Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge

Mbona kama kamewadharau sana hawa wajumbe wa kamati? Wangekaagiza kavue kwanza hiyo miwani, ona kanavyowaangalia kwa dharau!! Bunge letu linaongozwa na mataahira!!
 
Haya uhakika zaidi anao yeye mwenyewe.....
Wasukuma oyeeeh!
Ila isiwe katoka huko na ugonjwa wa kulainika ghafla kama yule mtu flani!
Afu kesha mshinda Muro hapo
 
Mwandishi wa kujitegemea, Ndg. Pascal Mayala (katikati) akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kuandika habari yenye maudhui ya kudharau Bunge kwenye safu yake ya gazeti la Rai Mwema

Amefika hapo ikiwa ni baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kuagiza Ndg. Pascal Mayala pamoja Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema wafikishwe mbele ya kamati hiyo.

Habari zaidi, soma => Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge
Kwa ninavyomjua Paschal, ni mtu muungwana ambaye naamini hata hiyo Kamati itakuwa imemuelewa.
 
Mwandishi wa kujitegemea, Ndg. Pascal Mayala (katikati) akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kuandika habari yenye maudhui ya kudharau Bunge kwenye safu yake ya gazeti la Rai Mwema

Amefika hapo ikiwa ni baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kuagiza Ndg. Pascal Mayala pamoja Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema wafikishwe mbele ya kamati hiyo.

Habari zaidi, soma => Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge
Naona Suti yako ilikuwa imefunika Mzee mayala, dressing code waige kwako mzee
 
Hao Wajumbe hapo moja ya Sharti lao wakiwemo humo ' Chumbani ' waliambiwa ni lazima wote wawe wamenuna kama vile wamelamba ' Limao ' mbichi?
 
Pascal ana hoja.
Hi tabia ya kuzuia kuambiwa naona imekithiri sana.
Ni kweli kuwa muhimili wa bunge unaingiliwa sana. Mfano halali ni pale mkuu wa kaya alipomwambia spika awashughulikie wapinzani ndani ya bunge, wakitoka nje ana deal nao. Ile ni kama amri na imeingilia madaraka ya spika.


Tanzania inapotea kidemokrasia

Wakati nikiwa Sekondari, kuna siku kulitokea ugomvi darasani kati ya mwl na mwanafunzi. Ilikuwa hivi: huyo mwl alikuwa akifundisha Chemistry, ila ki ukweli alikuwa mwl 'siyawezi'! Nadahni watu wazima wananielewa hapa. Sasa kuna mwanafunzi badala ya kumsikiliza mwl, akawa anaandika nukuu (notes) za somo jingine. Mwl alipomwona aling'aka, akafura, akamkwida shingoni. Baada ya yule mwanafunzi kukosa hewa, akajitetea na yeye akamkwida mwl.

Baadaye mwl. akatoa taarifa kwa Headmaster kuwa ameshambuliwa na mwanafunzi. Wote tukajua kuwa yule mwanafunzi atafukuzwa shule. Sasa siku moja tuliitwa ofisini kwa Headmaster kama mashahidi tulioshuhudia tukio hilo. Mwl husika hakuwepo ofisini. Baada ya ushahidi wote kutolewa, Headboy ambaye naye alikuwepo ofisini akamlipua mwl kuwa ni mwl 'siyawezi'! Wote tukajua atashughulikiwa. Cha ajabu Headmaster alimshukuru sana na alisema maneno haya: 'Umetusaidia sana kujua chanzo cha tatizo, kwa sababu Serikali ya wanafunzi ni jicho la tatu la utawala ambalo kazi yake ni kuona kule ambako utawala hauwezi kuona'.

Sasa hii kesi ya brother Paschal naifananisha na ile ya mwanafunzi na mwl. Ina maana hawa waheshimiwa sana hawataki kuoneshwa kule ambako hawawezi kuona, hawataki kukosolewa kwa kuwa wanadhani hawawezi kukosea. Sasa kama wanadhani wao ni wakamilifu hawakosei, huko makanisani na misikitini wanakoshinda tunawaona kwenye ma kamera wame bow na kunyeyekea wanaenda kufanya nini? Wanamdhihaki Mungu? Maana kwa sisi Wakristo tunaamini kwamba sisi ni wenye dhambi, na hata Yesu alitumwa kutukomboa wakosefu, akafa msalabani kwa ajili yetu!

Lakini uzuri, Mungu hamfichi mnafiki. Jaribu kuangalia picha za hao wajumbe wa kamati. Hakuna hata mmoja ambaye amemwangalia usoni Paschal. Ni kama their faces are guilt. Hawana confidence na kitu wanachokifanya, kwa hiyo ni unafiki tu! Kwa sababu, kama wanavyodai mtuhumiwa amelidharau Bunge which is a serious allegation. Nilitegemea wajumbe wote wam face Paschal squarely ili waone Eye activity ya Paschal ambayo kitaalam itawapa dondoo kama ana hatia ama la! Hapa nadhani wataalam wa interrogation watanielewa.

Lakini mwisho wa siku, haya yote yana mwisho. Kitu cha milele ni Mungu tu, lakini madaraka, cheo, pesa, utajiri ni vya kupita tu!
 
Back
Top Bottom