Ushauri wa Bure kwa Lowassa: Hata kama ni kweli uliibiwa kura; Kaa kimya, Mungu ndiye akupiganie!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,620
Wanabodi,

Uchaguzi Mkuu ulifanyika na kumalizika ile Octoba 25,2015 na matokeo 'halali' yametoka!, aliyeshinda ameshinda, aliyeshindwa ameshindwa kwa mtindo wa "The winner takes it all, and the looser standing small!".

Despite all the odds, the end justify the means, mshindi 'halali' ni John Pombe, Joseph Magufuli, kinachotakiwa sasa ni kumpa ushirikiano wa aina zote, kwa sisi Watanzani katika umoja wetu, iwe tulimchagua, hatukumchagua au hatukupiga kabisa kura, maadam katiba yetu inasema mshindi akiisha tangazwa na Tume ya Uchaguzi, NEC, ndiye mshindi, then uchaguzi ndio umeishia hapo!, aliyetangazwa ndiye mshindi 'halali' na ndie rais wetu, ni rais wa wote, ndiye rais wa CCM waliyemchagua, ndiye rais wa Watanzania wote waliopiga kura, ndiye rais wa Watanzinia wote ambao they never even bothererd kupiga kura, ndie rais wa Chadema na UKAWA wote waliomchagua Lowassa.

Infact, Magufuli ndiye sio tuu ni rais wa Lowassa, bali ni Magufuli ndie anayemlisha na kumvisha Lowassa kupitia pensheni, ni Magufuli ndiye anayeigharimia Chadema kupitia fedha za ruzuku!, Magufuli, akiamua kuiita ruzuku nayo ni ufisadi, anaweza kuandika presidential decree kuifutilia mbali ruzuku, japo CCM ndicho chama kitakacho suffer most, Chadema kitakufa kabisa, kwa sababu kuna nchi kibao tuu, hazina pesa za upuuzi kama huu wa kutoa ruzuku kwa vyama vya siasa, hivyo wana Chadema na wana UKAWA, mnatakiwa sio lazima kumpenda Magufuli, bali lazima kushirikiana naye kulijenga taifa letu changa!, kama ni kupenda, tuendelee kumpenda Lowassa wetu, tunywe nae chai, lakini katika ujenzi wa taifa, ushirikiano ni kwa Magufuli, kupitia "Hapa Kazi tuu!.

Nimetoa ushauri huu kwa Lowassa, baada ya kuendelea kusoma kuwa mpaka leo, Lowassa bado anaendelea kulalamika kuwa ni yeye ndiye alishinda kwenye urais lakini CCM wamempora ushindi wake kwa bao la mkono!.
Aliyekuwa mgombea Urais anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Edward Lowassa, ameendelea kudai ndiye mshindi kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita na dunia inajua.

Katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari kupitia msemaji wake, Aboubakary Liongo, Lowassa alisema ushindi wake uliporwa na kupewa mtu mwingine lakini amewataka Watanzania wasikate tamaa.

Lowassa pia aliwashukuru Watanzania kwa kumpa kura nyingi wakati wa uchaguzi huo, kura ambazo alidai kuwa zilimfanya kuongoza dhidi ya wagombea wengine.
Mkuu Chachu Ombara, Japo binafsi siamini kuwa Lowassa ameshinda ila ameibiwa kura, but yet one can never tell with CCM, anything is possible!, kule Zanzibar kila siku CUF inashinda lakini inayotangazwa mshindi ni CCM!.

Mimi binafsi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono Lowassa humu jukwaani na kuwashawishi watu wamuunge mkono, lakini katika matokeo, naamini kilichotokea ndicho Watanzania wengi zaidi walichotaka, hivyo ukiamua kufikiri kwa kutumia hisia na mapenzi kuwa ni kweli Lowassa alishinda lakini CCM wameiba ushindi wake, then utakuwa very right kujifurahisha nafsi yako, lakini ukifikiri kwa kutumia logic, lazima utakuwa na mashaka na madai haya ya Lowassa wetu kushinda!.

