Nchi yoyote ambayo taasisi nyingine au watu binafsi wana nguvu zaidi ya taasisi za usalama,haiwezi kubaki salama.
Unachosema mkuu pamoja na bwana Kivava ndivyo inavyopaswa kuwa.
Ukiona haiko hivyo,kwamba kuna watu au network ya watu regardless ya nafasi zao kwenye jamii,wana nguvu zaidi ya intelijensia ya nchi,basi ujue shida ni kubwa.
Taasisi yetu kwa maoni yangu,inataka kuharibiwa now,na wanasiasa.Na hii ni kutokana na loopholes kwenye sheria za nchi.
Tuweke sawa sheria yetu iipe nguvu kubwa intelijensia ya nchi kiutendaji na kimuundo,lakini pia kiusalama zaidi ni vema tukawa na kitu kimoja kinachoitwa intelijensia ambacho kimegawanywa kwa taasisi mbalimbali zenye mgawanyo wa majukumu kulingana na mahitaji ya nchi kwenye kila nyanja inayogusa mtanzania.
Mfumo wa intelijensia ni kama binadamu alivyo kimaumbile,kichwa kimoja,kinafanya coordination ya maeneo yote ya mwili kwa kupitia nerves.Shughuli zinafanyika maeneo husika kwenye misuli na kemikali zilizo special kwa kiungo,lakini lazima pawe na mawasiliano from head.Kichwa ni kichwa tu,hakiwezi kusema kinasimama pekee bila viungo vingine,wala hamna kiungo kinachoweza kusimama pekee bila vingine,kila kimoja kina kazi yake,ila vyote viko coordinated na kichwa.
Nchi ni kama mwili,intelijensia ni kama ubongo na nerves za fahamu,kuwe na taasisi kuu inayofanya coordination na taasisi nyingine zinazotekeleza majukumu ya kiintelijensia kulingana na matakwa ya nchi.
Matakwa ya nchi yagawanywe,kile kilichopo na kile kinachohitajika kuwepo.Matakwa ya nchi yajulikane kwa maswali yanayojitokeza kupitia uzoefu wa kiitelijensia kwa taasisi zote in coordination,sio maswali yanayoulizwa na viongozi wa nchi tu.
Unapokuwa na intelijensia ambayo muda wote iko busy kutafuta majibu kwa maswali yanayoulizwa na mtu mmoja au wawili sababu ya powers walizo nazo kimfumo,then you are dead as a nation,yanasubiriwa mazishi tu.
Kwa sababu inafika kipindi hata kichwa huwa kinapewa taarifa ya baadhi ya activity ambazo zimeshafanyika na kiungo bila kusubiri zaidi,maana ni urgent,meaning kwamba components za mfumo zinahitajiana,sio moja kuburuza nyingine.
Kama kweli tunataka kuibadili nchi yetu na kukimbizana na maendeleo ya dunia ya leo,hatuna budi kuanza na intelijensia ya nchi,lazima ifumuliwe,itanuliwe sana na kuanza upya.Lakini tunahitaji watu sahihi kuwaingiza na kuwatumia huko.Kila mahali tunahitaji intelijensia,hospitali,michezoni,muzikini,siasani,jeshini..just everywhere penye shughuli-binadamu,lazima kuwe na intelijensia inayokusanya data,kupeleka kichwani na kuimpose response kulingana na maslahi ya nchi,na malengo yake.Kuna mahali huhitaji siasa,bali sayansi,sasa kama intelijensia imejaa siasa tu,unawezaje kudeal na mambo ya kisayansi?lazima utakosea.Intelijensia ni pana mno,na nchi inavyokuwa,mahitaji yanaongezeka,hamwezi kubaki na akili ile ile,lazima iwe "akili kubwa".
Dunia ya sasa,nchi zote makini,lazima intelijensia yake iwe na vitengo ambavyo ni research based kwenye mambo mazito kama uchumi,sayansi,demographics,mabadiliko ya tabia jamii,sera na mahitaji ya kimataifa etc.Sijui tiss yetu iko level zipi kwenye hili,sijui kwa kweli,wasiwasi wangu ni kuwa huenda taasisi ni ndogo kuliko inavyotakiwa kuwa kwa sasa.