Part 4: TISS bado safari ngumu

Part 4: TISS bado safari ngumu

Mkuu kuna swali niliuliza posti zilizopita, bila shaka katika hizi mada watu wa kitengo wapo wengi tu. Swali langu imekuwaje tiss wakaachia nchi ikapata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wenye tatizo la afya ya akili. Tiss ipo na inasemwa iko imara na makini kulikoni?
acha tuone vile atajibu hili swali lako
 
Asante sana mkuu Kihava ktk comment yako post #87, umenikumbusha mbali sana.
Kabla sijaendelea nainukuu post yako Kama ilivyo kwa faida ya wengine ili wajue nini maana ya usalama wa taifa na una umuhimu gani kwa nchi.


"TISS ndio nchi yenyewe kama hujui. Hata ungekuwa na elimu kiasi gani huwezi kufanya jambo lolote la maana kama TISS hawataki. Nakuhakikishia hata kama una uwezo wa kujenga kiwanda kikubwa kiasi gani, kilichopo eneo halali kabisa kama TISS hawataridhika na wewe huwezi! Wewe ni 'mgeni' kwenye utawala wa nchi. Nchi ina wenyewe, sisi wengine hata tungekuwa na cheo kikubwa kiasi gani kama TISS wakisema NO! Huwezi kwenda tofauti nao 'ukaishi'. Hata huyu mzee wetu vituko anavyofanya vya kuwaumiza wenzake ni kwamba TISS wameridhia. Wakisema hatutaki hiki lifanyike hana ubavu wa kukataa. Maan ukiwakatalia wanachokisema kwa maslahi ya nchi basi wewe utaondoka ili Taifa libaki salama. Kwa hiyo kwa ujumla TISS ndio mhimili wa nchi. Hakuna anayeweza 'kukohoa' mbele ya TISS kama wakisema hili hapana. Kwa hiyo hata Musiba TISS waliamua wamwache afanye atakavyo, lakini wangesema MUSIBA 'stop' misiba yako hatuitaki hangekuwa na jeuri ya kuendelea kufanya chochote. Hivyo ndugu yangu jua ya kwamba hakuna mwenye ubavu kuliko TISS ndani ya nchi yoyote duniani. TISS ikiwa dhaifu nchi itakuwa dhaifu tuuuu! Tunaiombea TISS ya nchi yetu iwe imara kwa Taifa imara."

Mwisho wa kunukuu.

Baada ya mashambulizi ya kigaidi Marekani Sept 11,Rais George Walker Bush alifanya kikao cha siri Whitehouse chini ya handaki akiwa na waziri wake wa mambo ya nje, Condollezza Rice, mkuu wa majeshi ya Marekani Jenerari Tommy Franks, pamoja na mkurugenzi mkuu wa CIA Bob Tenet.
Katika kikao hicho Bush alimwambia Bob Tenet kwamba, hakuna Marekani bila CIA imara, CIA ingelikuwa legelege Marekani ingekuwa magofu hapa Duniani au ingekuwa ombaomba na maskini wa kutupwa.
Naandika makala hii kwa uchungu sana, nashangaa Kuna watu wanaleta siasa ktk jambo gumu wakati mimi nazungumzia mustakabali wa taifa letu Halafu watu wanaleta habari ya vyama vya siasa.
Makala hii haina U Chadema wala U CCM, ni maalumu kwa ajili ya taifa lenu.
Marekani, Uingereza, Ujerumani, Japan ,Sweden, Norway Finland, Australia, Canada, viongozi hawana ujanja chini ya idara za usalama wa taifa linapokuja suala la usalama wa nchi na maslahi ya uchumi,huwa wanafanyiwa zengwe na kutolewa.
Mungu ibariki Jamiiforums, makala hii ingelikuwa kwenye Gazeti la hard copy ingekuwa imeshapata misukosuko mikubwa Kama kufungiwa Gazeti na mwandishi kukamatwa.
Pia Mungu ibariki Kenyan forum, hiyo pia imechangia uwepo wa JF, waliona kabisa kwamba endapo wataifungia JF bado tungehamia jumla Kenyan forum ambako ndo ingekuwa hatari kwa sababu watu wangetapika nyongo bila breki, bora hapa kuna speed governor.
Mungu mbariki Maxence Melo kwa kuanzisha huu mtandao unaotikisa Dunia kwa sasa .

