Pata nafasi ya kumwona Raisi wetu Kikwete akiwa na Raisi Clinton leo LIVE

engmtolera

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
5,150
1,437
[h=1]#CGI2011 Breakout: Global Nutrition w/ Nicholas Kristof & President Kikwete[/h]Event is LIVE NOW!
calendar-live_now.png
Kwa wale watakao kuwa karibu na mitandao ya internet basi mnaweza kupata nafasi ya kumshuhudia Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano Mh Jakaya Kikwete akiwa na Raisi Mstahafu wa marekani Clitoni katika mahojiano ya moja kwa moja yanayo husu.
#CGI2011 Breakout: Global Nutrition w/ Nicholas Kristof & President Kikwete

Itumie nafasi hii kuona wataalamu wakichambuwa mada mbalimbali zinazohusu maisha yetu sisi waafrika kwa ujumla

CGI Live - live streaming video powered by Livestream
 
Huo muda mchafu haupo.

Atuambie kwanza alivyotubia kura kwenye uchaguzi wa mwaka jana na uhalali wa rais wa kupitia mlango wa nyuma naye kuendelea kurandaranda hovyo kote duniani akitumbua kodi zetu.
 
Asante kwa taarifa mkuu, ingawa nipo safarini lakini nitajitahidi nikipata nafasi. Naona ni katika kutimiza ahadi zake alizotuahidi. Kweli tumshukuru Mungu kwa kutupa Rais anayependa maendeleo na kuchukia ufiasadi.
 
mie sitoangalia...naona aibu..! mfano;

swali; Sababu za umaskini wa nchi yako ni nini..?

Rais; eeeh eeeeeh ehnnn hmmmm... SIJUI KWA KWELI..!
(tabasamu)
 
Kwa wale watakao kuwa karibu na mitandao ya ineternet basi mnaweza kupata nafasi ya kumshuhudia Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano Mh Jakaya Kikwete akiwa na Raisi Mstahafu wa marekani Clitoni katika mahojiano ya moja kwa moja yanayo husu.
#CGI2011 Breakout: Global Nutrition w/ Nicholas Kristof & President Kikwete

Itumie nafasi hii kuona wataalamu wakichambuwa mada mbalimbali zinazohusu maisha yetu sisi waafrika kwa ujumla

CGI Live - live streaming video powered by Livestream

Mwambie mama salma, Riz1, Khalfani na wacheza kiduku wote wa Ikulu watizame. Ni Heshima tu kwa UN. Tungemfuata huko huko, ila mwambie tunamsubiria Washington DC. Amezidi kuvuja rasilmali zetu, mengine anauza kwa suti 5? Sijui atakuwa amevaa moja ya hizo suti?
tunamwandikia clinton kuhachana na huyo fisadi. Wakuu tunawapa contacts za clinton ili waachane na huyu fisadi kilaza
 
Thubutu!! Kwa huyu jamaa anayeweza kusaini document bila hata kuisoma, kwa mtu anayeshindwa kujua chanzo cha umasikini wetu, kwa jamaa anaweza kuuza mahakama kwa vipande vitano vya suti! Sitarajii jipya lolote. Nakushauri dont dare to waste ur time.
 
Saa ngapi mkuu? Au tukae tumekodoa mijicho kama ngumi ya jambazi bila kujua muda wa hiyo kombolela ya mhishimiwa akiwa huko ughaibuni? Umeshaongea na Ngeleja kuhusu uwepo wa megawati zake?
Kaaaaaz kwekweli..!
 
Mkuu hizi siasa haziwezi kusaidia lolote.. tazama Haiti ebu pitia kipindi hiki kisha utaelewa kwamba kila mtu anabeba mzigo wake...Bofya
 
Nimejaribu kutafuta kwenye GOOGLE kama kuna RAISI CLITONI - ​Hakuna

Sorry my Bro I will Pass your Offer...
 
Kwa wale watakao kuwa karibu na mitandao ya internet basi mnaweza kupata nafasi ya kumshuhudia Raisi wetu wa Jamhuri ya Muungano Mh Jakaya Kikwete akiwa na Raisi Mstahafu wa marekani Clitoni katika mahojiano ya moja kwa moja yanayo husu.
#CGI2011 Breakout: Global Nutrition w/ Nicholas Kristof & President Kikwete

Itumie nafasi hii kuona wataalamu wakichambuwa mada mbalimbali zinazohusu maisha yetu sisi waafrika kwa ujumla

CGI Live - live streaming video powered by Livestream

Tuone anavyochekacheka au?
 
Rwenyemamu hebu kaniangalizie hapo kwenye meza kushoto hapo Magogoni kam mihuri yote ipo.

Huyu bwana asije akawa ameondoka na muhuri wetu mfukoni kama yule Waziri wa zamani Karamagi kwenda kuwabembeleza watu huko Ughaibuni kuwasainia MIKATABA TATA kuwaongezea ardhi zidi ya Buzwagi dhahabu zote mpaka watoboe ardhi upande wa pili.
 
Tuache dharau Jamani,ebu tuangalie hiki kipindi ni endelevu na kinajaribu kutuonyesha wapi tumetoka ,wapi tunakwenda,ni muhimu sana kwa sasa Raisi wa zamani wa Nigeria Obasanjo ndio anahojiwa na wenzake
 
Na yeye ni mtaalamu wa nini? tuangalie kwa kupitia umeme gani? Jenereta? kwa mafuta gani? Naenda kutafuta pesa ya kununulia wanangu sukari kwa 2500 huku wakitishia kutumia jeshi! wanazo kweli hawa? Mmmh haya, ngoja niwashe kibatari changu niunganishe labda kitazalisha umeme nimuone Mheshimiwa "RAHISI" wangu akiongea kidhungu na wadhungu!
 
Tuache dharau Jamani,ebu tuangalie hiki kipindi ni endelevu na kinajaribu kutuonyesha wapi tumetoka ,wapi tunakwenda,ni muhimu sana kwa sasa Raisi wa zamani wa Nigeria Obasanjo ndio anahojiwa na wenzake

Mpenzi siyo dharau, hivi kuna umeme?
 
Back
Top Bottom