Uchaguzi umeendeshwa kwa mfumo wa uwazi wa hali ya juu kupitia mawakala wa vyama, na UKAWA iliweka mawakala wake kila kituo!. Matokeo ya kila kituo, yanajumlishwa na kubandikwa vituoni, huku kila wakala akipewa nakala halisi yenye sahihi yake kuyakubali matokeo hayo, hivyo kama ni kweli CCM ilichakachua, by now, UKAWA imepata muda wa kutosha kujumlisha matokeo yao ya nchi nzima kupitia zile nakala za mawakala wao, hivyo sasa wangekuja to an open na kutueleza kuwa matokeo halisi kwa mujibu wa tallying ya UKAWA ni haya vs matokeo ya NEC, hivyo kutupa fursa ya kuuona huo uchakachuaji wa CCM na NEC yake jinsi ulivyofanyika!. Hizi blanket statements za Lowassa alishinda ila kaibiwa, sasa zitoshe!, uchaguzi umekwisha, sasa ni kazi ya kulijenga taifa kupitia falsafa ya "hapa ni kazi tuu!".

Ila kama ni kweli kabisa, Lowassa ndie aliyeshinda kihalali lakini CCM ikaiba kura kwa kuchakachua, then tutashuhudia 'karma' ikiishughulikia CCM kikamilifu hii ikimaanisha hata miaka 5 tuu hadi 2020 mbele ya karma, itakuwa ni mbali!, nikimaanisha haitafika, kuna kitu Mungu, atawaambia CCM!. Ila pia kama Lowassa anajua hakushinda, bali anaendelea kujitangazia ushindi wa mezani ili tuu kumkwamisha mshindi halali Magufuli, ili wale wafuasi wake milioni 6 waliompa kura zao Lowassa, wasimpe ushirikiano Magufuli, then hiyo hiyo karma, haina mswalie Mtume, itamshughulia Lowassa, na hiyo 2020 itakuwa mbali!.

Jee ni nini kitamkuta Magufuli and Lowassa within the next five years kuelekea 2020 with reference to 'karma', Lets just sit, wait and see the oparatives of karma, sisi tubaki tuu kuwa mashahidi tuu na mashuhuda ya kitakachotokea, tutakumbushana humu.

Namalizia kwa kusisitiza huu ni Ushauri Wa Bure kwa Lowassa, Hata Kama Ni Kweli Uliibiwa Kura, Kaa Kimya, Usijipiganie Haki Yako Ya Ushindi Halali Kwa Kupiga Makelele, Bali Mwachie Mungu YEYE Ndiye Akupiganie!.

Unachotakiwa kufanya kwa sasa ni kujiuzulu siasa kwa heshima na kwenda kuchunga ng'ombe wako kama ulivyoahidi, kwa sababu 2020 itakuwa too little too late for you.

Nawatakia Jumapili Njema.

Paskali

NB. Mimi ni shauri wa bure wa kujitolea, hizi ni baadhi ya shauri mbalimbali za bure niliowahi kuisha kutoa

Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, Kubali Matokeo
Ushauri Wa Bure kwa ENL, Chadema na UKAWA, Tuyakubali Matokeo
Ushauri wa bure kwa CCM: Hope for the best but get prepared for ..
Pasco wa JF atoa Ushauri wa bure kwa wana JF - Page 3 - Jamii ...
Ushauri wa Bure kwa Zitto, Shika lako, ya wengine waachie wenyewe!
Ushauri wa Bure kwa ZZK!-Congratulations..But
Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. Shein - Jamii ...
Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako
Ushauri wa bure kwa Mhe. Lowassa: Ili kuilinda Heshima yako ..
Ushauri wa bure kwa Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi - Jamii ...
News Alert: Kuelekea 2015, USHAURI wa Bure kwa Mhe LOWASSA - Jamii ...
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Zitto on Escrow Report: Please Keep Quite ..
ENL, CHADEMA na UKAWA, Tuyakubali Matokeo!, Tushukuru Kwa Yote ..
Ushauri: Lowassa Asikanyage Arumeru!, Atamponza Sioi!
Ushauri wa Bure Kwa Mhe. Rais Magufuli, Futilia mbali utawala wa sheria ..
Wito Kwa Watanzania:Tuitumie Nguvu ya Kauli, Kumuingiza Ikulu .
[/quote]
 