INAENDELEA
Mkuu ACHA KUOTA MCHANA PLS, acha kulinganisa mataifa ambayo inaheshimu sio tu sheria lakini HAKI ZA BINADAMU, Tz ni taifa linaongozwa na WANAFIKI WA CCM, wako wauaji na hata akili hawana, ona vile uchumi umeaporomoka kabisa, tazama korosho na mengine, hizo mataifa umetaja kina marekani , germany, japan na zingine hizo ni mataifa sheria inaheshimimwa na pia watu huchaguliwa kwa misingi ya ujuzi na elimu yao, angalia kina wale jiwe anachagua kaa makonda, dc saa mbaya, rc happy kule iringa kweli kaa hao tiss wana jali hali ya uchumi na mambo kaa hayo bona hawakumupa ushauri ulio bora jiwe jinsi ya kuchagua viongozi, kubali tu tz is a very poor under developed country which has very CLUE LESS LEADERS,inspite of having you heaping praises on tiss which is lead by uvccm crooks
 
Umeandika ukweli mtupu Mkuu hao wahuni waliosukumiziwa TISS na dikteta kwa kulazimisha kutoka CCM sasa hivi ndiyo wametake over TISS na ndiyo chanzo cha Kapilima kupigwa chini.

Tatizo Ninaloliona Ndan Ya Idara Yetu Ni Kugawanyika Kwa Idara Katika Vipande Viwili .

Kuna Wanaoleta Habari Za Kweli Na Mafaili Yamejaa Makao Makuu Ya Idara Na Ikulu Ila Cha Kushangaza Hayafanyiwi Kazi Na Mamlaka Wanachoambulia Ni Kupigwa Bench ( Yaan Wanakuwa Ndan Ya Idara Ila Uamz Hawana)

Kundi La Pili Ni Wafia Chama Wanao leta Habari Za Umbea Kama Walivyowafanyia Wakina Simbachawene Kipind Kile, Anthony Mtaka Na Wengine Kibao.

Ili Kund La Pili Lina Nguvu Kuliko La Kwanza Ndio Maana Unaona yanayoendelea xaxa
 
Nchi yoyote ambayo taasisi nyingine au watu binafsi wana nguvu zaidi ya taasisi za usalama,haiwezi kubaki salama.
Unachosema mkuu pamoja na bwana Kivava ndivyo inavyopaswa kuwa.

Ukiona haiko hivyo, kwamba kuna watu au network ya watu regardless ya nafasi zao kwenye jamii, wana nguvu zaidi ya intelijensia ya nchi, basi ujue shida ni kubwa.

Taasisi yetu kwa maoni yangu,inataka kuharibiwa now, na wanasiasa.Na hii ni kutokana na loopholes kwenye sheria za nchi.

Tuweke sawa sheria yetu iipe nguvu kubwa intelijensia ya nchi kiutendaji na kimuundo, lakini pia kiusalama zaidi ni vema tukawa na kitu kimoja kinachoitwa intelijensia ambacho kimegawanywa kwa taasisi mbalimbali zenye mgawanyo wa majukumu kulingana na mahitaji ya nchi kwenye kila nyanja inayogusa mtanzania.

Mfumo wa intelijensia ni kama binadamu alivyo kimaumbile, kichwa kimoja, kinafanya coordination ya maeneo yote ya mwili kwa kupitia nerves. Shughuli zinafanyika maeneo husika kwenye misuli na kemikali zilizo special kwa kiungo, lakini lazima pawe na mawasiliano from head. Kichwa ni kichwa tu, hakiwezi kusema kinasimama pekee bila viungo vingine, wala hamna kiungo kinachoweza kusimama pekee bila vingine, kila kimoja kina kazi yake,ila vyote viko coordinated na kichwa.

Nchi ni kama mwili, intelijensia ni kama ubongo na nerves za fahamu, kuwe na taasisi kuu inayofanya coordination na taasisi nyingine zinazotekeleza majukumu ya kiintelijensia kulingana na matakwa ya nchi.

Matakwa ya nchi yagawanywe, kile kilichopo na kile kinachohitajika kuwepo. Matakwa ya nchi yajulikane kwa maswali yanayojitokeza kupitia uzoefu wa kiitelijensia kwa taasisi zote in coordination, sio maswali yanayoulizwa na viongozi wa nchi tu.

Unapokuwa na intelijensia ambayo muda wote iko busy kutafuta majibu kwa maswali yanayoulizwa na mtu mmoja au wawili sababu ya powers walizo nazo kimfumo,then you are dead as a nation, yanasubiriwa mazishi tu.

Kwa sababu inafika kipindi hata kichwa huwa kinapewa taarifa ya baadhi ya activity ambazo zimeshafanyika na kiungo bila kusubiri zaidi, maana ni urgent,meaning kwamba components za mfumo zinahitajiana, sio moja kuburuza nyingine.

Kama kweli tunataka kuibadili nchi yetu na kukimbizana na maendeleo ya dunia ya leo, hatuna budi kuanza na intelijensia ya nchi,lazima ifumuliwe, itanuliwe sana na kuanza upya. Lakini tunahitaji watu sahihi kuwaingiza na kuwatumia huko. Kila mahali tunahitaji intelijensia, hospitali, michezoni, muzikini, siasani, jeshini.. just everywhere penye shughuli-binadamu, lazima kuwe na intelijensia inayokusanya data, kupeleka kichwani na kuimpose response kulingana na maslahi ya nchi, na malengo yake. Kuna mahali huhitaji siasa, bali sayansi, sasa kama intelijensia imejaa siasa tu, unawezaje kudeal na mambo ya kisayansi? lazima utakosea. Intelijensia ni pana mno, na nchi inavyokuwa, mahitaji yanaongezeka, hamwezi kubaki na akili ile ile, lazima iwe "akili kubwa".

Dunia ya sasa, nchi zote makini, lazima intelijensia yake iwe na vitengo ambavyo ni research based kwenye mambo mazito kama uchumi, sayansi, demographics, mabadiliko ya tabia jamii, sera na mahitaji ya kimataifa etc. Sijui tiss yetu iko level zipi kwenye hili, sijui kwa kweli, wasiwasi wangu ni kuwa huenda taasisi ni ndogo kuliko inavyotakiwa kuwa kwa sasa.
 
Mkuu kuna swali niliuliza posti zilizopita, bila shaka katika hizi mada watu wa kitengo wapo wengi tu. Swali langu imekuwaje tiss wakaachia nchi ikapata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wenye tatizo la afya ya akili. Tiss ipo na inasemwa iko imara na makini kulikoni?
TISS ni dhaifu ndo maana tuna viongozi wa hovyo
 
Nchi yoyote ambayo taasisi nyingine au watu binafsi wana nguvu zaidi ya taasisi za usalama,haiwezi kubaki salama.
Unachosema mkuu pamoja na bwana Kivava ndivyo inavyopaswa kuwa.
Ukiona haiko hivyo,kwamba kuna watu au network ya watu regardless ya nafasi zao kwenye jamii,wana nguvu zaidi ya intelijensia ya nchi,basi ujue shida ni kubwa.
Taasisi yetu kwa maoni yangu,inataka kuharibiwa now,na wanasiasa.Na hii ni kutokana na loopholes kwenye sheria za nchi.
Tuweke sawa sheria yetu iipe nguvu kubwa intelijensia ya nchi kiutendaji na kimuundo,lakini pia kiusalama zaidi ni vema tukawa na kitu kimoja kinachoitwa intelijensia ambacho kimegawanywa kwa taasisi mbalimbali zenye mgawanyo wa majukumu kulingana na mahitaji ya nchi kwenye kila nyanja inayogusa mtanzania.
Mfumo wa intelijensia ni kama binadamu alivyo kimaumbile,kichwa kimoja,kinafanya coordination ya maeneo yote ya mwili kwa kupitia nerves.Shughuli zinafanyika maeneo husika kwenye misuli na kemikali zilizo special kwa kiungo,lakini lazima pawe na mawasiliano from head.Kichwa ni kichwa tu,hakiwezi kusema kinasimama pekee bila viungo vingine,wala hamna kiungo kinachoweza kusimama pekee bila vingine,kila kimoja kina kazi yake,ila vyote viko coordinated na kichwa.
Nchi ni kama mwili,intelijensia ni kama ubongo na nerves za fahamu,kuwe na taasisi kuu inayofanya coordination na taasisi nyingine zinazotekeleza majukumu ya kiintelijensia kulingana na matakwa ya nchi.
Matakwa ya nchi yagawanywe,kile kilichopo na kile kinachohitajika kuwepo.Matakwa ya nchi yajulikane kwa maswali yanayojitokeza kupitia uzoefu wa kiitelijensia kwa taasisi zote in coordination,sio maswali yanayoulizwa na viongozi wa nchi tu.
Unapokuwa na intelijensia ambayo muda wote iko busy kutafuta majibu kwa maswali yanayoulizwa na mtu mmoja au wawili sababu ya powers walizo nazo kimfumo,then you are dead as a nation,yanasubiriwa mazishi tu.
Kwa sababu inafika kipindi hata kichwa huwa kinapewa taarifa ya baadhi ya activity ambazo zimeshafanyiwa tathmini na kiungo bila kusubiri zaidi,maana ni urgent,meaning kwamba components za mfumo zinahitajiana,sio moja kuburuza nyingine.
Kama kweli tunataka kuibadili nchi yetu na kukimbizana na maendeleo ya dunia ya leo,hatuna budi kuanza na intelijensia ya nchi,lazima ifumuliwe,itanuliwe sana na kuanza upya.Lakini tunahitaji watu sahihi kuwaingiza na kuwatumia huko.Kila mahali tunahitaji intelijensia,hospitali,michezoni,muzikini,siasani,jeshini..just everywhere penye shughuli-binadamu,lazima kuwe na intelijensia inayokusanya data,kupeleka kichwani na kuimpose response kulingana na maslahi ya nchi,na malengo yake.Kuna mahali huhitaji siasa,bali sayansi,sasa kama intelijensia imejaa siasa tu,unawezaje kudeal na mambo ya kisayansi?lazima utakosea.Intelijensia ni pana mno,na nchi inavyokuwa,mahitaji yanaongezeka,hamwezi kubaki na akili ile ile,lazima iwe "akili kubwa".
Dunia ya sasa,nchi zote makini,lazima intelijensia yake iwe na vitengo ambavyo ni research based kwenye mambo mazito kama uchumi,sayansi,demographics,mabadiliko ya tabia jamii,sera na mahitaji ya kimataifa etc.Sijui tiss yetu iko level zipi kwenye hili,sijui kwa kweli,wasiwasi wangu ni kuwa huenda taasisi ni ndogo kuliko inavyotakiwa kuwa kwa sasa.

