Part 4: TISS bado safari ngumu

Part 4: TISS bado safari ngumu

Mkuu kuna swali niliuliza posti zilizopita, bila shaka katika hizi mada watu wa kitengo wapo wengi tu. Swali langu imekuwaje tiss wakaachia nchi ikapata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wenye tatizo la afya ya akili. Tiss ipo na inasemwa iko imara na makini kulikoni?
Kwanza jiulize wewe na watanzania wote mlikuwa wapi hadi TISS ikawa hivyo..ukipata jibu la hilo swali ni rahisi kujibu swali lako wewe mwenyewe.
 
Umesema vyema...usalama wa nchi - ukienda kinyume nao wanakuwa kazini jkama jina lao linavosomeka .. Mnyonge mpeni haki yake hawa jamaa wamepigana kweli kuiokoa nchi na mpasuko wa kidini wamepigana vita ngumu ya dawa za kulevya na baba lao ukwapuaji wa madini (maslahi ya wenye dunia)..tuwaangalie kwa jicho + jamani wamefanya mengi...
As long as niko salama na ndugu zangu wako salama bila kusahau majirani na watanzania wa eneo nililopo. Basi nachekea kusema Tz ni nchi ya maziwa na asali. Lets keep this peace
 
Mkuu mimi nataka nikubali kuwa TISS imeingiliwa na chama, na hii ni bahati mbaya.

Akili za vongozi wetu tuwaonao sasa huku uraiani zinaakisi akili za hao hao watu / viongozi wa TISS. Hamna kitu, tumeramba galasa waswahili wanasema.!
 
Tatizo Ninaloliona Ndan Ya Idara Yetu Ni Kugawanyika Kwa Idara Katika Vipande Viwili .

Kuna Wanaoleta Habari Za Kweli Na Mafaili Yamejaa Makao Makuu Ya Idara Na Ikulu Ila Cha Kushangaza Hayafanyiwi Kazi Na Mamlaka Wanachoambulia Ni Kupigwa Bench ( Yaan Wanakuwa Ndan Ya Idara Ila Uamz Hawana)

Kundi La Pili Ni Wafia Chama Wanao leta Habari Za Umbea Kama Walivyowafanyia Wakina Simbachawene Kipind Kile, Anthony Mtaka Na Wengine Kibao.

Ili Kund La Pili Lina Nguvu Kuliko La Kwanza Ndio Maana Unaona yanayoendelea xaxa
Dah hapo nilipokoleza rangi ndugu yangu nakusihi jirekebishe.
 
Mm nadhani Tatatizo lina anzia kwenye udaili wa watumishi wa TISS vetting yako inakuwa hovyo sana, mfano Uvccm na Jkt....

Tatizo lingine ni Sheria ya kuanzishwa kwa TISS, yani tiss wapo kama wambea tu, kazi yao ni kukusanya na kuchakata, taharifa then kutoa ushauri, sasa ushauri unao tolewa haufanyiwi kazi kwa wakati mda mwingine haufanyiwi kazi kabisa. Hivyo tiss ni kibogoyo mpiga umbea tu.

Ushauri.
Tiss wapewe meno na waongezewe budget ya kutosha.
Udaili wao uwe smart kama wa CIA. Maana wote tunajuwa Jkt wengi wanao ende kule ni kwasababu ya uhaba wa ajira. Uvccm wengi ni njaaa na kukosa kazi sehemu nyingine pia hawana elemi ya kutosha, wengi husoma baada ya kuingia idaran. Kuna watu smart ndani ya tasisi za umma, udaili ufanyike vyuoni, mashulen na kwenye idara nyingine za serekali.
 
Tatizo Ninaloliona Ndan Ya Idara Yetu Ni Kugawanyika Kwa Idara Katika Vipande Viwili .

Kuna Wanaoleta Habari Za Kweli Na Mafaili Yamejaa Makao Makuu Ya Idara Na Ikulu Ila Cha Kushangaza Hayafanyiwi Kazi Na Mamlaka Wanachoambulia Ni Kupigwa Bench ( Yaan Wanakuwa Ndan Ya Idara Ila Uamz Hawana)

Kundi La Pili Ni Wafia Chama Wanao leta Habari Za Umbea Kama Walivyowafanyia Wakina Simbachawene Kipind Kile, Anthony Mtaka Na Wengine Kibao.

