Patrice Lumumba

Explainer

JF-Expert Member
Dec 16, 2015
516
504
patrice-lumumba-55-years-later-480x269.jpg
"Licha ya kubeba historia ya chama kikongwe nchini, mtaa wa Lumumba umebeba jina la aliekuwa mmoja wapo wa viongozi bora kabisa wa Afrika ya wakati huo. Si mwingine bali ni Patrice Lumumba"
Huu ukiwa ni utangulizi wa masimulizi ya kumbukumbu za mauaji ya Patrice Lumumba na waasisi wa kiafrika dhidi ya The central intelligence agency (CIA) na washirika wake wakati wa vita baridi.

Kutokana na kujihami na kuitaji kupambana na umoja wa kisoviet maajenti wa CIA walitawanyika kila Kona ili kudhibiti tawala zinazoinukia kupitia Soviet Union ya wakati huo kabla haijasambalatika.
Hivyo kuifanya CIA kuwa na historia ndefu juu ya mauaji na kusaidia mapinduzi kwa viongozi ndani ya bara la Afrika, na hata kujaribu kushawishi makundi mengi ya waasi ili tu kuharibu na kuvunja umoja wowote uliokuwa upo au unachipukia.
Kuna matukio mengi yaliofanywa na CIA dhidi ya tawala mbalimbali lakini leo tutayaangazia machache tu ikiwemo mauaji ya Patrice Lumumba,
Huyu jamaa nimekuwa nikimkubali sana kwa machache aliyokuwa akiyafanya kwaajiri ya Kongo na Afrika.
Patrice anakumbukwa kwa misimamo yake na uimara katika kusimamia ukweli na haki.
Kwa ufupi Patrice Lumumba alizaliwa July 2, 1925 nchini Kongo wakati huo ikiitwa Belgian Congo, baba yake akiitwa François Tolenga na mama yake akiwa Julienne Wamato Lomendja wakiwa wakulima katika kitongoji cha Onalua, mkoa wa Kasai.
Patrice Lumumba nje ya historia yake ndefu ya elimu yake, maisha yake na familia yake, pia alikuwa na uwezo wa kuzungumza lugha tano ikiwemo Kiswahili, Tutela, Kifalansa, kilingala,na Tshiluba.
Patrice Lumumba ni mmoja wapo wa watu ninao wafananisha sana kimatendo na mkongwe Fredrick Douglas. Fred akiwa mtumwa na mmoja wa viongozi maarufu sana katika historia za Marekani, huyu alikuwa mtu mweusi, mwenye asili ya Afrika. Kabla hatujamzungumzia Patrice Lumumba, ngoja tujikumbushe kidogo kuhusu Fredrick Douglas
frederick_douglass_portraitjpg.jpg
katika kitabu chenye nukuu fupi fupi ya vitabu vya historia za Marekani kiitwacho
"Awake to world's unfolding" kitabu kilichobeba kumbukumbu mbalimbali kuhusu Marekani na misingi yake, vitabu maarufu kama vile "The diary of Anne Frank, Marco Polo, the incredible traveler nadhani Marco Polo kazungumziwa sana hapa JF, 20000 Leagues under the sea, liberty or death, The Gettysburg address ambayo ni mojawapo ya hotuba nzuri iliyotolewa na Abraham Lincoln mnamo November 19, 1863 huko Gettysburg, Pennsylvania na vitabu vingine vingi.
Tukirudi kwa bwana Fredrick kabla ya kuendelea na simulizi yetu kuhusu Patrice Lumumba,
Fredrick alizaliwa mwaka 1818 huko Marekani, na ni mmoja wapo wa watu weusi mashuhuri katika ukombozi wa Dunia akiongozana na kina Martin Luther King, Malcolm X, Desmond Tutu, Nelson Mandela, Koffi Annan, Mohamed Ali na watu wengine wengi weusi walioleta mabadiliko katika Dunia ya kkibaguzi,
Fredrick anakumbukwa kwa nukuu zake nyingi, mfano ni ule walaka wake usemao

"Nilikuwa Fredrick Douglas.
Nilileta ulimwengu mpya na nguvu za kujieleza.
Nilikuwa Fredrick Douglas
Mhariri wa North Star Keen, maneno mazuri ambayo hayawezi kuzikwa au kusahaulika, nilikuwa ni mwenye ujasiri wa maneno ya mapigano, maneno ambayo yalikuwa na kukua katika mioyo ya wanadamu mpaka ikawa msitu wa wanaume wanaoshambulia.
Nina kuhimiza kuruka silaha na kupigana na kifo, nguvu ambazo zingemzika serikali na uhuru wako katika kabuli hilo lililokuwa na tumaini.
Nilikuwa Fredrick Douglas kuna sanamu yangu katika mraba wa Rochester, nilikuwa mhalili wa nyota ya kaskazini, niliwapigania watu wangu kwa sauti kubwa ya neno.
( Maneno yametafsiliwa kwa kiswahili, tokea kiingereza)
New-York-Talking-Statues-Listen-to-the-Voices-of-Famous-NYC-Sculptures-Right-From-Your-Smartph...jpg
Sanamu ya Fredrick Douglas