Wanabodi, Uchaguzi Mkuu ulimfanyika na kumalizika ile Octoba 25, na matokeo yametoka, aliyeshinda ameshinda, aliyeshindwa ameshindwa kwa mtindo wa "The winner takes it all, and the loose standing small, despite all the odds, the end justfy the means, mshindi ni John Pombe, Joseph Magufuli, kinachotakiwa sasa ni kumpa ushirikiano wa aina zote, kwa sisi Watanzani katika umoja wetu, iwe tulimchagua, hatukumchagua au hatukupiga kura, akiisha Tangazwa ndiye mshindi, yeye ndie rais wetu, rais wa wote, ndiye rais wa CCM waliyemchagua, ndiye rais wa Watanzania wote waliopiga kura, ndiye rais wa Watanzinia wote ambao they never even bothererd kupiga kura, ndie rais wa Chadema na UKAWA wote waliomchagua Lowassa, infact, Magufuli ndiye sio tuu ni rais wa Lowassa, bali ni Magufuli ndie anayemlisha na kumvisha Lowassa kupitia pensheni, ni Magufuli ndiye anayeigharimia Chadema kupitia fedha za ruzuku!, rais Magufuli, akiamua kuiita ruzuku nayo ni ufisadi, anaweza kuandika presidential decree kuifutilia mbali ruzuku, japo CCM ndicho chama kitakacho suffer most, Chadema kitakufa kabisa, kwa sababu kuna nchi kibao tuu, hazina pesa za upuuzi kama ruzuku kwa vyama vya siasa, hivyo wana Chadema na wana UKAWA, mnatakiwa sio kumpenda Magufuli, bali kushirikiana naye kulitenga taifa letu!, kama ni kupenda, tuendelee kumpenda Lowassa, tunywe nae chai, lakini katika ujenzi wa taifa, ushirikiano ni kwa Magufuli, kupiti "Hapa Kazi tuu!.

Nimetoa ushauri huu kwa Lowassa, kupitie kuendelea kusoma kuwa mpaka leo, Lowassa bado anaendelea kulalamika kuwa ni yeye ndiye alishinda lakini CCM wamempora ushindi wake!. Japo binafsi siamini kuwa Lowassa ameshinda ila ameibiwa kura, but yet one can never tell with CCM, anything is possible!, kule Zanzibar kila siku CUF inashinda lakini inayotangazwa mshindi ni CCM!.

Mimi binafsi ni miongoni mwa watu tuliomuunga mkono Lowassa humu jukwaani na kuwashawishi watu wamuunge mkono, lakini katika matokeo, naamini kilichotokea ndicho Watanzania wengi zaidi walichotaka, hivyo ukiamua kufikii kwa kutumia hisia kuwa ni kweli Lowassa alishinda lakini CCM wameiba ushindi wake, then utakuwa very right, lakini ukifikiri kwa kutumia logic, lazima utakuwa na mashaka na madai haya ya Lowassa wetu kushinda!.

Uchaguzi umeendeshwa kwa mfumo wa uwazi wa hali ya juu kupitia mawakala wa vyama, na UKAWA iliweka mawakala wake kila kituo!. Matokeo ya kila kituo, yanajumlishwa na kubandikwa vituoni, huku kila wakala akipewa nakala yenye sahihi yake kuyakubali matokeo hayo, hivyo kama ni kweli CCM ilichakachua, by now, UKAWA imepata muda wa kutosha kujumlisha matokeo yao ya nchi kupitia zile nakala za mawakala wao, hivyo sasa wangekuja to an open na kutueleza kuwa matokeo halisi kwa mujibu wa UKAWA ni haya vs matokeo ya NEC, hivyo kutupa fursa ya kuuona huo uchakachuaji jinsi ulivyofanyika!. Hizi blanket statements za Lowassa alishinda ila kaibiwa, zitoshe!, uchaguzi umekwisha, sasa ni kazi tuu!.

Hivyo kama ni kweli Lowassa ndie aliyeshinda kihalali lakini CCM ikaiba kura, then tutashuhudia 'karma' ikiishughulikia CCM kikamilifu hii ikimaanisha hata miaka 5 tuu hadi 2020 itakuwa ni mbali!, nikimaanisha haitafika, kuna kitu Mungu, atawaambia CCM!. Ila pia kama Lowassa anajua hakushinda, bali anaendelea kujitangazia ushindi ili kumkwamisha mshindi halali, Magufuli, ili wale wafuasi wake milioni 6 waliompa kura zao. ili wasimpe ushirikiano Magufuli, then hiyo hiyo karma, haina msalie Mtume, itamshughulia na hiyo 2020 itakuwa mbali!.

Jee ni nini kitamkuta Magufuli and Lowassa within the next five years kuelekea 2020 with reference to 'karma', Lets just wait and see the oparatives of karma, sisi tubaki tuu kuwa mashahidi!.

