulaini, ila si kipindi hiki, biashara zinakufa, mtu alikuwa na hotel na anapangisha kwa dola, sasa hivi mambo yamebadilika, na bado!
 
Madeni ni tofauti na kodi,kwani kwenye kodi huku kuna namna nyingi za kufanya na kupata msamaha hasa kwa kipindi cha awamu ya serikali ilyopita ukizingatia kulikua na sheria nyingi zinazotoa misamaha ya kodi na kuna maafisa wa mamlaka ya kodi wasio waaminifu ambao mfanyabiashara anaweza kula njama nao na akakwepa kodi na mambo yakawa poa tu ,vilevile kuna mchangiaji hapo juu alizungumzia kuwa huyo bwana aliwahi kufanya biashara na UN nao ulikuwa ni mwanya mzuri kwa mfanyabiashara kuweza kukwepa kodi,tofauti na mkopo wa benki,kwani mkopo ni obligation unayotakiwa kuitimiza kwa utii na unyenyekevu mkubwakusudi usije kujiharibia in the future,kama ilivyotokea kwao sasani kwamba walishindwa kutii masharti yaliyomo kwenye mkopo,still anaweza kwenda creditor wake wakaongea na yakawapoa tu,wengi tu waliingia kwenye hali kama hiyo na wakaweza toka salama,japo waliingia kwenye fedheha ya kutaka kunadiwa dhamana zao.
ok
 
Usijali Mkuu, sorry pia kama nimetumia lugha kali kwako. Ile inshu ya mkopo wa NBC sijui mzee aliimalizaje huko juu kwa juu.
Wala usijali bro,kwa kuwa hata mimi kutokana ukosoaji wako nimejifunza kitu,kwamba nisiharakie kuandika kitu bila kupitia details kwa umakini,kuhusu mzee nadhani alimaliza ile issuemaana kuna wakati hii issue kama ilitaka kuibuka tena mwanzoni mwa miaka ya 2000,lakini akajitokeza na kukana kwamba hadaiwi,so nadhani aliimaliza.
 
Shida ni kwamba vyombo vya habari vilimkuza sana, labda ndipo mabenki yalipoona anakopesheka.
Mkuu mabenki hayamkopeshi mtu eti kwa sababu anatangazwa sana na vyombo vya habari, la hasha,mabenki wanachoangalia wao je?huyu mtu anakopesheka? au kwa english wanauliza is he credit worth? basi.

Wakishakuona kwamba unakopesheka sasa ndio wanaangalia thamani ya mkopo wa kiasi gani?,na baada ya hapo taratibu zingine zinaendelea ili uweze kupewa huo mkopo,lakini sio jina tu likufanye wewe upate mkopo NO wanaangalia financial statement yako inasomaje Mkuu.
 
Wala usijali bro,kwa kuwa hata mimi kutokana ukosoaji wako nimejifunza kitu,kwamba nisiharakie kuandika kitu bila kupitia details kwa umakini,kuhusu mzee nadhani alimaliza ile issuemaana kuna wakati hii issue kama ilitaka kuibuka tena mwanzoni mwa miaka ya 2000,lakini akajitokeza na kukana kwamba hadaiwi,so nadhani aliimaliza.
Aisee pamoja Sana bro, kwenye miaka ya 2000's hapo Kipindi kile mzee amekorofishana na wakina Rostam Aziz, Jeetu Patel nakumbuka waliifufua hio inshu ya NBC ikabid mzee ajitetee
 
KUKOPA RAHA SANA ILA SUALA LA KULIPA DENI NDO ISHU KUBWA HAPO
NGOWI ATAWEZA AJITIE NGUVU AONGEE NAO WADENI WAKE ILI AWEZE KULIPA KIDOGOKIDOGO
 
