Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

Huyo uliyemtaja mwenyewe kuna kipindi alikua anadaiwa na benki hiyo hiyo sijui sakata lake liliishia wapi.
Uongo mtupu labda kama unamaanisha NBC lkn kwa STANBIC ni uongo
 
MK
By the way nitajibu hapo penye maandishi mekundu, kwa sababu pananihusu kiasi fulani.
Niko kwenye sekta ya nishati jadidifu kitambo sana, miaka 15 na kidogo. Huyu bwana ni mjasiriamali mzuri sana kwenye suala la umemejua (solar), ambako alitapa tenda kadhaa za UN, kufunga umemejua kambi za wakimbizi. Huko ndiko alikoanzia hizo fortune zake na kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors. Then baadae mwaka 2013 akaingia kwenye rekodi za jarida la Forbes kama milionea kijana, makala iko HAPA. Ndipo macho ya Watanzania wengi yakaanza kumuona na kumpa headlines kwenye magazeti na social media. Infact ni kati ya vijana wachache wenye mafanikio, ingawa kwa tunaoifahamu biashara ya solar (imeingiliwa sana na Wachina tangu 2000) kwa hapa Tanzania ilitupa mshituko kidogo kwamba inawezedkanaje kutengeneza mshiko mrefu kiasi kile (dola 8 milioni) ndani ya muda mfupi ule, kwa sababu soko la solar ni gumu kwa hapa kwetu.
Sasa nashangaa leo kawekwa kwenye orodha ya wadaiwa wa benki! Mtu mwenye 8 million dollar business anashindwaje kulipa mkopo wa benki?
Tuendelee kujadiliana.

Mkuu hili bandiko linaweza kuleta mjadala mzuri sana kwenye sekta ya ujasirimali Tanzania.Mimi mwenyewe nilipata habari za huyu jamaa mwaka 2013 kwa mara ya kwanza kwenye Gazeti la the Citizen kama sikosei tena kwa kuambiwa na Mnyika ninunue Gazeti hilo ili nisome stori ya huyo jamaa mintarafu alivyoweza kufanikiwa tena eti kwa kuanzia mtaji kidogo sana!

Sikuamini kama kweli jamaa ameweza kupata utajiri kiasi hicho kwa biashara hiyo tu.Mimi namfahamu rafiki yangu mmoja ambaye alianza biashara ya Solar kama hiyo ya Ngowi siku nyingi miaka ya 2000,Kampuni ya REX ENERGY,lakini mbona sijapata kuona amepata ukwasi kama huo wa Patrick!Nilisema muda utasema maana matajiri wengi wana siri nyingi zilizo nyuma ya utajiri wao.

Utawala wa Magufuli juzi ndio umenifumbua macho nijue kuwa kumbe watu wengi wanaoonekana wana ukwasi wa kutupwa wametengeneza pesa nyingi nje ya Circles za Profit Margins za kawaida.Pengine jamaa yetu naye ameathiriwa na Mtandao wa Magufuli.
 
Kama mtu ana usd 8mil na akawa anadaiwa usd 4mil unadhani ni rahisi kiasi hicho kuilipa? Point yangu ni kwamba Usd 8mil sio big deal, big deal nikujua anadaiwa fedha kiasi gani!
Mimi ni mangi orijino, najua inavyouma kulipa deni...huyu mangi mwenzangu yataweza yakafumuka Mengi zaidi. Dola mil.8 waungwana sio kitu kidogo, kwa alivyoanza sidhan Kama kuna Benk iliyokuwa tayari kumpa hizo dola mil.4. Huyu mangi alitumika. Time will tell.
 
Si alisema alianzisha biashara yake kwa mtaji sijui wa kuuza simu alipokua kwenye lile sijui kongamano la fursa pale Diamond ,wakati Helventic Solar Contractors sijui walikua ubia na mzungu gani akamchinjia baharini
 
Si alisema alianzisha biashara yake kwa mtaji sijui wa kuuza simu alipokua kwenye lile sijui kongamano la fursa pale Diamond ,wakati Helventic Solar Contractors sijui walikua ubia na mzungu gani akamchinjia baharini
anadaiwa sh ngapi
 
Mara nyingi matajiri wanataka kukopa,kuzungusha mkopo,kupata faida na kisha kurejesha Deni baada ya kutoa faida! Hiyo haina maana kuwa akaunti yake imekauka hapana,ni maamuzi ya kibiashara tu.
Kama ni ivyo angelipa, mpaka kuwekwa defaulters, yaan hadi kwenye credit bureau amechafuka, why akubali kujichafua na kuonekana kwenye magazeti? Kuna something wrong hapa lazima tukubali..
 
