Part 4: TISS bado safari ngumu

Part 4: TISS bado safari ngumu

Kama tiss ni imara na inafanya kazi kwa maslahi ya nchi ilikuwaje ikaruhusu yafuatayo:1Kati ya wagombea urais 42 ccm kwanini iliruhusu wagombea wenye sifa na weledi wa kutosha wakaachwa wakaletwa hawa? 2.Kwanini iliruhusu mkuu wa nchi Magu kuharibu uchumi wa nchi kwa kupandisha kodi, kusumbua wafanyabiashara mpaka wakafunga biashara zao 3. Kwanini waliruhusu Magu akabadili sheria akapandisha tozo na ushuru mbalimbali bandarini mpaka wafanyabiashara wa nchi za jirani wakaihama bandari yetu hivyo kupoteza mapato. 4.Kwanini wameruhusu Magufuli kubomolea watu maelfu ya nyumba zao, ambapo Magufuli hajapata chochote wala nchi haijapata chochote zaidi ya hasara. 5.Kwanini wameruhusu Magufuli kufukuzana Wafanyakazi vyeti feki wakati wamekaa kwenye utumishi muda mrefu, mfano walimu wamefundisha watu ambao wako ofisini mpaka sasa wakati wao wameondolewa, kwanini amewaacha vyeti feki jeshini , polisi,magerezani, uhamiaji na tiss ? Haya amewafukuza amepata nini sasa? 6.Kwanini tiss wameruhusu Magufuli ateue wakuu wa mikoa na wilaya wasiokuwa na sifa wengine wagonjwa wa afya ya akili.Tiss si wananguvu ya kumlazimisha rais afanyaje kwa maslahi ya nchi, vipi matilioni yamepotea 2.4 sehemu ya fedha hizo voti namba ishirini Ikulu. 7. Kwanini Tiss wameruhusu rais anunue ndege na kufanya matumizi mengine ya pesa za umma bila idhini ya bunge wala kufuata sheria ya manunuzi ya umma, hapa nina respond kwenye posti na 87, yapo mengi tu tiss hebu tusaidieni huu ni mtazamo tu kwa maslahi mapana ya nchi.
 
Pamoja na ukweli kuwa mashirika ya ujasusi ni mhimu katika usalama wa mataifa husika, taifa letu lina bahati mbaya ya kuwa na usalama wa taifa wanaotuhumiwa kuhalifu maisha ya wananchi kila kukicha.
Kama TISS imeundwa ili kuwang'ang'azia WaTZ utawala wa CCM basi tuna hasara kubwa.
 
Mkuu kichwa cha uzi na pointi unazotoa haziendani. Inaonyesha kabisa hujafika level ya uchambuzi wa maswala ya security. Jisomee vya kutosha ili uweze kutema madini. Kwa sasa kichwa cha uzi kinakufunika sana. Unaongelea swala sensitive na muhimu lakini kwenye contents huweki lolote zaidi ya mipasho.
unataka niseme TISS ipo chini ya kagame ndo ujue nimetema madini au unatakaje kwa mfano?
 