Nimemfananisha Fredrick na Patrice Lumumba kutokana na kwamba wote walijitoa kwaajiri ya kupigana haki za watu weusi, ijapokuwa Patrice Lumumba aliuwawa kwa kuwekewa sumu katika mswaki huku Fredrick akifa mwenyewe tu kwa maradhi ya kawaida.
Lakini haikuwa sawa kwa Patrice Lumumba ambapo tunaona muda mfupi tu baada ya Kongo kujipatia uhuru mwaka 1960 na baada ya hapo kutokea mtikisiko na mpasuko ndani ya jeshi na hii ikionyesha mwanzo wa machafuko na mauaji ndani ya Kongo, ndipo Patrice akaamua kuomba msaada kwa umoja wa mataifa na mshirika wake mkubwa Marekani ili kudhibiti waliokuwa wafuatiliaji wa katangan waliokuwa wakipata msaada toka kwa wabelgiji katika kuleta machafuko.
Lakini United national na mshirika wake Marekani wakakataa kumsaidia Lumumba, hivyo kufanya Lumumba kugeukia kwa umoja wa Soviet kwaajiri ya kupata msaada na hapo ndipo palisababisha kuongezeka kwa tofauti na Rais wa Kongo ya wakati huo Joseph Kwasababu na viongozi wengine wakuu kama vile Joseph Dèsirè Mobutu pamoja na Marekani na Ubelgiji iliyokuwa ikiitawala Kongo.
Baada ya Lumumba kuonekana kuwa karibu na umoja wa Soviet ya wakati huo huku kukiwa na upinzani mkubwa kati ya Soviet na mataifa mengine ya ulaya na Marekani yenyewe chini ya kivuli cha vita baridi (cold war) Patrice Lumumba alikamatwa na kuwekwa Gerezani na mamlaka ya serikali chini ya Mobutu na kuuwawa, huku mipango yote ikisukwa na CIA na Ubelgiji ili kupambana na umoja wa Soviet.
Baada ya Lumumba kuuwawa mwili wake ulikatwa katwa na kuyeyushwa na acid huku mauaji hayo yakihusisha wa Belgium na Wamarekani.


Kwa kumalizia kidogo tujikumbushe nukuu moja wapo ya aliekuwa Waziri mkuu wa kwanza wa Kongo, Patrice Lumumba

"Siku itakuja ambapo historia itasema.....
Afrika itaandika historia yake mwenyewe.......
Itakuwa historia ya utukufu na heshima" (PATRICE LUMUMBA)
_89707828_gettyimages-158270628.jpg
 
"I know I have no reason that I'm going to die, but I die with my head higher above with destructible face than to live in humility and profound belief in the destiny of my country and renounce the principles which I consider secrete to me, because I know the history of the Congolese will be written by the Congolese" Patrice Lumumba
 
Niliona hii clip PL alipokamatwa huku analishwa speech yake while Mobutu chuckled!

Asee ile clip I wet in tears!

Nilivyoanza kufatilia hizo historia zao hasa Lumumba I wish angekuwepo kizazi changu daah!

Zamani kulikuwa na majembe hasa!
 
Ni nzuri mkuu. Kwa nyiongeza tu ni kuwa agizo la kumuua lilitoka cia ,walitaka hadi kumuua kwa mswaki wenye sumu . Balozi wa marekani congo anadai alipokea ujumbe kua "lumumba must be eliminated either physically or by any means"
 
Surphilic acid ni kifo cha mateso makali,why all this?
No waliwa m shoot akafa then wakamkakata kata vipande na kuviyeyusha kwenye acid.
Kwa kweli africans usaliti hatujaanza leo maana mobutu kwa tamaa ya power huku akiwa backed na cia plus belgium alikubali kumgeuka aliyekuwa mkuu wa nchi Lumumba.
Na wale wazee waliotekeleza niliona wakisema im not guilty because he insulted our king.Hapa ndipo najua kamwe wazungu si rafiki zangu hata punje wapo tu kwa ajili ya maslahi yao.
Ingekuwa n israel walai wange trace wale wauaji na kuwamaliza one after another.
Nadhan damu ya Lumumba inalilia haki thus why congo won't settle down forever.
 
am commited to surpass Lumumba,though i appreciate him. "To fight for peoples welfare you must risk your own welfare"
 
Back
Top Bottom