Ili Kund La Pili Lina Nguvu Kuliko La Kwanza Ndio Maana Unaona yanayoendelea xaxa
Mkuu badilisha hiyo xaxa isomeke sasa ili kulinda utu uzima wako
 
Naunga mkono hoja

yaani kwa idadi ya comments na Threads nilizozianzizha humu, nikizicompile vizuri naweza kuandika Thesis ya PhD iliyosimama kabisa, halafu eti atokee mtu mon
mmoja asiyejielewa huko TISS kwa sababu ya ulevi tu wa madaraka aagize eti fungia JF
Yaani inamaana hawaoni madini yaliyomo humu JF hata ukiweka siasa pembeni!

Sio kila Mtu anaweza kutambua Thamani ya Mawazo ya baadhi ya Watu Mkuu ,Wajinga na wasio fikiri sawa sawa wana thaminisha Vitu vinavyo shikika na kusahau haya yote tunayo yaona yalikuwa ni Mawazo ya Watu/Mtu ila yalio tekelezwa kwa Vitendo.
 
Mm nadhani Tatatizo lina anzia kwenye udaili wa watumishi wa TISS vetting yako inakuwa hovyo sana, mfano Uvccm na Jkt....

Tatizo lingine ni Sheria ya kuanzishwa kwa TISS, yani tiss wapo kama wambea tu, kazi yao ni kukusanya na kuchakata, taharifa then kutoa ushauri, sasa ushauri unao tolewa haufanyiwi kazi kwa wakati mda mwingine haufanyiwi kazi kabisa. Hivyo tiss ni kibogoyo mpiga umbea tu.

Ushauri.
Tiss wapewe meno na waongezewe budget ya kutosha.
Udaili wao uwe smart kama wa CIA. Maana wote tunajuwa Jkt wengi wanao ende kule ni kwasababu ya uhaba wa ajira. Uvccm wengi ni njaaa na kukosa kazi sehemu nyingine pia hawana elemi ya kutosha, wengi husoma baada ya kuingia idaran. Kuna watu smart ndani ya tasisi za umma, udaili ufanyike vyuoni, mashulen na kwenye idara nyingine za serekali.

Ni kweli Mkuu uyasemayo ila wakiwepo ma 'Genious' kwenye Idara wanaweza kwenda mbele zaidi ya hapo kumfanya Mtawala atimize (Bila ya kujijua) yale aliyo shauriwa.Tatizo ndio Mzee ndio nyingi kwa Sababu ya Kapu kuwa na Magarasa mengi ,so wanaishia ktk Hali kama uliyo isema wewe ..
 
Umesema vyema...usalama wa nchi - ukienda kinyume nao wanakuwa kazini jkama jina lao linavosomeka .. Mnyonge mpeni haki yake hawa jamaa wamepigana kweli kuiokoa nchi na mpasuko wa kidini wamepigana vita ngumu ya dawa za kulevya na baba lao ukwapuaji wa madini (maslahi ya wenye dunia)..tuwaangalie kwa jicho + jamani wamefanya mengi...

Mhhhhh ..
 
Mkuu nchi imejaliwa kuwa na vichaa wengi sana.
Kibaya zaidi wengi wa vichaa hao wanamamlaka ya kufanya maamuzi ya kitaifa kama taifa hatuna budi kufanya maamuzi magumu.
Ila wewe nimekutana na comments zako kadhaa unaonekana una shida. Kila kitu ni kupinga. Kibaya huna point hata za maana.
Kweli kilamtu hutoa alicho nacho...
 
Asante sana mkuu Kihava ktk comment yako post #87, umenikumbusha mbali sana.
Kabla sijaendelea nainukuu post yako Kama ilivyo kwa faida ya wengine ili wajue nini maana ya usalama wa taifa na una umuhimu gani kwa nchi.

"TISS ndio nchi yenyewe kama hujui. Hata ungekuwa na elimu kiasi gani huwezi kufanya jambo lolote la maana kama TISS hawataki. Nakuhakikishia hata kama una uwezo wa kujenga kiwanda kikubwa kiasi gani, kilichopo eneo halali kabisa kama TISS hawataridhika na wewe huwezi! Wewe ni 'mgeni' kwenye utawala wa nchi. Nchi ina wenyewe, sisi wengine hata tungekuwa na cheo kikubwa kiasi gani kama TISS wakisema NO! Huwezi kwenda tofauti nao 'ukaishi'. Hata huyu mzee wetu vituko anavyofanya vya kuwaumiza wenzake ni kwamba TISS wameridhia. Wakisema hatutaki hiki lifanyike hana ubavu wa kukataa. Maan ukiwakatalia wanachokisema kwa maslahi ya nchi basi wewe utaondoka ili Taifa libaki salama. Kwa hiyo kwa ujumla TISS ndio mhimili wa nchi. Hakuna anayeweza 'kukohoa' mbele ya TISS kama wakisema hili hapana. Kwa hiyo hata Musiba TISS waliamua wamwache afanye atakavyo, lakini wangesema MUSIBA 'stop' misiba yako hatuitaki hangekuwa na jeuri ya kuendelea kufanya chochote. Hivyo ndugu yangu jua ya kwamba hakuna mwenye ubavu kuliko TISS ndani ya nchi yoyote duniani. TISS ikiwa dhaifu nchi itakuwa dhaifu tuuuu! Tunaiombea TISS ya nchi yetu iwe imara kwa Taifa imara."

