Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

Patrick Ngowi mmoja wa wanaodaiwa na Stanbic Bank

dhamana ya mkopo daima thamani yake inakuwa ni kubwa kupita kiwango cha mkopo unaopewa....
inatokea nyakati kama za mdororo wa uchumi thamani ya dhamana hushuka sana. hapo wajanja huamua kudefault.
 
inatokea nyakati kama za mdororo wa uchumi thamani ya dhamana hushuka sana. hapo wajanja huamua kudefault.
ni lini thamani ya nyumba au ardhi imewahi kushuka? Kumbuka benki nyingi dhamana yao ni mali isiyohamishika mfano nyumba au ardhi hazishuki thamani labda uzungumzie vicoba au saccos wanaweka dhamana ya sofa na masufuria
 
  • Thanks
Reactions: MC7
ukitolewa kwenye gazeti jua huyo ni mdaiwa sugu na bank wamejaribu kila njia imeshindikana na ni deni la muda mrefu sana..huyo ngowi ameshindwa kulipa...
Kuna nyakati benki wanakosea. Barclays ni wazoefu kunyanyasika na mikopo
 
By the way nitajibu hapo penye maandishi mekundu, kwa sababu pananihusu kiasi fulani.
Niko kwenye sekta ya nishati jadidifu kitambo sana, miaka 15 na kidogo. Huyu bwana ni mjasiriamali mzuri sana kwenye suala la umemejua (solar), ambako alitapa tenda kadhaa za UN, kufunga umemejua kambi za wakimbizi. Huko ndiko alikoanzia hizo fortune zake na kampuni yake ya Helvetic Solar Contractors. Then baadae mwaka 2013 akaingia kwenye rekodi za jarida la Forbes kama milionea kijana, makala iko HAPA. Ndipo macho ya Watanzania wengi yakaanza kumuona na kumpa headlines kwenye magazeti na social media. Infact ni kati ya vijana wachache wenye mafanikio, ingawa kwa tunaoifahamu biashara ya solar (imeingiliwa sana na Wachina tangu 2000) kwa hapa Tanzania ilitupa mshituko kidogo kwamba inawezedkanaje kutengeneza mshiko mrefu kiasi kile (dola 8 milioni) ndani ya muda mfupi ule, kwa sababu soko la solar ni gumu kwa hapa kwetu.
Sasa nashangaa leo kawekwa kwenye orodha ya wadaiwa wa benki! Mtu mwenye 8 million dollar business anashindwaje kulipa mkopo wa benki?
Tuendelee kujadiliana.
Duuuh, hatari sana kama ni kweli jamaa anadaiwa kias cha kushndwa kulipa, inamaana kifuatato ITV ni kufilisiwa. Wachna wameharibu biashara za weng sana!
 
ni lini thamani ya nyumba au ardhi imewahi kushuka? Kumbuka benki nyingi dhamana yao ni mali isiyohamishika mfano nyumba au ardhi hazishuki thamani labda uzungumzie vicoba au saccos wanaweka dhamana ya sofa na masufuria
Mdororo wa kidunia 2008 nyumba zilishuka thamani sana huko USA na mabenki yaliingia hasara hadi kuomba huruma (bail out?) ya Obama
 
ni lini thamani ya nyumba au ardhi imewahi kushuka? Kumbuka benki nyingi dhamana yao ni mali isiyohamishika mfano nyumba au ardhi hazishuki thamani labda uzungumzie vicoba au saccos wanaweka dhamana ya sofa na masufuria
inawezekana alikopa kutokana na biashara yake na kutokana na ushindani na wateja kukosa pesa imeshuka thamani. biashara hailingani na deni hivyo ni bora kuiwind up kwa mtindo wa kudefault.
 
pengine amefanya strategic default. unaacha kulipa baada ya kuona dhamana hailingani na pesa unayodaiwa.

Watu wanapiga porojo tu, ila ukiwa financial analyst unaweza nusa kitu hapa! Nahisi insurance NA bank kuna MTU atahumia tu hapa si ngowi
 
Mmojawapo pia ni huyo Bwn. Sanctus. Km ndo yuleyule wa kuhamasisha vijana na ndio mawazo yake, basi tuna safari ndefu sana kuwa na fikra na matendo ya kikwasi.

