Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

cerengeti

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2011
Posts
3,879
Reaction score
1,634
Jamani nilikuta kwenye gazeti la mwananchi la leo Ijumaa tarehe 5 agosti 2016.
1470382940897.jpg
 
Kukopa huwa raha sana ila wakati wa kurejesha huwa mchungu sana...Na ukute pesa uliyoichukua umeingiza mahali na ikazamia huko yote..huwa ngumu sana...BTW Patrick ni nani?
By the way nitajibu hapo penye maandishi mekundu, kwa sababu pananihusu kiasi fulani.
Niko kwenye sekta ya nishati jadidifu kitambo sana, miaka 15 na kidogo. Huyu bwana ni mjasiriamali mzuri sana kwenye suala la umemejua (solar), ambako alitapa tenda kadhaa za UN, kufunga umemejua kambi za wakimbizi. Huko ndiko alikoanzia hizo fortune zake na kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors. Then baadae mwaka 2013 akaingia kwenye rekodi za jarida la Forbes kama milionea kijana, makala iko HAPA. Ndipo macho ya Watanzania wengi yakaanza kumuona na kumpa headlines kwenye magazeti na social media. Infact ni kati ya vijana wachache wenye mafanikio, ingawa kwa tunaoifahamu biashara ya solar (imeingiliwa sana na Wachina tangu 2000) kwa hapa Tanzania ilitupa mshituko kidogo kwamba inawezedkanaje kutengeneza mshiko mrefu kiasi kile (dola 8 milioni) ndani ya muda mfupi ule, kwa sababu soko la solar ni gumu kwa hapa kwetu.
Sasa nashangaa leo kawekwa kwenye orodha ya wadaiwa wa benki! Mtu mwenye 8 million dollar business anashindwaje kulipa mkopo wa benki?
Tuendelee kujadiliana.
 
Kama mtu ana usd 8mil na akawa anadaiwa usd 4mil unadhani ni rahisi kiasi hicho kuilipa? Point yangu ni kwamba Usd 8mil sio big deal, big deal nikujua anadaiwa fedha kiasi gani!
 
By the way nitajibu hapo penye maandishi mekundu, kwa sababu pananihusu kiasi fulani.
Niko kwenye sekta ya nishati jadidifu kitambo sana, miaka 15 na kidogo. Huyu bwana ni mjasiriamali mzuri sana kwenye suala la umemejua (solar), ambako alitapa tenda kadhaa za UN, kufunga umemejua kambi za wakimbizi. Huko ndiko alikoanzia hizo fortune zake na kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors. Then baadae mwaka 2013 akaingia kwenye rekodi za jarida la Forbes kama milionea kijana, makala iko HAPA. Ndipo macho ya Watanzania wengi yakaanza kumuona na kumpa headlines kwenye magazeti na social media. Infact ni kati ya vijana wachache wenye mafanikio, ingawa kwa tunaoifahamu biashara ya solar (imeingiliwa sana na Wachina tangu 2000) kwa hapa Tanzania ilitupa mshituko kidogo kwamba inawezedkanaje kutengeneza mshiko mrefu kiasi kile (dola 8 milioni) ndani ya muda mfupi ule, kwa sababu soko la solar ni gumu kwa hapa kwetu.
Sasa nashangaa leo kawekwa kwenye orodha ya wadaiwa wa benki! Mtu mwenye 8 million dollar business anashindwaje kulipa mkopo wa benki?
Tuendelee kujadiliana.
Asante kwa taarifa mkuu...Duh jamaa wapi alipojikwaa nakuanguka..maana huo mkwanja si wa kitoto kabisa..
 
Amekuwa akialikwa kwenye makongamano mbalimbali ya vijana kama kijana aliyefanikiwa Sana. Yale mabilioni yote tunayoambiwa anayo yameyeyuka? Yaan mpaka bank wakuweke kwenye list ya defaulters ujue umeshindwa kulipa kwa Muda mrefu na efforts nyingi zimetumika lakini umeshindwa. Kuna jambo la kujifunza hapa, Nini kimepata huyu ndugu?
 
Asante kwa taarifa mkuu...Duh jamaa wapi alipojikwaa nakuanguka..maana huo mkwanja si wa kitoto kabisa..
Sijui kajikwaa wapi ndg, ila wazoefu watakuja watueleze.
 
Cerengeti hebu tumia akili japo kidogo sura ya ngowi mchumi unaijua Na ya huyo imebandikwa ambacho hujui nini?
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mara nyingi matajiri wanataka kukopa,kuzungusha mkopo,kupata faida na kisha kurejesha Deni baada ya kutoa faida! Hiyo haina maana kuwa akaunti yake imekauka hapana,ni maamuzi ya kibiashara tu.
Sawia kabisa. Kingine ninachojifunza ni kwamba, mtu anaweza kuthanimisha dhamana yake aliyokopea, akiona thamani ni ndogo kuliko mkopo then anachia iende. Akili kumkichwa.
 
Wafanya biashara walio wengi wana madeni si suala la kushangaa sana,laiti kama vitabu vya wafanya biashara wote vinawekwa wazi kwa matumizi ya umma mngeshangaa hao mnaowaita mabilionea walivyo na madeni ,ndivyo biashara zilivyo sio jambo la kustaajabu sana,hata bilonea Trump alishapitia msukosuko kama huo na baadae kuibuka upya all the way hadi sasa anagombea uraisi wa Amerika ,kwa hiyo hata bilonea wetu kijana nae anaweza kuyaepuka haya kama atakaa chini na wakopeshaji wake na kupanga ni kwa namna gani ataweza kurejesha mkopo ili aweze kuendelea na biashara zake,kwani kwa sasa inabidi awe makini kwa kuwa kuna kitengo kilianzishwa kinaitwa credit bureau sina uhakika kama kimeshaanza kazi tayari na kazi ya kitengo hichi ni ku deal na madefaulter wote katika taasisi mbalimabali za fedha ambapo hutoweza kukopa mpaka uwe umeshalipa madeni ya awali kwenye taasisi zingine kwa maana usidhani ukikopa NMB ukakimbia uende Barclays utapata mkopo NO ,ukienda huko utakuta taarifa zako wanazo wanakwambia kalipe NMB kwanza halafu ndo uje kukopa kwetu,Mungu amsaidie huyu kijana aweze kumaliza shida hizi salama kwani alikua mfanokwa vijana wengine.
 
Back
Top Bottom