=========
Asante ndugu kwa kuuliza,kwani Kuuliza si Ujinga!!
Ukumbbuke kuwa, PASAKA ni sherehe pekee duniani inayoadhimishwa kipindi kimoja/hicho hicho na imani 2 za dini kongwe duniani: UYAHUDI (Judaism) na UKRISTO.
Sasa, kwa kuwa PASAKA ni adhimisho la UHURU wa Waisraeli kutoka utumwani Misri zaidi ya miaka 6,000 iliyopita, basi Mungu aliwaambia Waisraeli (Wayahudi) waadhimishe siku hii kila mwaka.
Mwaka huu 2014, Pasaka kwa Wayahudi imesherehekewa Jumatatu na Jumanne (Tarehe 14 na 15 April). Kalenda yetu hii (Gregorian Calendar) hufanyiwa mahesabu ili kuoanisha na Kalenda ya Kiyahudi kujua Pasaka otakuwa lini. Ina maana kuwa,tarehe zile ambazo Pasaka ya Kiyahudi itaadhimishwa, ndizo tarehe ambazo Kalenda ya Pasaka kwa Wakristo inapaswa kuonesha Jumapili ya karibu ili PASAKA iadhimishwe kwa Wakristo.
NB: Kwa Wakristo Paska sharti iangukie siku ya Jumapili kwani ndiyo siku Yesu Kristo alifufuka toka kwa wafu kwa kipindi kile cha kuadhimisha Pasaka miaka ile. Yesu yu hai leo hii, milele na milele zote. Kwa Wayahudi, Kalenda yao haifuati Jua bali ni Mwezi, na hivyo Pasaka yao yaweza angukia siku yoyote ile. In short, Pasaka ya Wakrito lazima iongozwe na ratiba ya Kiyahudi kuhusiana na Pasaka.