Hamjambo wakulungwa!
1. Robert ninapoandika maandiko na makala zangu. Mwanasaikolojia atakuwa na uwezo wa kuchambua Makala na content niliyoandika lakini hataweza kuchambua hisia, mtazamo na kilichopo moyoni mwangu.
2. Mfano, wasomaji wengi wa Makala zangu huniona kama mwanaume mchukia Wanawake, mwenye mfumo dume, Mkali Sana. Au mwenye maneno yamoja Kwa Moja. Hivyo wanaweza kunichambua hivyo kutokana na maandiko Yangu.
3. Lakini uhalisia ukawa mwingine kabisa. Kwamba maandiko au makala hazithibitishi tabia, na hisia za mwandishi.
4. Kwani Mwandishi anaweza kuandika kwa ukali lakini yeye moyoni asiwe mkali. Anaweza kuandika kwa uchungu. Lakini moyoni wala asiwe na uchungu.
5. Mimi watu wengi hasa wanawake wananiona kama Mchukia wanawake. Lakini wanaonijua, wanaoishi pamoja na mimi watatoa maoni tofauti.
6. Ndivyo ilivyo kwa Watoa hotuba. Mtoa hotuba anapozungumza unaweza kuchambua contents anayozungumza lakini huwezi kuchambua hisia zake za ndani.
7. Kwa mchambuzi na mwanahabari kitaaluma wanajua sio maadili kuweka maoni binafsi ya mwandishi katika kuchambua hisia binafsi za mtu ambazo kimsingi huwezi kuthibitisha.
8? Contents anayohutubia unaweza kuichambua kwa sababu inathibitika. Umeisikia au kuisoma. So unaweza kusema contents hii imeandikwa na mtu anayeonekana alikuwa na hasira.
9.
Pascal Mayalla kusema Mwigulu Nchemba alikuwa amechukia ni kosa la kiuchambuzi na kiuandishi. Kwa sababu Hana uwezo WA kuthibitisha jambo hilo.
10. Ila angesema Mwigulu alionekana kuchukia aliposema blah blah blahm hapo Pascal angekuwa sahihi kwa asilimia Mia moja kwani amem-judge Mwigulu kulingana na content na context iliyokuwepo.
Lakini ushahidi hana.
11. Mwigulu anaweza kusema sikuwa nimechukia. pascal hataweza kuthibitisha kwamba Mwigulu alichukia au hakupenda.
12. Kuonekana umechukia na kuchukia ni mambo mawili tofauti.
Kuonekana unapenda na kupenda ni mambo mawili tofauti.
13. Hakuna uthibitisho wa hisia za mtu kisaikolojia ila viashiria vinaweza kutoa maana zaidi ya moja na kulingana na mtu na mtu.
14. MTU anaweza akalia na akawa na furaha. Yaani akalia kwa furaha.
MTU anaweza akacheka lakini akacheka kwa huzuni au kebehi.
15. Wanafasihi wao ndio wanaweza kuchambua Jambo kivyovyote kwani sisi tunatoa maoni yetu katika kazi ya Sanaa.
16. Muandishi wa habari sio Mwanafasihi ila anaweza kutumia vipengele vya Fasihi.
Mwandishi anatakiwa kutoa habari, kuripoti habari kama ilivyo. Ukweli.
17. Maoni ya mwandishi WA habari yajikite kwenye contents kuliko hisia za mtu kwani kujikita kwenye hisia za mtu lazima uzue taharuki, lazima uripoti uongo kwa sababu unaongea Jambo ambalo huna ushahidi nalo.
18. Alionekana anafuraha.
19. Ingawaje kesi kama hizi zinaweza kuendeshwa kisiasa au kwa mrengo wa siasa. Kwani Wapo waandishi huchambua hisia za watu na hapa ni viongozi wengine katikaa namna ya kuwasifia. Na waandishi hao hawajawahi kuambiwa wathibitishe uchambuzi wao kwa viongozi hao.
20. Wachambuzi na watangazaji mara kadhaa tumekuwa tukiwasikia wakichambua hisia za watu ambazo hazithibitishiki.
Mfano utasikia mtangazaji akisema, "Namuona Mhe. Rais akifurahia pale. Mambo anayoyapenda Sana haya"
Kisa amemwona Raia anatabasamu na kucheka.
Wakati ingetakiwa kwa mwandishi aseme" Namuona Mhe Rais akitabasamu na akicheka sana. Anaonekana kufurahia pale. Hakika huenda haya ndio mambo ayapendayo"
Hiyo ni kwa muandishi mweledi.
21. Wanafasihi wao ndio wapo huru kutoa maoni kwenye kazi zao. Wao wanachanganya uandishi wa habari, Sanaa ya lugha na maoni Yao kulingana na interest, ujumbe, dhamira n.k.
22. Kwenye kesi kama hiyo kwa Mwanafasihi anachomoa asubuhi tuu kwa sababu msingi mkuu wa wanafasihi ni maoni ya mtunzi na mwandishi. Sio kile ambacho msomaji atatafsiri.
23. Hiyo inaitwa kufungwa break kidogo. Hatari Sana.
Kufikia hapo sina la ziada.
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam