Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

By the way nitajibu hapo penye maandishi mekundu, kwa sababu pananihusu kiasi fulani.
Niko kwenye sekta ya nishati jadidifu kitambo sana, miaka 15 na kidogo. Huyu bwana ni mjasiriamali mzuri sana kwenye suala la umemejua (solar), ambako alitapa tenda kadhaa za UN, kufunga umemejua kambi za wakimbizi. Huko ndiko alikoanzia hizo fortune zake na kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors. Then baadae mwaka 2013 akaingia kwenye rekodi za jarida la Forbes kama milionea kijana, makala iko HAPA. Ndipo macho ya Watanzania wengi yakaanza kumuona na kumpa headlines kwenye magazeti na social media. Infact ni kati ya vijana wachache wenye mafanikio, ingawa kwa tunaoifahamu biashara ya solar (imeingiliwa sana na Wachina tangu 2000) kwa hapa Tanzania ilitupa mshituko kidogo kwamba inawezedkanaje kutengeneza mshiko mrefu kiasi kile (dola 8 milioni) ndani ya muda mfupi ule, kwa sababu soko la solar ni gumu kwa hapa kwetu.
Sasa nashangaa leo kawekwa kwenye orodha ya wadaiwa wa benki! Mtu mwenye 8 million dollar business anashindwaje kulipa mkopo wa benki?
Tuendelee kujadiliana.
Kwa mfanyabiashara bilionea kudaiwa na benki ni jambo la kawaida. Jambo ambalo sio la kawaida ni kushindwa kulipa. Sasa hapo inaonekana pana tatizo. Kwasababu benki imetangaza kwamba wamekaidi kulipa hata baada ya kufuatiliwa kwa muda mrefu.
Matajiri wengi, japo asilimia 40 ya mali zao zinakuwa ni madeni. Kwahiyo hiyo ni hali ya kawaida kabisa kwenye biashara. Kama hukopi, sahau kuendelea kibiashara.
 
Sawia kabisa. Kingine ninachojifunza ni kwamba, mtu anaweza kuthanimisha dhamana yake aliyokopea, akiona thamani ni ndogo kuliko mkopo then anachia iende. Akili kumkichwa.
mkuu wewe unatokea idimi kule kawetere??
 
By the way nitajibu hapo penye maandishi mekundu, kwa sababu pananihusu kiasi fulani.
Niko kwenye sekta ya nishati jadidifu kitambo sana, miaka 15 na kidogo. Huyu bwana ni mjasiriamali mzuri sana kwenye suala la umemejua (solar), ambako alitapa tenda kadhaa za UN, kufunga umemejua kambi za wakimbizi. Huko ndiko alikoanzia hizo fortune zake na kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors. Then baadae mwaka 2013 akaingia kwenye rekodi za jarida la Forbes kama milionea kijana, makala iko HAPA. Ndipo macho ya Watanzania wengi yakaanza kumuona na kumpa headlines kwenye magazeti na social media. Infact ni kati ya vijana wachache wenye mafanikio, ingawa kwa tunaoifahamu biashara ya solar (imeingiliwa sana na Wachina tangu 2000) kwa hapa Tanzania ilitupa mshituko kidogo kwamba inawezedkanaje kutengeneza mshiko mrefu kiasi kile (dola 8 milioni) ndani ya muda mfupi ule, kwa sababu soko la solar ni gumu kwa hapa kwetu.
Sasa nashangaa leo kawekwa kwenye orodha ya wadaiwa wa benki! Mtu mwenye 8 million dollar business anashindwaje kulipa mkopo wa benki?
Tuendelee kujadiliana.
What if the loan is more than the 8 million dollars? Usishangae kusihindwa kwake.
 
Jamaa si yuko CCM, amwambie baba Jeth amkopeshe alipe!
 
Ila mkae mkijua hata aliko dangote ana madeni mengi sana huko kwao nigeria aiseee....na pia inabidi mtofautihe kipato cha kampuni helvetic contractors na huyo patrick mwenyewe maana kwa sheria za makampuni owner na business hao ni watu wawili tofauti...kwaio kumpima kama mtu ana hela sana au hana unaangalia net worth yake kipato chake kwaio kampuni yaweza kua na hela nyingi kumshinda mmiliki....
 
Kama alipata hela kwa kufunga mitambo kwenye kambi ya wakimbizi ujue hiyo hela imeshuka sana kwani asipopata tender nyingine ndiyo kwishneyi. Mi nilifikiri anatengeneza vifaa vya solar
Kwenye makambi ya wakimbizi siku hizi Unhcr wanatumia generator na kwa maofisi yao na pia kambi za bongo hazina umeme kabisa usiku kunakua giza totoro hio ni nyarugusu camp sijawahi kuona solar system zaidi ya solar za 60,000 wanazonunua wakimbizi kwa matumizi yao binafsi....
 
Kuna kitu watu wanakosea kuhusu mikopo. Naamini Ngowi is smart enough to handle his financials.
 
Hivi kila anaedaiwa anatolewa gazetini?
 
Anaweza kuwa ana deni dogo sana, lkn pr dept ya stanbic wakaamua kumchafua jina na business rep yake kwa makusudi sababu ya wivu. Si unajua tena wabongo walivyo.
 
Kwanza kwa nini corporations kama stanbic waweke tangazo kwenye gazeti kwa style hii? Haileti picha nzuri na hii ni desturi na utaratibu usiofaa na ambao haundeani na basic civility rules ambazo zinalinda dignity ya kila mtu katika jamii. Nategemea kuwa makubaliano kati ya stanbic na mhusika yanalindwa na sheria za privacy na confidentiality and its not a matter of public interest. Stanbic wana uwezo wa kuwasiliana na wahusika kuh madeni bila ya ku publish humiliating ads in daily newspapers.
 
Amekuwa akialikwa kwenye makongamano mbalimbali ya vijana kama kijana aliyefanikiwa Sana. Yale mabilioni yote tunayoambiwa anayo yameyeyuka? Yaan mpaka bank wakuweke kwenye list ya defaulters ujue umeshindwa kulipa kwa Muda mrefu na efforts nyingi zimetumika lakini umeshindwa. Kuna jambo la kujifunza hapa, Nini kimepata huyu ndugu?
Ama ali-overstate networth yake au amefanya over expansion ya miradi yake akakomba working capital!!?!
 
nmewakumbuka 'malkia wa nguvu'. kumbe wengine wanasafirisha ngada
 
Hii ya kutangazana kwenye magazeti imekaa aje? Walipokopana hawakutangazwa, iweje kwenye kudaiana wanaanikwa hadharani. Mawasiliano ya barua na barua pepe na simu hayakutosha?
 
Back
Top Bottom