Part 1: TISS bado safari ngumu

Part 1: TISS bado safari ngumu

Kuna watu wanadhani kuondoka kwa mzee wangu wa Kanisa,TISS ndugu Kipilimba basi mambo yanaenda kubadilika na kuifanya idara hiyo ifanye kazi nzuri la hasha.

TISS bado ina safari ndefu mno ili iwe idara bora Kama zingine, recruitment ya TISS imejaa viroja na maajabu, tofauti na mashirika mengi ya kijasusi Duniani.

TISS imejaa kina "kamlete ",yaani watu wanaopewa ajira na ndugu zao kwa sababu ya ugumu wa maisha ya Bongo, hakuna usahili wa uhakika, madhara yake kumejaa ma agent ambao wakiona post Kama hii wanatamani wamkamate mtoa mada na kumpoteza.
Haina watu wazalendo kwa Taifa lao bali wazalendo wa chama tawala cha CCM chenye ndoto za kutawala Tanzania milele.

TISS haiwezi kumwajiri mwanachama wa CHADEMA au mpinzani yoyote bali Lazima awe mfia CCM na siyo mfia Tanzania.

Kazi kubwa za idara za kijasusi ni kuhakikisha nchi iko salama wakati wote na kuhakikisha hakuna umaskini ktk nchi kwa gharama yoyote ile.

Hongera zenu CIA, MI6, MOSSAD nyie ndo mnaipeleka Dunia puta kwa maslahi ya mataifa yenu, hamna muda na siasa.

Kazi ya idara ya usalama wa taifa ni kuwa loyal kwa nchi na si kwa wanasiasa...

INAENDELEA
Haha haha wakiona post kama hizi wanatamani wakukate mikono au wakutoboe macho ili usitype tena sababu unawachomea ni kweli wengi usaili wasasa taasisi nyingi si wa kiprofosheno zaidi ni kujuanajuana tu ili wapate mshahara kazi hawaziwezi
 
Mambo yamebadilika sana yaani watu tunajadili masuala ya TISS rahisi rahisi tu 😁.
Miaka ile ya akina mzee Apson unaweza kukaa hata mwaka mzima na usikutane na habari ya TISS.
Walau miaka ya mzee wangu mzanzibar Othuman na msaidizi Balozi Jack Zoka tulikuwa tunasikia habari za idara walau Mara mbili kwa mwaka lakini miaka hii kila siku tunajadili TISS.
Sisemi kuwa ni jambo baya lakini kwa asili ya idara yenyewe na mambo yanayojadiliwa nadhani aidha idara imekuwa wazi sana au wasiotakiwa kujua masuala ya TISS basi wamejua habari nyingi kupitiliza.
Ufanisi wa idara hizi popote duniani umejengwa kwenye "usiri wa kutotabirika" kwenye mipango yake na mfumo wake wa kiutendaji.
 
Kuna watu wanadhani kuondoka kwa mzee wangu wa Kanisa,TISS ndugu Kipilimba basi mambo yanaenda kubadilika na kuifanya idara hiyo ifanye kazi nzuri la hasha.

TISS bado ina safari ndefu mno ili iwe idara bora Kama zingine, recruitment ya TISS imejaa viroja na maajabu, tofauti na mashirika mengi ya kijasusi Duniani.

TISS imejaa kina "kamlete ",yaani watu wanaopewa ajira na ndugu zao kwa sababu ya ugumu wa maisha ya Bongo, hakuna usahili wa uhakika, madhara yake kumejaa ma agent ambao wakiona post Kama hii wanatamani wamkamate mtoa mada na kumpoteza.
Haina watu wazalendo kwa Taifa lao bali wazalendo wa chama tawala cha CCM chenye ndoto za kutawala Tanzania milele.

TISS haiwezi kumwajiri mwanachama wa CHADEMA au mpinzani yoyote bali Lazima awe mfia CCM na siyo mfia Tanzania.

Kazi kubwa za idara za kijasusi ni kuhakikisha nchi iko salama wakati wote na kuhakikisha hakuna umaskini ktk nchi kwa gharama yoyote ile.

Hongera zenu CIA, MI6, MOSSAD nyie ndo mnaipeleka Dunia puta kwa maslahi ya mataifa yenu, hamna muda na siasa.

Kazi ya idara ya usalama wa taifa ni kuwa loyal kwa nchi na si kwa wanasiasa...

INAENDELEA
Nikweli tusitegemea makubwa sana maana mfumo wa TISS yetu inautii sana kwa Rais aliyepo madarakani na siutii kwa maslahi ya Taifa.

Kwa mfumo uliopo, TISS yetu haina uwezo wa kusimama kidete au kufanya maamuzi magumu dhidi ya Rais anaeenda kinyume na maslahi ya Taifa kama mashirika mengine kama CIA, KGB, n.k.
 
Mambo yamebadilika sana yaani watu tunajadili masuala ya TISS rahisi rahisi tu .
Miaka ile ya akina mzee Apson unaweza kukaa hata mwaka mzima na usikutane na habari ya TISS.
Walau miaka ya mzee wangu mzanzibar Othuman na msaidizi Balozi Jack Zoka tulikuwa tunasikia habari za idara walau Mara mbili kwa mwaka lakini miaka hii kila siku tunajadili TISS.
Sisemi kuwa ni jambo baya lakini kwa asili ya idara yenyewe na mambo yanayojadiliwa nadhani aidha idara imekuwa wazi sana au wasiotakiwa kujua masuala ya TISS basi wamejua habari nyingi kupitiliza.
Ufanisi wa idara hizi popote duniani umejengwa kwenye "usiri wa kutotabirika" kwenye mipango yake na mfumo wake wa kiutendaji.
Miaka ya akina apson mitandao ya kijamii ilikua imesambaa kama hivi?

