Paschal Mayala atoa Ushauri wa bure kwa wana JF

Asante mtoa mada, asante Mayala, ni kweli member wenzangu humu wengi wao ni kupinga tu, matusi tu, bila ya kupima na kujenga hoja ya hali halisi
Kule kijijini kwenu utokako hali ikoje na maeneo ya jirani? Hamkawii kusema mmezaliwa kariakoo ambapko keenyewe kuna matatizo lukuki
 
JF usipokandia Serikali na kusifia cdm na viongozi wake hueleweki.
Pole Mayala ngoja utaona majibu yake hapa.


Serikali ikijenga lami haisifiwi, ni wajibu wake! itasifiwa ikiwaajibisha wahujumu wa fedha zetu. Serikali inakusanya kodi kutoka kwetu ili iendeshe nchi, inawasomesha watui sio kuwa ni zawadi, inawasomesha wawe na uwezo wa kuajiliwa na walipe kodi, sio vingeyoooo
 
maendeleo yanayopimwa kwa barabara na majengo hovyo ya madarasa ya shule za kata.
Nchi yeyote duniani aliyoendelea lazima uchumi wake kwa kiasi kikubwa itokane na ability to manufacture/fabricate, sasa sisi tumeua viwanda vyote, hata kile cha kutengeneza baiskeli aina ya swala walizozipenda sana wasukuma. Tukakiua taratibu huku tukiingiza baiskeli kutoka china zikiitwa phoenex.

Miaka 50 ilopita tulikuwa tunalima kwa jembe la mkono, leo tunalima kwa jembe hilo hilo.....miaka ya kati hapa kulikuwa na matrekta ya vijiji....yamekufa kama nyerere.
Miaka 50 ya uhuni, bajaji ndio ambulance!!
Mkuu umeongea vema nadhani Maylalya atakuwa amekuelewa
 
Serikali ikijenga lami haisifiwi, ni wajibu wake! itasifiwa ikiwaajibisha wahujumu wa fedha zetu. Serikali inakusanya kodi kutoka kwetu ili iendeshe nchi, inawasomesha watui sio kuwa ni zawadi, inawasomesha wawe na uwezo wa kuajiliwa na walipe kodi, sio vingeyoooo

now umenena hicho ndicho wahanga wasiasa ndio wanakiongelea kama kivuli chao kikubwa..
 
Tusimlaumu Paschal Mayalla alikuwa akilinda kibarua hata hivyo huyo ni tofauti na huyu wa hapa kwetu jf huyu yeye huitwa Pasco wa jf.Hapa kuna uhuru wa maoni sio kule TB c
 
Pascal labda anafukuzia kuwa mwandishi wa Raisi maana kama ni Mtanzania halisi na unaguswa na yanayoendelea nchini sidhani kama sifa zitazidi lawama kwa existing regime
 
hakuna chochote killichofanyika.....CCM wakoloni tu

Namwalika paschal na nyie wengine,hata Utouh, wapitie thread ya Star TV .... Humo tumejadili maendeleo ya Tanzania kwa kina! Watu humo wamelilia viwanda vya nguo,kandambili,viatu,chupa,tairi za magari[General Tyre],n.k. Pitieni thread hiyo,tupate maana halisi ya Uhuru! Kuandikwa jina la Star TV isiwe hoja!
 
Maendeleo yako wapi bwana!!! Miaka 50 ya uhuru watu wanaishi kwenye nyumba za tembe- tope juu chini mtindo mmoja, kipato cha mtu kwa siku ni chini dola 1, maji na umeme vimekuwa vikwazo kwenye jamii,
kwa Tanzania ni familia chache mno zinazo nusa harufu ya maendeleo lkn kwa ujumla tusidanganyane.
 
Hatusemi kikweli maendeleo hayapo ila tungekuwa na tafsiri nzuri ambayo tunakubaliana kwamba 'maendeleo' ninini.
Hakuna ubishi kwamba ukimkuta mtoto ana miaka kumi na bado hali chakula chake mwenyewe ila bado ana nyonya sikubaliani na hili.
Mali tunazo tatizo letu ni kwamba viongozi wameacha vipaumbele vya taifa na kushughulika na familia zao badala ya nchi.
 
Mayala hana sababu ya kusubri ashike mike ndio aiseme JF si ni member hapa ainisha hapa unayoona wewe ndani ya miaka 50 tumefanikiwa halafu usubiri ufundishwe inawezekana kisomo chako hakijakusaidia sana kupambanua mambo,najua wewe pia ni miongoni mwa wanaotegemea bahasha pole sana,jaribu kuwa mkweli.
 
Tatizo ninalo liona ni kwamba wakati tunasema kuna maendeleo.....hatuongei kulinganisha na nini? Kulinganisha na nani> Kulinganisha na what resources in our exposure/reach, kulinganisha na nchi nyingine wasio kuwa na hizo resources.....hapa pia kulinganisha na unexploited resources and opportunities. Kulinganisha na nchi `za Kusini Mashariki (kama Korea) ambao wamekuwa from ashes into their current state! Si haki kusema tumeendelea wakati sisi wenyewe ndo judges, ndo implementers na ndio wanaoandika job description! Hebu tuangalie barabara, shule za kata (na sasa zahanati za kata) na hata uingizwaji wa wanafunzi wengi vyuo vikuu, kwa jinsi gani tunaweza kujivunia pasipo kuwa na pre-judgement. Mi ninahisi, kama tungekuwa wakweli na dhamira zetu, ingekuwa vema tungemtafuta mtu ambaye ni impartial atusaidie kutuambia wapi tunaweza kuweka jitihada - kwenye madini, kilimo, kuwekeza kwenye viwanda, upatikanaji wa nishati na mengine ili tujue within the next 50 years tutakuwa tumesonga mbele, otherwise nachelea kusema hizi ni POROJO TUUUUUUUUUUU!
tatizo sio kwamba hakuna maendeleo tatizo ni kuwa kuna watu wamesimamisha maendeleo wanajiendeleza wao na familia zao badala ya taifa kwa ujumla
 
Ewe jk endelea na safari za nje za kuombaomba maana ulisha wahi kusema bila wewe kwenda kuomba omba tutakufa njaa,tia bidii uzishinde iraq na afaghanstan uwe wa kwanza hayo ni maendeleo ya miaka 50 poor thinking capacity.
 
Back
Top Bottom