Kama ni ivyo angelipa, mpaka kuwekwa defaulters, yaan hadi kwenye credit bureau amechafuka, why akubali kujichafua na kuonekana kwenye magazeti? Kuna something wrong hapa lazima tukubali..
nasikia ukiwekwa huko hukopesheki tena popote
 
mkopo wa benk ni dhambi na haramu kubwa
ni kama uzinzi uchawi nk ni shirki huwa nashangaa makanisa yana benk eti dini nyingine jamani
 
Kama ni ivyo angelipa, mpaka kuwekwa defaulters, yaan hadi kwenye credit bureau amechafuka, why akubali kujichafua na kuonekana kwenye magazeti? Kuna something wrong hapa lazima tukubali..

Kwa mfanyabiashara wa aina yake na kwa mazingira ya jinsi mabenki yanavyofanya kazi siku hizi na kwa kuzingatia kuwa yeye tayari ni International Business Figure hawezi kukubali ku-defame jina lake kiasi hicho.Kuna jambo kubwa lipo nyuma ya kile kilichokuwa kinasababisha yeye apate ukwasi huo.
 
Hivi kwanini watanzania wanapenda kuona mtu anafail.!?hii pia nmeiona kwenye hotuba za raisi pale anaposemaga matajiri atawashusha wawe kama raia wengine huwa watu wanashangilia sana..huku mitaani ndo balaa ukifanikiwa kidogo tu figisufigisu kibao na kashfa za kijingajinga.
 
Wafanya biashara walio wengi wana madeni si suala la kushangaa sana,laiti kama vitabu vya wafanya biashara wote vinawekwa wazi kwa matumizi ya umma mngeshangaa hao mnaowaita mabilionea walivyo na madeni ,ndivyo biashara zilivyo sio jambo la kustaajabu sana,hata bilonea Trump alishapitia msukosuko kama huo na baadae kuibuka upya all the way hadi sasa anagombea uraisi wa Amerika ,kwa hiyo hata bilonea wetu kijana nae anaweza kuyaepuka haya kama atakaa chini na wakopeshaji wake na kupanga ni kwa namna gani ataweza kurejesha mkopo ili aweze kuendelea na biashara zake,kwani kwa sasa inabidi awe makini kwa kuwa kuna kitengo kilianzishwa kinaitwa credit bureau sina uhakika kama kimeshaanza kazi tayari na kazi ya kitengo hichi ni ku deal na madefaulter wote katika taasisi mbalimabali za fedha ambapo hutoweza kukopa mpaka uwe umeshalipa madeni ya awali kwenye taasisi zingine kwa maana usidhani ukikopa NMB ukakimbia uende Barclays utapata mkopo NO ,ukienda huko utakuta taarifa zako wanazo wanakwambia kalipe NMB kwanza halafu ndo uje kukopa kwetu,Mungu amsaidie huyu kijana aweze kumaliza shida hizi salama kwani alikua mfanokwa vijana wengine.
Kama madeni anashindwa kulipa vipi kuhusu KODI?
 
Kukopa na kidaiwa ni kawaida sana kwa wafanya biashara. Nikuambie siri ni kuwa unaweza ukawa umekopa say 500m bank kuzungusha katika biashara na marejesho ya mwezi say ni 30m lakini ukizungusha hii hela unapata faida kubwa sana say 100m a month. Ninakuambia mkopaji yuko radhi kuharibu mzunguko wa marejesho ili kufaidi hela. Kwa misingi hii raha ya mkopo inakua tu pale mkopajia napoweza kuwa na biashara inayotoka haraka na kuleta fedha nyingi. Kwa hiyo basi huyu Ngowi wala msiseme kafilisika. Ninakataa kabisa kwa nimjuavyo mimi ila ni mjanja sana. Na wengine tumepitia mbinu hizo hizo za madeni japo mwisho wa siku tunalipa ila tukiwa tumeshapata faida kubwa sana pia. Shida si kukopa, shida ni kupata mradi sahihi unaozalisha kwa wingi na kwa haraka.
 
Back
Top Bottom