Passwords Zinantesa!

Passwords Zinantesa!

Hauko peke yako Kongosho. Mie kazini natakiwa kubadilisha kila baada ya wiki sita yaani nakaribia kumaliza majina ya ndugu na marafiki. Nikiishiwa basi nitazuka hapa nianze kutumia ID za hapa 🙂🙂🙂 halafu inabidi uweke vitu kama hivi ~@!#^*&$ pamoja na namba ili ikubalike kwenye system.
tumia password hii: j^m!1f@rum$. Nalog off
 
ili password iwe na nguvu malizia na 100. eg kongosho100fb,kongosho100jf,kongosho100yahoo, kongosho100gmail,kongosho100myspace etc. Mia
 
cha muhimu ni kuwa na password moja ambaya itakuwa easy kuikumbuka. achan na milolongo mingi ambayo itakuchanganya na kukuumiza akili.
 
cha muhimu ni kuwa na password moja ambaya itakuwa easy kuikumbuka. achan na milolongo mingi ambayo itakuchanganya na kukuumiza akili.

Ni kweli anachosema nizzo kuwa na password moja itakupunguzia mzigo wa kumbukumbu.unakuwa na password yako moja ngumu nzuri.try and you will tell us.
 
Kuna watu wana password za matusi. Nilishdwa kuvumilia nikaachana na tabia na ku hack account za watu.
 
passwords zangu zilizokaa kichwani nyingi ni jina na tarehe za kuzaliwa X girlfriend wangu!napenda kuzibadilisha ila ndo zishakaa kichwani basi inakuwa ngumu kumsahau...nimeamua kuzichunia tu kibishi!nikienda bank namkumbuka,nikizama mitandaoni namkumbuka basi balaa!
 
Duh! Mi passwords zangu za mitandao huwa zinafanana.
Kongosho ulisomaga history?
 
Hauko peke yako Kongosho. Mie kazini natakiwa kubadilisha kila baada ya wiki sita yaani nakaribia kumaliza majina ya ndugu na marafiki. Nikiishiwa basi nitazuka hapa nianze kutumia ID za hapa 🙂🙂🙂 halafu inabidi uweke vitu kama hivi ~@!#^*&$ pamoja na namba ili ikubalike kwenye system.

tumia husninyo. Lol.
 
Unaweza tumia pasword moja katika shughuli zako zote zinazo hitaji kutumia pasword, ila unahakikisha pasword yako inakua strong na unaibadili mara kwa mara.
 
Ngoja nikuazime zangu ili uzitumie kwa muda,ni rahisi kuzihifadhi na ni vigumu kwa hackers kuzishtukia.
Nalog off
 
..na bado kwenye simu zako umeweka security code/password
..unaweza kuzichanganya!
Hii teknolojia ya digital inanitesa. Nimejikuta nina passwords nyingi ambazo nashindwa kuzikumbuka kichwani zote.
Nikiangalia kwenye miongozo ya IT wanataja baadhi ya sifa za password nzuri ni
1. Iwe na mchanganyiko wa herufi na namba, ili kuwa ngumu kwa hackers ku-guess
2.Usiiandike popote, itunze kichwani
3. and so on

Kwa haraka haraka nikiangalia passwords tunazomiliki
1. Bank, na ukute una account zaidi ya benk moja, hapa epuka kutumia aniversaries za mkeo, mmeo, watoto, miaka ya kuzaliwa, mwaka wa kufunga ndoa, eashy for clever hackers to guess kama anakufahamu vizuri
2. Kazini una passwords kwa ajili ya ku-login kwenye systems, tena hulazimika kubadilika badilika baada ya kipindi fulani
3. Una personal email accounts, official, kuna zile mamluki kwa ajili ya vitu mamluki tena hizi ni nyingi kweli nazo una passwords
mfano una gmail 2, yahoo 2
4. Facebook, una account ya ukweli na mamluki
5. Mitandao ya kijamii labda ni member wa mitandao zaidi ya miwili, plus multiple ID's!!
6. Mitandao ya kufatuta ajira let say ni member wa mitandao mimwili tu
7. Professional groups eg Linkedin na mingine ming nako una password

Utunzaji wa hizi password unantatiza, wenzangu mnalionaje.
Naboreka sometimes.

Sijui nifungue kampuni la kutunza password za waungwana?
 
Back
Top Bottom