Hili bandiko ni la kisomi haswa!
Hongera sana mkuu kwa uchambuzi makini.

Ni kupoteza muelekeo kwa TISS kutumika kisiasa, kuumiza wapinzani wakati wapinzani wapo kwa mujibu wa katiba ambayo ni sehemu na nguzo kuu ya Usalama wa nchi.

Chombo cha Intelijensia kinachotumika na kubariki mtu afunguliwe kesi ya kubumba isiyodhaminika halafu ikawaachia baada ya kupata kinguvu wanachokitaka kisicho halali yao kutoka kwa huyo mtu ni Idara muflisi!

Au Idara ambayo mawazoni mwa watendaji wake wanadhani wana deni la kuisaidia CCM kisiasa kupata advantage dhidi ya wapinzani ni idara isiyojua haswa ni nini lengo la yenyewe kuwepo.

Ngoja niwakumbushe TISS Taifa Maana yake nini

Taifa ni Ardhi, Anga, Maji na vilivyomo katika hivyo vitu plus Watu yaani wanaume kwa wanawake na Mali zao na Utamaduni wao na Mifumo na Taasisi zao kama vile serikali zao, Siasa zao, Ulinzi wao, Mifumo ya uchumi wao, huduma mbalimbali n. k

Sasa TISS ikiligeuza Taifa kuwa ni Serikali, Viongozi wake na CCM basi TISS hiyo inabidi iwapeleke tena watumishi wake shule ili wajue Taifa maana yake nini haswa!
 
Ila wewe nimekutana na comments zako kadhaa unaonekana una shida. Kila kitu ni kupinga. Kibaya huna point hata za maana.
Kweli kilamtu hutoa alicho nacho...
Huyu atakuwa lile choko lilotolewa nishai majuzi. Laana ya kuwekwa kinyumba na mzungu na ya kuzaa na dada yake inamtafuna
 
Tatizo Ninaloliona Ndan Ya Idara Yetu Ni Kugawanyika Kwa Idara Katika Vipande Viwili .

Kuna Wanaoleta Habari Za Kweli Na Mafaili Yamejaa Makao Makuu Ya Idara Na Ikulu Ila Cha Kushangaza Hayafanyiwi Kazi Na Mamlaka Wanachoambulia Ni Kupigwa Bench ( Yaan Wanakuwa Ndan Ya Idara Ila Uamz Hawana)

Kundi La Pili Ni Wafia Chama Wanao leta Habari Za Umbea Kama Walivyowafanyia Wakina Simbachawene Kipind Kile, Anthony Mtaka Na Wengine Kibao.