Aisee pamoja Sana bro, kwenye miaka ya 2000's hapo Kipindi kile mzee amekorofishana na wakina Rostam Aziz, Jeetu Patel nakumbuka waliifufua hio inshu ya NBC ikabid mzee ajitetee
Yah! kitu kama hicho,inawezekana kwa kuwa wale ni wafanyabiashara wakubwa wenzake wanajuana,lakini yule mzee ni mafia nadhani ile ishu aliimaliza kiutu uzima na wakuu,kwani ilikua inafahamika wazi,wadaiwa sugu wa ile benki ni wakina nani,na kipindi hicho mambo hayo yanaanza ndio kipindi ambacho NBC inataka kununuliwa na ABSA kwa hiyo inabidi madeni yakusanywe kusudi ifanywe tathmini ili igawanywe mara mbili na kuwa NMB so wadaiwa ni kina nani sasa hapo ndo kasheshe ilipoanzia,ndo hivyo lakini siku zinaenda na mambo yametulia na mzee anadunda.
 
Kukopa na kidaiwa ni kawaida sana kwa wafanya biashara. Nikuambie siri ni kuwa unaweza ukawa umekopa say 500m bank kuzungusha katika biashara na marejesho ya mwezi say ni 30m lakini ukizungusha hii hela unapata faida kubwa sana say 100m a month. Ninakuambia mkopaji yuko radhi kuharibu mzunguko wa marejesho ili kufaidi hela. Kwa misingi hii raha ya mkopo inakua tu pale mkopajia napoweza kuwa na biashara inayotoka haraka na kuleta fedha nyingi. Kwa hiyo basi huyu Ngowi wala msiseme kafilisika. Ninakataa kabisa kwa nimjuavyo mimi ila ni mjanja sana. Na wengine tumepitia mbinu hizo hizo za madeni japo mwisho wa siku tunalipa ila tukiwa tumeshapata faida kubwa sana pia. Shida si kukopa, shida ni kupata mradi sahihi unaozalisha kwa wingi na kwa haraka.
ukitolewa kwenye gazeti jua huyo ni mdaiwa sugu na bank wamejaribu kila njia imeshindikana na ni deni la muda mrefu sana..huyo ngowi ameshindwa kulipa...
 
pengine amefanya strategic default. unaacha kulipa baada ya kuona dhamana hailingani na pesa unayodaiwa.
dhamana ya mkopo daima thamani yake inakuwa ni kubwa kupita kiwango cha mkopo unaopewa....
 
Kwa mfanyabiashara wa aina yake na kwa mazingira ya jinsi mabenki yanavyofanya kazi siku hizi na kwa kuzingatia kuwa yeye tayari ni International Business Figure hawezi kukubali ku-defame jina lake kiasi hicho.Kuna jambo kubwa lipo nyuma ya kile kilichokuwa kinasababisha yeye apate ukwasi huo.
Je kama amewekwa kimakosa?

Namfahamu muhanga mmoja wa hilo. Benki walikosea hesabu za riba na makato ya jumla. Na aliwataarifu rasmi. Hawakuchukua hatua. Wakamtoa kwenye gazeti na picha kabisa. Sasa wanapambana kulipa mamilioni kwa mamia. Hawakujua ni mtu mwelewa sana na aliwaacha wajikaange.

Huyo Patrick Ngowi ndo huyo huyo wa Helvetic? Anadaiwa kias gani? Kuna mengi ya kujadili
 
Hivi kwanini watanzania wanapenda kuona mtu anafail.!?hii pia nmeiona kwenye hotuba za raisi pale anaposemaga matajiri atawashusha wawe kama raia wengine huwa watu wanashangilia sana..huku mitaani ndo balaa ukifanikiwa kidogo tu figisufigisu kibao na kashfa za kijingajinga.
Mmojawapo pia ni huyo Bwn. Sanctus. Km ndo yuleyule wa kuhamasisha vijana na ndio mawazo yake, basi tuna safari ndefu sana kuwa na fikra na matendo ya kikwasi.
 
Back
Top Bottom