Mwisho wa kunukuu.

Baada ya mashambulizi ya kigaidi Marekani Sept 11,Rais George Walker Bush alifanya kikao cha siri Whitehouse chini ya handaki akiwa na waziri wake wa mambo ya nje, Condollezza Rice, mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerari Tommy Franks, pamoja na mkurugenzi mkuu wa CIA Bob Tenet.

Katika kikao hicho Bush alimwambia Bob Tenet kwamba, hakuna Marekani bila CIA imara, CIA ingelikuwa legelege Marekani ingekuwa magofu hapa Duniani au ingekuwa ombaomba na maskini wa kutupwa.

Naandika makala hii kwa uchungu sana, nashangaa Kuna watu wanaleta siasa ktk jambo gumu wakati mimi nazungumzia mustakabali wa taifa letu Halafu watu wanaleta habari ya vyama vya siasa.

Makala hii haina U Chadema wala U CCM, ni maalumu kwa ajili ya taifa lenu.
Marekani, Uingereza, Ujerumani, Japan ,Sweden, Norway Finland, Australia, Canada, viongozi hawana ujanja chini ya idara za usalama wa taifa linapokuja suala la usalama wa nchi na maslahi ya uchumi,huwa wanafanyiwa zengwe na kutolewa.

Mungu ibariki Jamiiforums, makala hii ingelikuwa kwenye Gazeti la hard copy ingekuwa imeshapata misukosuko mikubwa Kama kufungiwa Gazeti na mwandishi kukamatwa.

Pia Mungu ibariki Kenyan forum, hiyo pia imechangia uwepo wa JF, waliona kabisa kwamba endapo wataifungia JF bado tungehamia jumla Kenyan forum ambako ndo ingekuwa hatari kwa sababu watu wangetapika nyongo bila breki, bora hapa kuna speed governor.

Mungu mbariki Maxence Melo kwa kuanzisha huu mtandao unaotikisa Dunia kwa sasa .

INAENDELEA
Mkuu kichwa cha uzi na pointi unazotoa haziendani. Inaonyesha kabisa hujafika level ya uchambuzi wa maswala ya security. Jisomee vya kutosha ili uweze kutema madini. Kwa sasa kichwa cha uzi kinakufunika sana. Unaongelea swala sensitive na muhimu lakini kwenye contents huweki lolote zaidi ya mipasho.
 
Condoleezza Rice alikuwa mshauri wa masuala ya usalama wa rais Bush katika awamu yake ya kwanza awamu ya pili aliteuliwa kuwa secretary of state.
Secretary of State kipindi cha September 11 alikuwa Colin Powell.
 
Mm nadhani Tatatizo lina anzia kwenye udaili wa watumishi wa TISS vetting yako inakuwa hovyo sana, mfano Uvccm na Jkt....

Tatizo lingine ni Sheria ya kuanzishwa kwa TISS, yani tiss wapo kama wambea tu, kazi yao ni kukusanya na kuchakata, taharifa then kutoa ushauri, sasa ushauri unao tolewa haufanyiwi kazi kwa wakati mda mwingine haufanyiwi kazi kabisa. Hivyo tiss ni kibogoyo mpiga umbea tu.

Ushauri.
Tiss wapewe meno na waongezewe budget ya kutosha.
Udaili wao uwe smart kama wa CIA. Maana wote tunajuwa Jkt wengi wanao ende kule ni kwasababu ya uhaba wa ajira. Uvccm wengi ni njaaa na kukosa kazi sehemu nyingine pia hawana elemi ya kutosha, wengi husoma baada ya kuingia idaran. Kuna watu smart ndani ya tasisi za umma, udaili ufanyike vyuoni, mashulen na kwenye idara nyingine za serekali.
Hata kama wakiongezewa bajeti ya pesa. Iwapo waliopo ndio hawa hawa tusitarajie mabadiliko yoyote zaidi ya kujiingiza kwenye matatizo mengine. Kinachotakiwa ni kaunagalia namna ya kuokoa na kufikiri namna ya kusonga mbele. Hapa tunaweza kujiuliza, je waliopo wanaweza kutuvusha? Kama hawawezi ni nini kifanyike?
 
Back
Top Bottom