Saint Ivuga
JF-Expert Member
- Aug 21, 2008
- 55,024
- 59,686
huyu naye vipi ..tumuwekee picha kabisa?
Akiwa kwenye kipindi chake cha PPRA alikuwa akimhoji bwana Utoh wa ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za serikali.
Utoh kama nilivyotegemea kuwa anatetea mkate usiingie matope akaanza mapambio ya sifa za miaka 50 ya Uhuru wa Tanganyika.
Akataja idadi ya vyuo vikuu na kilometa za lami zilizoongezeka.
Mayala akatoa wito kwa wanasiasa na wanahababi kuwa wasipinge kila kitu. Baadae kwa msisitizo na kwa umakini akasema, 'nawashauri nduguzangu na member wenzangu wa JF, tuwe wakweli mioyoni mwetu. Serikali imefanya mengi sio tupinge kila kitu. Tukubali tu kuwa tuna maendeleo'
mada haina maana hii pia humu jf vilaza wengi sana
Asante mtoa mada, asante Mayala, ni kweli member wenzangu humu wengi wao ni kupinga tu, matusi tu, bila ya kupima na kujenga hoja ya hali halisi
Maendeleo kulinganisha na wp?miaka 50 nch ya tatu kwa umasikin..!
...... Baadae kwa msisitizo na kwa umakini akasema, 'nawashauri nduguzangu na member wenzangu wa JF, tuwe wakweli mioyoni mwetu. Serikali imefanya mengi sio tupinge kila kitu. Tukubali tu kuwa tuna maendeleo'
hivi ni maendeleo gani tulnayo ambayo yanaendana na miaka 50? Mwambie hv huyo mayala na hao wachumia tumbo wenzake aache UNAFIKI?
Kuweka bandiko kama la Jwagu inahitaji uwe na roho ngumu.... Hivi we Jwagu, umeshawahi kujiuliza kwa nini raisi Kagame alimwambia JK NIPENI BANDARI TU NA NITAILISHA TZ NA RWANDA.... Watu tunalinganisha tulipo na tulipotakiwa kuwa...Asante mtoa mada, asante Mayala, ni kweli member wenzangu humu wengi wao ni kupinga tu, matusi tu, bila ya kupima na kujenga hoja ya hali halisi
mada haina maana hii pia humu jf vilaza wengi sana
hakuna anaesema hakuna maendeleo
ni kama unasafiri kwenda mwanza unatoka daresalaam
wenzio wanatumia siku tatu wanafika mwanza
wewe baada ya wiki uko morogoro bado....sasa watu hawasemi hauendi mbele
wanazungumza kuwa ulipaswa kuwa uko mbali au kuwa umefika zaidi ya hapo