Namalizia kwa kusisitiza huu ni Ushauri Wa Bure kwa Lowassa, Hata Kama Ni Kweli Uliibiwa Kura, Kaa Kimya, Usijipiganie Haki Yako Ya Ushindi Halali Kwa Kupiga Makelele, Bali Mwachie Mungu YEYE Ndiye Akupiganie!.

Nawatakia Jumapili Njema.

Pasco



Nilichokiona mimi huku kanda yetu ya ziwa ni dhahili Lowasa ameshindwa kwa haki na hajaibiwa kura yoyote,CDM ktk kipindi kijacho wajitahidi sana kuondoa uongozi wenye vinasaba vya ukanda mmoja,lakini pia kama wapinzani wawe wanaangalia na kauli za kuwaaminisha watanzania alafu baada ya muda wanageuka tena na kwa jambo lile lile na kulisafisha,hapo nazungumzia kauli walizozitoa za ufisadi wa EL na kisha kuja kumsafisha tena,kuna watanzania siyo waongeaji ila wanajua kupima mambo na wanaamua kupitia sanduku la kura.swala la ukanda liwepo au lisiwepo lakini limeleta madhara makubwa kwao kwa sababu mimi binafsi nilikua nasikia kauli nyingi kwa watu vijiweni hapa Mwanza kua na sisi tutampigia kura wa kwetu kanda yetu,hili jambo ni baya hapa Tanzania likipamba moto,ikumbukwe kwamba kanda ya ziwa ina watu wengi sana na wakiamua kupiga kura kwa wingi juu ya chama fulani lazima chama hcho kitoboe,lakini pia jambo hli tukubali lina ukweli ndani yake na liepukwe,jaribu kufikili ukiitamka CCM pamoja na mabaya yake lakini huwezi ona CCM ni ya wapi kwa maana ya ukanda,utaiona CCM pote Tanzania,lakini ukiitamka CDM katika masikio ya watu na ufahamu wao wanaiona picha ya ukanda wa Arusha na Kilimanjaro,hili ni kosa kubwa,nchi hii ni kubwa mno ya makabila kwa makabila na ktk chama chochote wanapaswa kuiondoa hii picha.ASANTE
 
Nilichokiona mimi huku kanda yetu ya ziwa ni dhahili Lowasa ameshindwa kwa haki na hajaibiwa kura yoyote,CDM ktk kipindi kijacho wajitahidi sana kuondoa uongozi wenye vinasaba vya ukanda mmoja,lakini pia kama wapinzani wawe wanaangalia na kauli za kuwaaminisha watanzania alafu baada ya muda wanageuka tena na kwa jambo lile lile na kulisafisha,hapo nazungumzia kauli walizozitoa za ufisadi wa EL na kisha kuja kumsafisha tena,kuna watanzania siyo waongeaji ila wanajua kupima mambo na wanaamua kupitia sanduku la kura.swala la ukanda liwepo au lisiwepo lakini limeleta madhara makubwa kwao kwa sababu mimi binafsi nilikua nasikia kauli nyingi kwa watu vijiweni hapa Mwanza kua na sisi tutampigia kura wa kwetu kanda yetu,hili jambo ni baya hapa Tanzania likipamba moto,ikumbukwe kwamba kanda ya ziwa ina watu wengi sana na wakiamua kupiga kura kwa wingi juu ya chama fulani lazima chama hcho kitoboe,lakini pia jambo hli tukubali lina ukweli ndani yake na liepukwe,jaribu kufikili ukiitamka CCM pamoja na mabaya yake lakini huwezi ona CCM ni ya wapi kwa maana ya ukanda,utaiona CCM pote Tanzania,lakini ukiitamka CDM katika masikio ya watu na ufahamu wao wanaiona picha ya ukanda wa Arusha na Kilimanjaro,hili ni kosa kubwa,nchi hii ni kubwa mno ya makabila kwa makabila na ktk chama chochote wanapaswa kuiondoa hii picha.ASANTE

Maneno kuntu. Subiri nyumbu waje kutoa mapovu.
 
Inapendeza kuona mtu kama Pasco anaanza kuruhusu akili zake halisi kufanya kazi.

Nashukuru kwamba angalau ule ushawishi wako unaanza kuupeleka kwenye jambo muhimu "kushirikiana na Rais aliyetangazwa mshindi kuijenge nchi yetu"

Kwenye uchangiaji wangu niliwahi kumshambulia MM wakati ule wa kampeni kwamba ilifikia mahali hakua anajua aende wapi aligeuka popo umbo la ndege kumbe mnyama. Tunapofika kwenye maslahi mapana ya nchi swala mahaba, ushabiki na kejeli ni vya kuachwa.