Kama tiss ni imara na inafanya kazi kwa maslahi ya nchi ilikuwaje ikaruhusu yafuatayo:1Kati ya wagombea urais 42 ccm kwanini iliruhusu wagombea wenye sifa na weledi wa kutosha wakaachwa wakaletwa hawa? 2.Kwanini iliruhusu mkuu wa nchi Magu kuharibu uchumi wa nchi kwa kupandisha kodi, kusumbua wafanyabiashara mpaka wakafunga biashara zao 3. Kwanini waliruhusu Magu akabadili sheria akapandisha tozo na ushuru mbalimbali bandarini mpaka wafanyabiashara wa nchi za jirani wakaihama bandari yetu hivyo kupoteza mapato. 4.Kwanini wameruhusu Magufuli kubomolea watu maelfu ya nyumba zao, ambapo Magufuli hajapata chochote wala nchi haijapata chochote zaidi ya hasara. 5.Kwanini wameruhusu Magufuli kufukuzana Wafanyakazi vyeti feki wakati wamekaa kwenye utumishi muda mrefu, mfano walimu wamefundisha watu ambao wako ofisini mpaka sasa wakati wao wameondolewa, kwanini amewaacha vyeti feki jeshini , polisi,magerezani, uhamiaji na tiss ? Haya amewafukuza amepata nini sasa? 6.Kwanini tiss wameruhusu Magufuli ateue wakuu wa mikoa na wilaya wasiokuwa na sifa wengine wagonjwa wa afya ya akili.Tiss si wananguvu ya kumlazimisha rais afanyaje kwa maslahi ya nchi, vipi matilioni yamepotea 2.4 sehemu ya fedha hizo voti namba ishirini Ikulu. 7. Kwanini Tiss wameruhusu rais anunue ndege na kufanya matumizi mengine ya pesa za umma bila idhini ya bunge wala kufuata sheria ya manunuzi ya umma, hapa nina respond kwenye posti na 87, yapo mengi tu tiss hebu tusaidieni huu ni mtazamo tu kwa maslahi mapana ya nchi.
Post #87 naona bado hujaielewa vizuri mkuu, mleta Post alikuwa anazungumzia nguvu waliyonayo TISS endapo wakiamua jambo flani, ila kwa sababu wanatumika kisiasa na wengi wao ni mambumbumbu ya kutupwa ya UVCCM ndo maana ni Kama hatuna TISS tu
 
Mbona kafupi mno ila ukweli ni kuwa usalama wa taifa lazima ujitenge na vyama vya siasa. Hii idara ndiyo injini ya nchi. Wengine watakuja na Sera na ilani zao ila msingi na itikadi ya nchi lazima ubaki
 
Idara imejaa ma form four failures, inawezaje kuwa na umuhimu wote huo kwa TAIFA. Nadhani mleta mada unachanganya kitu.

Usiforce objectives za CIA na akina MOSAD ndio ziwe objectives za TISS.
 
Post #87 naona bado hujaielewa vizuri mkuu, mleta Post alikuwa anazungumzia nguvu waliyonayo TISS endapo wakiamua jambo flani, ila kwa sababu wanatumika kisiasa na wengi wao ni mambumbumbu ya kutupwa ya UVCCM ndo maana ni Kama hatuna TISS tu
TISS wametoa wapi hayo mamlaka makubwa namna hiyo jamani.
Katiba yetu inasemaje juu ya hao TISS.

Au tupeni mfano wa hiyo post no.87.
eti TISS isipotaka kiwanda kijengwe hakijengwi, seriously?

Mambo mangapi ya hovyo kabisa yanafanyika kila awamu kuanzia awamu ya kwanza mpaka ya sasa ambayo yalipaswa kushughurikiwa na aina ya kikaragosi mnachokizungumzia hapa na hayakutendewa haki?

Anza na vita vya Kagera, TISS ilikuwa wapi japo kuwatonya masoja kwamba Amin anafikiria upuuzi alioishia kuutenda?
Mauaji ya kimbali ya Rwanda na dhahama yaliyotuletea watanzania, kuanzia mafuriko ya wakimbizi na sasa jamii ya kinyarwanda iliyotapakaa kila kona ya nchi, TISS hawakuyaona haya?
Uwekezaji sekta ya madini na sasa gas? Tiss walikuwa wapi?
TISS walishindwa nini kumcontroll nyerere na Kawawa na mambo yao ya vijijii vya ujamaa?
Mpaka leo hatujaambiwa Mwalimu alikufa kufaje huko jerumani? TISS wako wapi?
walimu wa vodafasta wa lowassa, TISS hawakuwaona?
wakati MUNGAI anafuta elimu ya michezo mashule hili halikuwa tishio la usala kwa Taifa? au mimi ndio mjinga?
TISS ndio walimuelekeza JECHA kufanya yake? kwa nini hawakuona kilichokuwa kinakuja na kukiachia mpaka kututia aibu namna hii?
Yuko wapi Balali?
Muungano wa Africa mashariki wakati unavunjika, hawakuhitajika TISS kulinda maslahi ya Taifa?
UKIMWI,Maradhi ya Sukari, Maradhi ya Cancer, Maralia na sasa Tabia za kishoga, TISS hawaoni kama ni tishio kwa Usalama wa Taifa?

Siwaelewi.
Hawa ni ghost security personell, security kwa maana ya kupambana na vibaka na mambo yasiyo maalumu.
sina namna bora zaidi ya kuwaelezea.
 
Leo nimeelewa kwanini afisa usalama(TISS) kwanini huogopwa sana popote aendapo, iwe kwenye majeshi au hata taasisi za kiraia.
 
TISS hii ni taasisi mhimu katika nchi yetu, haya magufuli anayoyafanya yana baraka zote toka kwa taasisi hii kwahiyo miradi yote yamaendeleo anayotekeleza Raisi magufuli inahitaji mtu mwenye maamuzi magumu kama jpm, unazani kuondoa watumishi wenye vyeti feki ni mchezo lilihitaji maamuzi magumu, Kwahiyo tuzidi kumsapoti Raisi wetu mpendwa na Taasisi yetu hii ndio inayotufanya tuwe kisiwa chaamani,
 
Bado hajawatoa vyeti feki jeshini, polisi, uhamiaji, magereza na usalama wa taifa anasubiri nini?
 
Post #87 naona bado hujaielewa vizuri mkuu, mleta Post alikuwa anazungumzia nguvu waliyonayo TISS endapo wakiamua jambo flani, ila kwa sababu wanatumika kisiasa na wengi wao ni mambumbumbu ya kutupwa ya UVCCM ndo maana ni Kama hatuna TISS tu
Sasa mkuu na mimi ninaona hayo niliyoyataja ni muhimu sana imekuwaje tiss wakashindwa kumzuia rais kufanya hayo maana nguvu hiyo si wanayo? Halafu kuna tena hili linasemwa semwa sana hii habari ya askari kutoka Rwanda kumlinda rais na ukuta wa mererani kulindwa na wanyarwanda tiss wameridhia? Na hili la nchi kuiingiza Bahima empire nalo tiss wameridhia, mpango wa watusi kutawala nchi za maziwa makuu na lenyewe wameridhia? Hivi tuna usalama wa taifa kweli?
 
nahisi mtandao wenye member wengi wa TISS ni JF,,,,,,,,,,,

Na kwa bahati mbaya ' Members ' ambao hatujapata bahati ya kuwa huko kutokana na kwamba hatuna Sifa ' toshelezi ' ni Wewe na Mimi tu Ndugu. Hivi tulikosea wapi Ndugu mpaka na Sisi siyo sehemu hiyo ya TISS kama walivyo ' Members ' wengine hapa Jamvini?
 
Hizi post za kijinga na mihemko zimezidi humu kila Sikh TISS ,TISS tu tafuta kazi ufanye hata kuchoma mihogo tu

Maajabu sasa Watoa nyuzi mahoka kuhusu TISS wote wako majuu hamna aliyepo bongo
 
TISS THIS TISS THAT

Principle ya usiri ambayo imezingatiwa vilivyo awamu hii ngumu ya social networks ndo inawafanya wewe na watu wa jamii yako kina kigogo na Spy mstaafu muibuke na mafumbo ya kijinga na utunzi usio na uhalisia

unadai hao unaowaita TISS hawaajili wapinzani si sishangai sana Vijana wengi wanaotafuta popularity humu jf huandika wasiyoyajua.Ushajiuliza informants wa chadema wanatoka wapi???

USIRI unazingatiwa nyie endeleeni na porojo mufilisi
 
Wee jamaaa acha utani kwenye mambo ya msingi...
Jf ni kokoro lililojaa takataka Kwa asilimia 70.
Ni forum uliyojaa watu wasio na uwiano au kuwa kiwango fulani cha taaluma au fani.
Tunaunganishwa na kitu kimoja Tu .....
UWEZO WA KUINGIA MTANDAONI. Mostly Kwa kumiliki smartphone tena wengine za kupewa, kurithi au kuiba... achilia mbali wale wengine wanaingia na vibatani vya 30000.
Ukiwa muelewa huwezi kutegemea kupata elimu humu. Unless uwe na ufahamu mpana WA kuanalyse mambo na sio kujifunza.
luna variations of umderstandimg humu!
kwa hiyo ni kisima cha kuchota maarifa!
 
Hizi post za kijinga na mihemko zimezidi humu kila Sikh TISS ,TISS tu tafuta kazi ufanye hata kuchoma mihogo tu
Duh! Mkuu uwezo wako wa kufikiri umeisha hapo, uwezo wako wa kujibu hoja umeishi kwenye mitari miwili..!!?

Kama wewe ni moja wa hao TISS basi kwa kweli Taifa la Tanzania lina safari refu..

Kama mleta mada anavyosisitiza kuwa bila Taifa kuwa na Idara ya Usalama wa Taifa wa uhakika basi nchi huwa dhaifu, Kiuchumi, Kiulinzi nk..

Mungu ibariki Tz
 
TISS haiwezi kufanyiwa mabadiliko kwasababu nguvu kubwa wamewekeza kuilinda CCM , Watanzania maendeleo tutayasikia kwa wenzetu.
 
TISS wametoa wapi hayo mamlaka makubwa namna hiyo jamani.
Katiba yetu inasemaje juu ya hao TISS.

Au tupeni mfano wa hiyo post no.87.
eti TISS isipotaka kiwanda kijengwe hakijengwi, seriously?

Mambo mangapi ya hovyo kabisa yanafanyika kila awamu kuanzia awamu ya kwanza mpaka ya sasa ambayo yalipaswa kushughurikiwa na aina ya kikaragosi mnachokizungumzia hapa na hayakutendewa haki?

Anza na vita vya Kagera, TISS ilikuwa wapi japo kuwatonya masoja kwamba Amin anafikiria upuuzi alioishia kuutenda?
Mauaji ya kimbali ya Rwanda na dhahama yaliyotuletea watanzania, kuanzia mafuriko ya wakimbizi na sasa jamii ya kinyarwanda iliyotapakaa kila kona ya nchi, TISS hawakuyaona haya?
Uwekezaji sekta ya madini na sasa gas? Tiss walikuwa wapi?
TISS walishindwa nini kumcontroll nyerere na Kawawa na mambo yao ya vijijii vya ujamaa?
Mpaka leo hatujaambiwa Mwalimu alikufa kufaje huko jerumani? TISS wako wapi?
walimu wa vodafasta wa lowassa, TISS hawakuwaona?
wakati MUNGAI anafuta elimu ya michezo mashule hili halikuwa tishio la usala kwa Taifa? au mimi ndio mjinga?
TISS ndio walimuelekeza JECHA kufanya yake? kwa nini hawakuona kilichokuwa kinakuja na kukiachia mpaka kututia aibu namna hii?
Yuko wapi Balali?
Muungano wa Africa mashariki wakati unavunjika, hawakuhitajika TISS kulinda maslahi ya Taifa?
UKIMWI,Maradhi ya Sukari, Maradhi ya Cancer, Maralia na sasa Tabia za kishoga, TISS hawaoni kama ni tishio kwa Usalama wa Taifa?

Siwaelewi.
Hawa ni ghost security personell, security kwa maana ya kupambana na vibaka na mambo yasiyo maalumu.
sina namna bora zaidi ya kuwaelezea.
'Mpaka leo hatujaambiwa Mwalimu alikufa kufaje huko jerumani?'

Mwl Nyerere alifia Ujerumani?
 
Back
Top Bottom