Ili Kund La Pili Lina Nguvu Kuliko La Kwanza Ndio Maana Unaona yanayoendelea xaxa
Una uhandishi wa kitoto sana
 
Mkuu kuna swali niliuliza posti zilizopita, bila shaka katika hizi mada watu wa kitengo wapo wengi tu. Swali langu imekuwaje tiss wakaachia nchi ikapata baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wenye tatizo la afya ya akili. Tiss ipo na inasemwa iko imara na makini kulikoni?
Kama nani? Jiwe ama bashite?
 
Tatizo Ninaloliona Ndan Ya Idara Yetu Ni Kugawanyika Kwa Idara Katika Vipande Viwili .

Kuna Wanaoleta Habari Za Kweli Na Mafaili Yamejaa Makao Makuu Ya Idara Na Ikulu Ila Cha Kushangaza Hayafanyiwi Kazi Na Mamlaka Wanachoambulia Ni Kupigwa Bench ( Yaan Wanakuwa Ndan Ya Idara Ila Uamz Hawana)

Kundi La Pili Ni Wafia Chama Wanao leta Habari Za Umbea Kama Walivyowafanyia Wakina Simbachawene Kipind Kile, Anthony Mtaka Na Wengine Kibao.

Ili Kund La Pili Lina Nguvu Kuliko La Kwanza Ndio Maana Unaona yanayoendelea xaxa

Nyie mnaoilalamikia TISS kila kukicha, hebu jaribuni kwanza kufanya utafiti wa kina kuhusiana na hiyo Taasisi yenyewe kwanza.

Fanyeni utafiti TISS ukilinganisha na Taasisi zingine za Ujasusi ktk nchi zingine mbalimbali, kuizingatia suala LA Sheria, na Kanuni za Taasisi husika, Miundo yao ya Utendaji, Recruitment systems zake, n.k.

Narudia tena kusema kuwa, tatizo kubwa linaloikabili TISS linatokana NA kuwepo kwa Sheria mbaya , Kanuni, Miongozo NA Taratibu zilizopo ambazo hazifai zinazosimamia utekelezaji wa shughuli za kila siku za Taasisi yenyewe.
Sheria na Kanuni ni mbaya, zimepitwa na wakati, hazifai NA wala hazina tija ktk Kulinda NA Kuitetea Maslahi mapana ya umma wa wananchi wa Tz.

USHAURI ILI IWEPO TISS NZURI TZ

1.KUREKEBISHA SHERIA

Yafanyike Marekebisho ya Sheria, Kanuni, Miongozo mbalimbali inayotumika ktk kusimamia uendeshaji wa Shughuli za kila siku za Taasisi hii nyeti kabisa, TISS .
Bila kusahau kurekebisha Katiba ya nchi.
Sheria na Kanuni zibadilishwe ili ziendane na mahitaji ya wakati wa sasa wa Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, Utandawazi, Ushindani wa Kiuchumi kupitia nguvu ya Soko.

TISS ijikite zaidi NA ielekeze nguvu zaidi ktk kufanya UJASUSI wa Kiuchumi, badala ya Ujasusi wa Kisiasa ambao hauna tija yoyote ile kwa maslahi mapana ya umma.
TISS iwe ni Taasisi ya UKOMBOZI WA KIUCHUMI KWA Watz, KWA sababu adui mkubwa zaidi KWA sasa nchini Tz ni Umaskini na Uchumi mbaya kwa nchi na wananchi wake KWA ujumla

2.KUFANYA MAPINDUZI YA FIKRA KUPITIA "ELIMU BORA"

Elimu Bora ni silaha nzito zaidi kuliko zote ili kuleta maendeleo endelevu yaliyo ya kweli mahali popote pale. Bila ya Elimu bora hakuna maendeleo ya kweli, kamwe maendeleo hawawezi kuja KWA miujiza isipokuwa kupitia Elimu bora.
Wananchi wote wahimizwe kuhusu suala la Elimu bora.
TISS nayo ifanye recruitment ya Watu wenye upeo mkubwa, ambao watakuwa na tija ktk Taasisi hiyo NA KWA nchi KWA ujumla. Watu waajiriwe kulingana na UWEZO wao NA taaluma zao walizonazo, wala siyo kutokana na mitazamo yao ya kiitikadi kwenye masuala ya Kisiasa kama ilivyo hivi sasa.