JPM angalau mpaka sasa anaipeleka nchi tulipo papigania sote. Sote kama watanzania tumuunge mkono.

Thumb up bro Pasco
 
Mkuu Pasco Kumbuka ni mungu na mbio uctegemee unakimbizwa na simba ukakaa chini na wala ucpge kelele au kufanya njia yeyote ya kujiokoa ukategemea mungu anacho fanya lowassa ni sawa kama kweli anauhakika kweli kaibiwa kura ukiona jambo baya linafanyka kama unauwezo liondoe kwa mikono au nguvu yako au lisemee ila kila m2 ajue ni baya ya mwisho na ambayo ni dhaifu ni kuchukia na kuondoka
 
Last edited by a moderator:
Mwache lowassa alalamike maana haisaidii kitu, JK alikuwa raisi japo naye alifika kipindi akaanza kulalama...PINDA naye hivyo hivyo.....upinzani wanalalamika....chama tawala hivyo hivyo...mawaziri wanalalamika na wabunge pia....wananchi huku ndo kabisa,,,ni walalamishi kupindukia....yote haya ni kelele za chura.......
 
CCM ina wanachama takribani milioni saba, katika hao ukipigiwa kura na milioni tano tu, halafu ukaokota milioni tatu za wasio wanachama wake tayari hizo ni kura milioni nane zinazotosha kumpa mtu uraisi.

Next time wapinzani inabidi wakakite miguu huko vijijini.
Pia wahimize turn out ya wapiga kura, ili advantage ya wananchi wasio na vyama iweze kuoffset advantage ya CCM kwa wanachama wake, hapo Wapinzani watafanya vizuri zaidi.
 
Hili jambo linamgeuza huyu mzee aonekane kama mchekeshaji, nilishaandika mada hapa kumshauri astaafu siasa za ushindani, bado anaendelea tu, anatafuta aibu ya kuondoka nayo. Mshaurini tena apumzike.
 
Fisadi Lowasa anajua fika kwamba ameshindwa kihalali kabisa na hili alilijua tangu wakati anahamia chadema kwamba hakuna jinsi ambavyo angeweza kuishinda CCM kwa kura ila kilichokuwa kunamsukuma ni kwamba baada ya CCM kumuondoa kwenye uraisi ina maana alikuwa anakuwa irrelevant kwenye siasa za TanZania na fisadi Lowasa ni mtu anayependa kuabudiwa na kutukuzwa nafikiri hiyo ni hulka yake ni ngumu sana kuishi bila ya kuwa relevant hivyo alichotaka kufanya kwa kwenda chadema ni kwamba alifikiri kwamba angeweza kupata kura nyingi ingawaje alijua siyo kuizidi CCM ili asusie matokeo halafu kuishinikiza Serikali kwa kupitia jumuiya ya kimataifa kwamba aliibiwa kura na hivyo jumuiya ya Kimataifa kufanya kama walivyofanya Kenya kuishinikiza serikali yetu kuunda Serikali ya umoja wa Kitaifa model yake akiwa Maalim Seif na ndiyo maana walikuwa karibu hiyo ndiyo ilikuwa Plan B ya fisadi Lowasa baada ya kukatwa na CCM lkn kwa bahati mbaya kwa upande wake wazungu walimpuuzia na kumpotezea akabaki hana wakumkingia kifua ndiyo kila siku ulisikia mara sijui ICC mara ICJ n.k!

Sasa kwa kuwa ni hulka yake kupenda kuwa relevant na kupenda ukubwa ndiyo maana kila apatapo nafasi huongea jambo ambalo litampa air time tena na kundelea kujadiliwa kama tunavyofanya hapa basi huitumia, kwa maana sasa hivi kila kona ya nchi ni Magufuli tu sasa fisadi Lowasa anapenda sana kuwa relevant na hii haimfurahishi, swali linabakia tu kama hii strategy yake ya kutaka kuwa relevant itawaimarisha au kuwabomoa chadema, muda tu ndiyo utatoa jibu la hilo swali, lkn chadema wana kazi ngumu sana ya kudili na super ego ya fisadi Lowasa!


OTH_6079.jpg


 
Back
Top Bottom