Paschal Mayala atoa Ushauri wa bure kwa wana JF

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,615
Akiwa kwenye kipindi chake cha PPRA alikuwa akimhoji bwana Utoh wa ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za serikali.
Utoh kama nilivyotegemea kuwa anatetea mkate usiingie matope akaanza mapambio ya sifa za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akataja idadi ya vyuo vikuu na kilometa za lami zilizoongezeka.
Mayala akatoa wito kwa wanasiasa na wanahababi kuwa wasipinge kila kitu. Baadae kwa msisitizo na kwa umakini akasema, 'nawashauri nduguzangu na member wenzangu wa JF, tuwe wakweli mioyoni mwetu. Serikali imefanya mengi sio tupinge kila kitu. Tukubali tu kuwa tuna maendeleo'
 
tatizo sio kwamba hakuna maendeleo tatizo ni kuwa kuna watu wamesimamisha maendeleo wanajiendeleza wao na familia zao badala ya taifa kwa ujumla
 
Hao wanaoimba maendeleo watueleze na changamoto/matatizo makubwa kwa wananchi wa vijijini. siyo kila siku mazuri wakati magumu/mabaya ni mengi zaidi.
Tuwe tunalinganisha na rasilimali tulizo nazo.
 
Asante mtoa mada, asante Mayala, ni kweli member wenzangu humu wengi wao ni kupinga tu, matusi tu, bila ya kupima na kujenga hoja ya hali halisi
 
hakuna anaesema hakuna maendeleo

ni kama unasafiri kwenda mwanza unatoka daresalaam
wenzio wanatumia siku tatu wanafika mwanza
wewe baada ya wiki uko morogoro bado....sasa watu hawasemi hauendi mbele
wanazungumza kuwa ulipaswa kuwa uko mbali au kuwa umefika zaidi ya hapo
 
maendeleo yanayopimwa kwa barabara na majengo hovyo ya madarasa ya shule za kata.
Nchi yeyote duniani aliyoendelea lazima uchumi wake kwa kiasi kikubwa itokane na ability to manufacture/fabricate, sasa sisi tumeua viwanda vyote, hata kile cha kutengeneza baiskeli aina ya swala walizozipenda sana wasukuma. Tukakiua taratibu huku tukiingiza baiskeli kutoka china zikiitwa phoenex.

Miaka 50 ilopita tulikuwa tunalima kwa jembe la mkono, leo tunalima kwa jembe hilo hilo.....miaka ya kati hapa kulikuwa na matrekta ya vijiji....yamekufa kama nyerere.
Miaka 50 ya uhuni, bajaji ndio ambulance!!
 
hivi ni maendeleo gani tulnayo ambayo yanaendana na miaka 50? Mwambie hv huyo mayala na hao wachumia tumbo wenzake aache UNAFIKI?
 
Kwani kuna mtu anabisha kuna maendeleo suala ni kwamba kwa rasilimali tulizonazo ilitakiwa tuwe kama Libya au SA, ila sasa nchi zilizotoka vitani juzi tu zinatupita (Rwanda) tukiuliza wanajibu kwamba majimbo yao ni makubwa kuzidi Rwanda.

Halafu pia majibu ya vingozi wetu ndio yanachefua na kutia hasira...........Gharama za maisha zimepanda sana Dodoma kuliko sehemu nyingine.
 
Back
Top Bottom