ELIMU (Intelligence) ndio nguzo kuu kabisa ktk kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake yote kwenye Taasisi yoyote ile ya Ujasusi popote pale duniani, ndio maana zinaitwa "INTELLIGENCE SECURITY AGENCY"


3.KUUNDA TAASISI ILIYO COMPETENT KIUTENDAJI

Taasisi hii ni nyeti sana ktk nchi yoyote ile, hivyo basi, inatakiwa itawaliwe na weledi WA hali ya juu kabisa ktk utendaji wao wa kazi, isiingilwe hovyo hovyo kiutendaji na wanasiasa.Ni hatari sana KWA Usalama wa nchi NA wananchi wake.

Endapo kama wanasiasa na watu wengine wasiohusika watakuwa na maamuzi kwenye Taasisi nyeti kabisa kama hii, hatari yake ni kwamba badala ya kuwa Taasisi ya Usalama WA Taifa itageuka NA kuwa Taasisi HATARI ZAIDI kwa Usalama WA nchi NA wananchi wake. Itakuwa ni "Genge LA Mauaji" ktk nchi husika, "Mafia Gangs", na mifano hao ipo mingi sana kwenye hili, e.g. KGB, GESTAPO, etc.

Isipokee maagizo ya hovyo hovyo kutoka WA Wanasiasa NA kuyatekekeza pasipo na kuyafanyia upembuzi yanikifu kwanza, uzalendo na maslahi mapana ya umma yawekwe mbele kwanza KWA kila uamuzi au muafaka unaofikiwa au KWA kila jambo litakaloamriwa NA Taasisi hii.

Mfano mzuri wa maamuzi bora kabisa ya kizalendo KWA maslahi mapana ya umma ni kupitia tukio moja LA kisa cha kweli huko nchini Afrika Kusini. "Mamlaka" ziliwahi kutoa Amri za Kuua (Assassination Orders ) zikipendekeza kuuliwa kwa mwanasiasa kijana wa upinzani, ambaye ni machachari zaidi na mkosoaji mkubwa zaidi wa Serikali Bwana Julius Malema. Baadhi ya Wajumbe wa Security Committees ambao kisheria wana mamlaka ya kuidhinisha assassination orders kabla ya kutekelezwa kwake, walipinga pendekezo hili la kumuua huyo mwanasiasa. Pale Mamlaka zilipoendelea kutoa pendekezo hili kwa kurudia rudia, baadhi ya wajumbe WA Security committee walikerwa na badala yake waliamua kuvujisha taarifa hizi nyeti kabisa kwa umma ili kuzima kabisa hilo jaribio ovu la kumuua huyo mwanasiasa.
 
Mleta mada uko sahihi.
Kipindi kile Wameifungia JF kwa miezi miwili tulipata hifadhi ya ukimbizi Kenya Forum
Kule tulitapika nyongo haswa kutokana na kukerwa na tabia za uminywaji wa haki za kutoa maoni.

laiti wasingeturudishia JF yetu tungebaki Kenya Forum.
Yaani Jamaa wana mambo ya ajabu sana, yaani wako tayari data, elimu nzito iliyomo kwenye archives za JF izimike na ipotee ilimradi tu kumlinda Jiwe dhidi ya criticisms tu za kawaida za kisiasa.
Leo hii ukigoogle kitu kuhusu Tanzania, JF inatokea kama sehemu mojawapo ya Kukupa Taarifa, Sasa cha ajabu hawa jamaa walitaka JF ife na hazina hii ya data.
Ajabu sana!
Hilo jambo la data kupotea huku wao wakiona ni sawa tu ndio lililokuwa likinistaajabisha mno. Ila nimejifunza kitu hapo juu "sisi wote ni wageni wa utawala" hata ukiwa na akili za kuzidi dunia kama jamaa hawakutaki hautakaa uishi.... ktk mfumo uliostahili kuishi
 
Hili bandiko ni la kisomi haswa!
Hongera sana mkuu kwa uchambuzi makini.
Ni kupoteza muelekeo kwa TISS kutumika kisiasa, kuumiza wapinzani wakati wapinzani wapo kwa mujibu wa katiba ambayo ni sehemu na nguzo kuu ya Usalama wa nchi.
Chombo cha Intelijensia kinachotumika na kubariki mtu afunguliwe kesi ya kubumba isiyodhaminika halafu ikawaachia baada ya kupata kinguvu wanachokitaka kisicho halali yao kutoka kwa huyo mtu ni Idara muflisi!

