Paschal Mayalla: Matangazo ya kumnadi Magufuli Star TV yamelipiwa kiasi gani na CCM?

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
10,129
35,146
Mwandishi wa kujitegemea Paschal Mayalla amehoji ni kiasi gani CCM wametumia kulipia matangazo ya kumnadi kupitia Star Tv ambayo yanaoneka zaidi ya mara 100 katika masaa 24 (Wastani wa Tangazo 1 kwa kila baada ya Dakika 15).

Matangazo hayo ni mbali ya matangazo ya Live katika mikutano ya Magufuli katika mikoa mbalimbali.

Pasco amehoji hayo katika kipindi cha jicho letu ndani ya Habari, leo asubuhi Star Tv katika muktadha wa kuzungumzia sheria ya Uchaguzi ya matumizi na mipaka ya gharama za uchaguzi.
 
Star TV ni televisheni bora kwa mitambo yao ya kisasa ambayo wanaweza kufanya live mbili kwa wakati mmoja kuliko televisheni yoyote nchini kwa kusheheni vifaa vya kisasa na vingi, Pengine Azam Tv sasa anaweza kuwa wapili au wako sawa

Ndiyo maana watia nia wa CCM wengi waliitumia star TV hapo ilivuna mamilioni ya pesa maana live kwa saa moja tshs 5 milioni

Sasa hivi CCM wamekuwa wajanja sana wamelipa live 10 kwa Star Tv na kurusha matangazo ya CCM madogomadogo hapo Star Tv wamevuna zaidi ya milioni 300 .

Kampeni za CCM zimefanikiwa na kuboreka zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwa star tv ni televisheni inapatikana kwenye ving'amuzi vyote na live yao haikatiki kama televisheni nyingine isipokuwa Azam Tv.

Tusubiri matunda ya CCM kwa kampeni zao za kisayansi.
 
Kwani huyo Pascal Mayalla hajui kuwa Star TV ni yetu? Ni ya kada mwenzetu? Mbona hahoji UKAWA wanapopewa airtime ya kutosha ITV na Channel Ten? Anthony Diallo kaamua kuchangia chama kwa staili hiyo. Sema kinachomuuma Pascal ni ujumbe unaowasilishwa na si kujua gharama
 
Mkuu Ch10 tena?

Ka ch10 wangekua ni team Lowasa, sidhani ka kila siku wangekua mkubalia Polepole kuja kumchafua lowasa.
 
hakuna malipo hapo kwa matangazo ya ccm sababu mmiliki ni kada wa ccm.angalia sasa wanavyomuonyesha sumaye akiongea akiwa ccm na sasa akiwa ukawa. ni propaganda tupu ambazo tcra wanatakiwa kulikemea kwa biased reporting.
 
Kibaya chajitembeza kizuri chajiuza ,kwa kujaa matangazo ya Mgufuli katika channel hio na sehemu zinginezo ni wazi kuwa anajitembeza.

Lowasa chini ya UKAWA hahitaji hata matangazo wala mikutano,basi tu anatimiza wajibu kwani tayari wananchi wameisha mchagua tokea akiwa CCM ambako choyo cha wachache ndio kiliosababisha kumuengua ,sasa Lowasa na wengine wameenda kuyatafuta maendeleo na kuwaletea maendeleo waTz nje ya CCM na ndio hivyo ,Magufuli na wenzake kila wanapouliza nani Raisi wanajibiwa na wanaohudhuria mikutano yao yote tena kwa sauti kuu LOWASA ,kulikowapelekea kuwacha kuuliza suali hilo kwenye mikutano mingine,
 
Kwa mfano umekaa kimya kuliko kujidhalilisha hivi ingekuwaje?
 
Hebu tufanye mahesabu.

Kwa makadirio kuna watu milioni moja (mtu mmoja kwa kila watu 45 nchini) wanaotazama TV, japo mara moja kwa siku. Tangu kuletwa ving'amuzi, kuna zaidi ya TV stations 50 (ukijumlisha vingamuzi vyote) zinazoonekana Tz.

Milioni 1 gawanya kwa 50, kila TV channel inatazamwa na wastani wa watu 20,000 kwa siku. Kati ya hawa 20, chance kwamba ni waelewa, wamejiandikisha na watapiga kura ni 50%. Kwa hiyo ni watu 10,000 hayo matangazo ni relevant kwao. Kati ya hao watu 10,000 waelewa, chance kuwa mtu atabadilishwa mawazo yake juu ya nani ampigie kura ni 20% yaani watu 2,000. Kwa maana kwamba 80% tayari walishaamua wapige wapi, CCM au kwingine.

Watu wanaotazama TV kila siku almost ni wale wale. Kwa hiyo kwa miezi miwili channel moja ya TV inaweza kuwa imneshawishi watu wasiozidi 10,000 nchi nzima, au kote inakotazamwa.
 
Pascal nawe tuambie umelamba ngapi kwa Lowassa maana toka anagombea akiwa Ccm unaye. Tunafahamu kuwa na wewe ni mmoja wa Nyumbu wanaelekea anapoelekea mmoja. Hapa ni kazi tu. Nyumbu na viroba na vichaa wa Bavicha kwa Lowassa. Great thinkers kwa Magufuli tu. Pascal unakula matapishi yako. Jinukuu uliyoyasema kuhusu Ukawa huko nyuma. Kura zoooooote kwa Dr Magufuli
 
Mwandishi wa kujitegemea Paschal Mayalla amehoji ni kiasi gani CCM wametumia kulipia matangazo ya kumnadi kupitia Star Tv ambayo yanaoneka zaidi ya mara 100 katika masaa 24 (Wastani wa Tangazo 1 kwa kila baada ya Dakika 15).

Matangazo hayo ni mbali ya matangazo ya Live katika mikutano ya Magufuli katika mikoa mbalimbali.

Pasco amehoji hayo katika kipindi cha jicho letu ndani ya Habari, leo asubuhi Star Tv katika muktadha wa kuzungumzia sheria ya Uchaguzi ya matumizi na mipaka ya gharama za uchaguzi.
Inasikitisha kwa mwandishi wa habari 'nguli' kama huyu kuhoji kuuliza swali la kipumbavu kama hili, nje ya topic kabisaaaaaa!!
Sasa waandishi wenyewe ndo hawa?? kazi tunayo.
 
Kibaya chajitembeza kizuri chajiuza ,kwa kujaa matangazo ya Mgufuli katika channel hio na sehemu zinginezo ni wazi kuwa anajitembeza.

Lowasa chini ya UKAWA hahitaji hata matangazo wala mikutano,basi tu anatimiza wajibu kwani tayari wananchi wameisha mchagua tokea akiwa CCM ambako choyo cha wachache ndio kiliosababisha kumuengua ,sasa Lowasa na wengine wameenda kuyatafuta maendeleo na kuwaletea maendeleo waTz nje ya CCM na ndio hivyo ,Magufuli na wenzake kila wanapouliza nani Raisi wanajibiwa na wanaohudhuria mikutano yao yote tena kwa sauti kuu LOWASA ,kulikowapelekea kuwacha kuuliza suali hilo kwenye mikutano mingine,
Mnatapatapa.
 
Back
Top Bottom