Mkuu nadhani nimeeleweka vibaya! Lengo langu sio kushangilia hilo lililotokea! Ukinisoma vizuri kwenye reaction zangu zote utaona kuwa ninashangaa ni nini kimetokea kwa mazingira ya kawaida.
 
Amekuwa akialikwa kwenye makongamano mbalimbali ya vijana kama kijana aliyefanikiwa Sana. Yale mabilioni yote tunayoambiwa anayo yameyeyuka? Yaan mpaka bank wakuweke kwenye list ya defaulters ujue umeshindwa kulipa kwa Muda mrefu na efforts nyingi zimetumika lakini umeshindwa. Kuna jambo la kujifunza hapa, Nini kimepata huyu ndugu?
Ukitaka kuwa Tajiri usiogope kudaiwa, kwa mantiki hiyo Kudaiwa sio dhambi!
 
Mkopo n jambo la kawaida.ata USA inadaiwa.
Anao uweZo wa kulpa na co Solar pekee bali ana Real estate compny na mambo mengne.
Then ths guy is vry flexble when comes to bznec.
Kutokulpa deni haimaanish kuwa c tajir.myb kuna mgongano kat yake na wakopeshaj n.k.
Kukopa ni kulinda mtaj na kutafuta faida kuptia mkopo!
 
Mkuu nadhani nimeeleweka vibaya! Lengo langu sio kushangilia hilo lililotokea! Ukinisoma vizuri kwenye reaction zangu zote utaona kuwa ninashangaa ni nini kimetokea kwa mazingira ya kawaida.
Nimekuelewa tofauti kabisa. Between the lines umefurahia. Post yako ya kwanza ndo nimeona hivyo
 
Nimekuelewa tofauti kabisa. Between the lines umefurahia. Post yako ya kwanza ndo nimeona hivyo

Mimi ni mjasirimali kama jamaa.Ninakopa kama yeye na masuala ya kudaiwa mabenki nayafahamu.Labda unachokiona kwangu kama ni furaha dhidi ya madhila yanayomkumba ni mshangao wangu kwa hatua aliyokwishafikia na kinachoendelea.Point ni moja tu mpaka jamaa kukubali publicized hivyo basi sio pesa kidogo anadaiwa.Sasa suspicion yangu ikawa kwamba kama ni kweli imekuwaje wakati ni juzi tu hata vyombo vya habari vimetoka tu mwaka huu ku-brand jamaa kama mtu anayefanya vizuri.Nichekelee ili iweje mkuu.Matatizo kwa mwanadamu hayaangalii sura,jinsia,taaluma na wala kiwango cha mafanikio.
 
Mkopo n jambo la kawaida.ata USA inadaiwa.
Anao uweZo wa kulpa na co Solar pekee bali ana Real estate compny na mambo mengne.
Then ths guy is vry flexble when comes to bznec.
Kutokulpa deni haimaanish kuwa c tajir.myb kuna mgongano kat yake na wakopeshaj n.k.
Kukopa ni kulinda mtaj na kutafuta faida kuptia mkopo!
Huenda ukawa na HOJA ila jifunze kuandika vzr huo uandishi wa Facebook ungeuacha huko
 
dhamana ya mkopo daima thamani yake inakuwa ni kubwa kupita kiwango cha mkopo unaopewa....
usichokijua USA ukiwa na nyumba unaweza kukopa deni lenye thamani Mara 25 zaidi ya thamani Halisi ya nyumba
 
Ngowi Patrick Kafulia....Bilionea wa kwenye magazeti ni kama Diamond naye ana zaidi ya bilioni kwenye account ya Take one TV.
 
Sawia kabisa. Kingine ninachojifunza ni kwamba, mtu anaweza kuthanimisha dhamana yake aliyokopea, akiona thamani ni ndogo kuliko mkopo then anachia iende. Akili kumkichwa.
hivyo ndiyo ilivyo
 
Jamaa niliwahi msikiliza hafanyi starehe yoyote,pia Hana mke.
Sasa pesa labda mpango wake wa kuwekeza kwenye gas ndio umemkata maana nayo ni moja ya kitu nilichomsikia akidhungumzia.
Chanzo mkasi
 
Back
Top Bottom