Au Idara ambayo mawazoni mwa watendaji wake wanadhani wana deni la kuisaidia CCM kisiasa kupata advantage dhidi ya wapinzani ni idara isiyojua haswa ni nini lengo la yenyewe kuwepo.

Ngoja niwakumbushe TISS Taifa Maana yake nini
Taifa ni Ardhi,Anga, Maji na vilivyomo katika hivyo vitu plus Watu yaani wanaume kwa wanawake na Mali zao na Utamaduni wao na Mifumo na Taasisi zao kama vile serikali zao, Siasa zao, Ulinzi wao, Mifumo ya uchumi wao, huduma mbalimbali n. k

Sasa TISS ikiligeuza Taifa kuwa ni Serikali, Viongozi wake na CCM basi TISS hiyo inabidi iwapeleke tena watumishi wake wajue Taifa maana yake nini haswa!
Ccm ni mfa maji haishi kutapatapa, ndiyo mana unaona hata humu wapo wale wa buku 7. Hata TISS imebidi lumumba fc wapelekwe kulinda maslai yao huko.
 
Mimi nimeanza kujua maana ya TISS miaka ya hapa baada ya Baba wa taifa kututoka, kabla ya hapo, hawa watu huwajui ila wapo, na cha ajabu siku hizi wanatajwa hadharani na wao pia wajitokeza kwenye "live" mtindo wa kisasa, wakikemea mambo.
Yaani Siku hizi wana dili na............ ...... ....... Sio umasikini au rushwa, ufisadi, na mengine..... Mbaya zaidi sasa wanajulikana kama wafia chama na sio Nchi.
Mmmh
 
Umeandika ukweli mtupu Mkuu hao wahuni waliosukumiziwa TISS na dikteta kwa kulazimisha kutoka CCM sasa hivi ndiyo wametake over TISS na ndiyo chanzo cha Kapilima kupigwa chini.
Mamlaka ya Rais ni makubwa kuliko mamlaka ya Taasisi yoyote Tanzania kulingana na mfumo uliopo, kwa mfumo uliopo, TISS sichochote kwa Magu kwa sasa anaweza kufanya lolote.

Pamoja na mapungufu aliyokuwa nayo Kipilimba, hajaondolewa kwasababu ya mapungufu hayo bali ameondolewa kwenye nafasi yake sababu hafanyi yanayomfurahisha Magu personally.

Naomba ufanye utafiti, Magu hajawahi hata siku moja kumuondosha mtu kazini anayemsifia, anayefanya matakwa yake ambayo hayana maslahi kwa Taifa, n.k. Hatakama atakuwa anavunja Katiba, Sheria za nchi, mtu huyo atabaki salama hata guswa na mtu yeyote au chombo chochote!.
 
Na huyo dikteta na nduli wa chato ndiye anayefanya mambo kwa maslahi ya Taifa siyo!? 😳

Kudharau katiba, bunge, Mahakama, ofisi ya CAG, kuteka, kubambikia kesi wasio na hatia na kuwafunga. kutesa na hata kuua? Kukwapua 1.5 trillion hazina na kujichotea trillions hazina bila idhini ya Bunge.

Hayo ndiyo maslahi ya Taifa yanayofanywa na huyo nduli na dikteta siyo!?

Mamlaka ya Rais ni makubwa kuliko mamlaka ya Taasisi yoyote Tanzania kulingana na mfumo uliopo, kwa mfumo uliopo, TISS sichochote kwa Magu kwa sasa anaweza kufanya lolote.

Pamoja na mapungufu aliyokuwa nayo Kipilimba, hajaondolewa kwasababu ya mapungufu hayo bali ameondolewa kwenye nafasi yake sababu hafanyi yanayomfurahisha Magu personally.

Naomba ufanye utafiti, Magu hajawahi hata siku moja kumuondosha mtu kazini anayemsifia, anayefanya matakwa yake ambayo hayana maslahi kwa Taifa, n.k. Hatakama atakuwa anavunja Katiba, Sheria za nchi, mtu huyo atabaki salama hata guswa na mtu yeyote au chombo chochote!.
 
Back
Top Bottom