Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge

Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge

Kunyamazia persecutions is the best medicine!, hata Yesu pale msalabani, hakupiga kelele!.
P
Usilete mambo ya imani hapa tupo kwenye mambo ya Siasa kwenye hilo uliferi mkuu hata hapa utakataa wakina Stive Biko wangekaa kimya Nchi yao mpaka kesho ingekua na ubaguzi wa rangi kelele zao unaona kilichotokea wewe ulitishwa ukaamua kufata maamuzi yao ulikua sahihi ingawaje maombi yetu yalijibu yule aliekutisha nae alipata aibu kubwa mimj binafsi nilikua upande wako naomba tuishie hapa uzuri upo ok na yalishapita...
 
Mwandishi wa kujitegemea, Ndg. Pascal Mayala (katikati) akihojiwa na Kamati ya kudumu ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kosa la kuandika habari yenye maudhui ya kudharau Bunge kwenye safu yake ya gazeti la Rai Mwema

Amefika hapo ikiwa ni baada ya Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai kuagiza Ndg. Pascal Mayala pamoja Wahariri wa Gazeti la Raia Mwema wafikishwe mbele ya kamati hiyo.

Habari zaidi, soma => Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge
Naikumbuka hii, Kipindi hicho Ndugai wa moto
 
Sina chuki binafsi na watajwa hapo juu. Inakera mibaba mizima inapokubali na kukumbatia uchawa ili ijaze mitumbo yao.

Ukisiliza matamko ya watajwa, unaishia kusononeka na kukata tamaa. Huyu kiumbe anaipeleka wapi nchi?
Wajuzi wa mambo tusaidie.

Tufanye nini kuondokana na Uchafu na uchawa huu wa kujitakia kwa baadhi yetu wajiitao viongozi? Taifa lonateketea tukiona. Tutawambia nini watoto na wajukuu zetu?
Mkuu Faza, Father of All , nakushauri kuwa makini sana unapozungumza lolote kuhusu Bunge letu tukufu!, mwenzio nilipouliza tuu maswali haya, Wabunge Wetu wa Ajabu!, Wanaachaje Bunge Lijipendekeze Kwa Serikali!, Wanajua Wajibu Wao?. Check 'n' Balance Itoke Wapi? na Sehemu ya Pili: Je, Bunge letu tukufu linajipendekeza kwa Serikali?, na Bunge butu linaloingiliwa na kunyamaza, linapojikomba na kujipendekeza kwa Rais, linaweza kweli kuisimamia Serikali?!, cha moto nilikipata!, lilitokea jinga fulani, likashika lile gazeti na kunishitaki kwa Spika kuwa nimesema Bunge Linajipendekeza!, Mbunge kama huyu, ukiwaita baadhi ya wabunge wetu ni vilaza, utakuwa umewakosea?, Spika nae akapanic!,
Spika aagiza mwandishi Pascal Mayalla na Wahariri wa gazeti la Raia Mwema wahojiwe kwa kulidhalilisha Bunge niliitwa kuhojiwa na Kamati ya Bunge kwa tuhuma za kulidhalilisha Bunge!, Pascal Mayalla ahojiwa na kamati ya Bunge kufika kule tukayamaliza kiutu uzima!

Afadhali enzi hizo, vilaza walikuwa ni wabunge tuu na Spika, ambao hawaingii kwenye cabinet, lakini sasa vilaza ni hadi waheshimiwa mawaziri wetu ambao wanaingia kwenye cabinet!, kama waziri mzima anakuwa kilaza hivi, bungeni! unategemea nini akiwa ndani ya cabinet?!.
P
 
Back
Top Bottom