Possibly. Kwa uzoefu wangu red royale sprouting yake sio nzuri kama yale ya orange. Lakini hayo ya red ndio matamu zaidi. Mimi bado nasubiria mbegu 13 zifunguke na ni siku ya 15 leo. Pack ilisema 85% na kwetu kuna baridi so nazisubiria hadi nione hatima yake.
View attachment 184353 kilimo hiki kinalipa, ukipanda vizuri kwa kufata maelekezo, mbegu nzuri zinapatikana Kenya Agriculture Research Institute (KARI) huku kwetu ubabaishaji mwingi, karibuni shambani kwangu muone
Wadau nipeni ushauri nimefika kujionea shamba langu linakatisha tamaa, zaidi ya nusu ile ya mipapai ya kienyeji imekuwa madume. Kwa upande wa mipapai iliyotokana na mbegu kutoka Thailand bado haijaonesha but inaokena kama yote ni majike. Je kuna mbinu ya kuigeuza midume iwe majike?
Haya leo ndo nimefika toka 2013Zion Daughter njoo huku uchangie
View attachment 184353 kilimo hiki kinalipa, ukipanda vizuri kwa kufata maelekezo, mbegu nzuri zinapatikana Kenya Agriculture Research Institute (KARI) huku kwetu ubabaishaji mwingi, karibuni shambani kwangu muone
Hata mimi pia naomba mnisaidie ni jinsi gani naweza badilisha mipapai midume kua majike.
Ila nakumbuka zamani mama yangu alikua anachukua gunzi la muhindi halafu anafunga na kamba kwenye mti kama mpapai ni dume. Sikuelewa kwa nini anafanya hivyo.
Yale yale mambo ya 'ceritis peribus" etii upate milioni arobaini mwaka wa kwanza halafu usitumie hata cent wakati unakula nn upepo?ACHA KULALAMIKA MPWA WANGU...
HEBU CHUKUA KALUKUKETA YAKO KAMA NZIMA TUFANYE HESABU HII..!!
Eka moja ya shamba la papai inaweza kuingiza miche 1000-1200(elfu moja hadi elfu na mia mbili)-zile mbegu fupi. Tufanye umepanda miche 1,000. Mti mmoja ukiuhudumia vema unaweza kutoa matunda hadi 120 kwa msimu. Tufanye umetoa matunda 80, tu. Tunda moja kwa bei ya shamba tufanye umeuza bei ya "kutupwa" ya Tsh. 500/= (lakini papai lililoshiba linauzwa hadi Tsh. 3,000/= sokoni). Chukua 500/= mara 80 unapata 40,000/=(elfu arobaini kwa mti mmoja). Sasa chukua 40,000/= zidisha mara 1,000 unapata 40,000,000/=(milioni arobaini). Gharama za kulima papai ekari moja haizidi milioni mbili. Toka kupandwa hadi kuvunwa papai inachukua miezi kumi tu. Tufanye hivi: ukishavuna hii milioni 40 jibane, usiitumie, mwaka unaofuata nenda kapande tena papai ekari 20! Kama kalukuketa yako haisumbui utapata total ya Tsh. Milioni mia nane (800,000,000/=). Hapo nakuruhusu chukua milioni 100 zitumbue kwa raha zako(na mtu yeyote akikuhoji kwa nini unatumbua pesa nyingi namna hiyo? Mwambie Mjomba kaniruhusu!), Then, milioni 200 wekeza tena shambani, halafu milioni 500 weka benki. Naishia hapa kuhusu "kukalukuketi", malizia mwenyewe uone kama utakosa milioni 890 ndani ya miaka mitano. Tuache hayo. Najua utaniuliza, maswali kuhusu soko, hali ya hewa, udongo, mbegu na mengine. Tafadhali hayo maswali tafuta majibu mwenyewe, (nimekuachia home work-usilete uvivu wa kutafuniwa kila kitu). Lakini ukilima mapapai ukakosa soko hapa nchini, niletee nikupelekee Comoro na Madagascar. Kama umeungana na waliokariri kwamba hela ni ngumu zama hizi za mtumbua majipu, shauri yako, maana huo sasa ni uzembe laivu! Nimemaliza!....hizi nisalaam zangu kwako ni mimi mjomba wako nakusalimia