Passwords Zinantesa!

Kongosho

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
35,999
24,163
Hii teknolojia ya digital inanitesa. Nimejikuta nina passwords nyingi ambazo nashindwa kuzikumbuka kichwani zote.
Nikiangalia kwenye miongozo ya IT wanataja baadhi ya sifa za password nzuri ni
1. Iwe na mchanganyiko wa herufi na namba, ili kuwa ngumu kwa hackers ku-guess
2.Usiiandike popote, itunze kichwani
3. and so on

Kwa haraka haraka nikiangalia passwords tunazomiliki
1. Bank, na ukute una account zaidi ya benk moja, hapa epuka kutumia aniversaries za mkeo, mmeo, watoto, miaka ya kuzaliwa, mwaka wa kufunga ndoa, eashy for clever hackers to guess kama anakufahamu vizuri
2. Kazini una passwords kwa ajili ya ku-login kwenye systems, tena hulazimika kubadilika badilika baada ya kipindi fulani
3. Una personal email accounts, official, kuna zile mamluki kwa ajili ya vitu mamluki tena hizi ni nyingi kweli nazo una passwords
mfano una gmail 2, yahoo 2
4. Facebook, una account ya ukweli na mamluki
5. Mitandao ya kijamii labda ni member wa mitandao zaidi ya miwili, plus multiple ID's!!
6. Mitandao ya kufatuta ajira let say ni member wa mitandao mimwili tu
7. Professional groups eg Linkedin na mingine ming nako una password

Utunzaji wa hizi password unantatiza, wenzangu mnalionaje.
Naboreka sometimes.

Sijui nifungue kampuni la kutunza password za waungwana?
 
ngoja nikupe passwords zangu unitunzie. Nikizisahau unikumbushe....
1.Hi5.mbung2015e,
2.Face1000.hatuogopis3g3rea,
3. Yahoo.kufanikula1a,
4.Gmail.m1esiogop1
5.Hotmail.uswahilin1.
Nalog off
 
Bora, nacopy zako kama zilivyo

ngoja nikupe passwords zangu unitunzie. Nikizisahau unikumbushe.... 1.Hi5.mbung2015e, 2.Face1000.hatuogopis3g3rea, 3. Yahoo.kufanikula1a, 4.Gmail.m1esiogop1 5.Hotmail.uswahilin1. Nalog off
 
Amka, umejinu ukiwa unaota.
Hujajenga, bado umepanga. Sema nyumba yako ina automatic doors te te mapazia ya gunia.

mi nyumba yangu kila mlango na password yake, madirisha hali kadhalika, lakini still, nazikumbuka zote na sijaandika popote
 
Dah,hata mie haya mambo ya password yananichosha,
Nina mbili tu na nazitumia kila mahali panapohitajika password.
 
mi nyumba yangu kila mlango na password yake, madirisha hali kadhalika, lakini still, nazikumbuka zote na sijaandika popote

Buji, angalia siku ukifa hata maiti yako itawekwa nje ya nyumba yako mwenyewe! otherwise labda waungwana wafanye uharibifu kuvunja milango ili kukusitiri. Au hiyo nayo haujali?
 
Back
Top Bottom