Hizi story za Tiss huoni zinapigwa tu huku mitandaoni tena na watu wenye fake id's?

Au huko mtaani kwenu ulishawahi kuona watu wamekaa kwny makundi wakiongea story za Tiss kama hivi.
 
TISS haiwezi kumwajiri mwanachama wa CHADEMA au mpinzani yoyote
Hapa ndipo unaonyesha wazi kuwa umeparamia mambo ya TISS wakati kichwa chako cheupeee .Umejaa ujuaji hewa.TISS wasipoajiri wanachama wa vyama vya upinzani nani atawaletee taarifa za kiinteligencia za ndani ya Chadema na hivyo vyama vingine vya Upinzani? Naona unaandika story za vijiweni.Kichwani uko mweupeeee.Wewe kijiweni ndie wanakuona expert wa mambo ya TISS vijiweni 😀😀😀 !!!!!!!
 
Idara nyeti inapaswa kuwa na watu ambao brains zao zinacharge kweli kweli
Watu wenye upeo mkubwa kiakili na kinidhamu.

Idara inapaswa iwe na cream of the cream ya nchi

Siyo unachukua watu kwa milengo ya kisiasa matokeo yake hata analysis simple tu za mambo yanayojiri nchini hawawezi na hawana inputs zozote za maana!

Siyo lazima wachukue wenye madigrii tu bali wachukue watu bright kisha wawaendeleze, maana kuna watu hawakwenda shule za madarasani lakini wana akili kishenzi!

Kiukweli mambo yaliyokuwa yakifanyika nchini ndani ya miaka minne iliyopita utadhani yanapangwa na kufanywa na amateurs, kuanzia scripts za matukio feki ambazo raia siku hizi wanacheka tu!

Wewe imagine mtu anapiga picha kijijini kakaa na Jiwe anajifanya eti na yeye ni mmoja wa wazee masikini wa huko Chato kumbe ni.mmoja wa waambata wa Jiwe kwenye matukio mengine na picha zake zipo!

Eti mwanamama yuko hospitali anajifanya kumuomba raisi hela ya kukomboa maiti, halafu eti yuko peke yake na hakuwa cleared njiani anapopita rais, umewahi kuona wapi hii zaidi ya script?

Eti mtu anaenda bandarini na kisha kuokota vichwa vya treni

Vijana kufuatiliwa facebook kwa comment za maoni yao tu ya kisiasa na kupewa msoto mkali!

Unaenda kuandaa script ya maandamano kwenye ubalozi wa nchi nyingine kinyume cha protokali za Kidiplomasia duniani eti kushinikiza nchi iingilie mchakato wa madai yaliyoko mahakamani

Mambo gani haya ya ajabu kabisa!

TUNATAKA IDARA SMART, SHARP, JUST na YENYE KULINDA USALAMA WA NCHI KWANZA SIYO POLITICAL ambitions za MTU
Nataman Sana hiki ulichokiandika angekisoma mkuu Wa kaya, labda angepata wazo mbadala
 
Nikweli tusitegemea makubwa sana maana mfumo wa TISS yetu inautii sana kwa Rais aliyepo madarakani na siutii kwa maslahi ya Taifa.

Kwa mfumo uliopo, TISS yetu haina uwezo wa kusimama kidete au kufanya maamuzi magumu dhidi ya Rais anaeenda kinyume na maslahi ya Taifa kama mashirika mengine kama CIA, KGB, n.k.
MKUU iv unamjua vizuri puti? unafikiri hao KGB wana sauti juu ya putin?
 
Tatizo lipo kwenye Muundo wa Nchi ya Tanzania ni hovyo. Chama tawala hakijatenganishwa na Serikali, Jambo la kwanza ilitakiwa ni Kuubadili Muundo kwa Kubadili Katiba ili Kuwepo na Separation ya Kueleweka kati ya Vyombo vya Dola na Chama tawala kama Mataifa mengine.

Sasa hivi Serikali ya Tanzania huwezi tofautisha na JWTZ,Polisi, Uhamiaji na Vyombo vingine vyote. Yaani Ukikosoa CCM unakuwa Umekosoa Vyombo vya Dola vyote vya Nchi hivyo Lazima Wakushughulikie.

Hivyo basi Vyombo vya dola vinaendeshwa na Chama ili kulinda Vibarua vyao.
 
TISS imejaa kina "kamlete ",yaani watu wanaopewa ajira na ndugu zao kwa sababu ya ugumu wa maisha ya Bongo, hakuna usahili wa uhakika, madhara yake kumejaa ma agent ambao wakiona post Kama hii wanatamani wamkamate mtoa mada na kumpoteza.
Haina watu wazalendo kwa Taifa lao bali wazalendo wa chama tawala cha CCM chenye ndoto za kutawala Tanzania milele.
Ndugu hizi ni tuhuma nzito sana umeandika hapa.

Mfano ukiombwa kutoa ushahidi wa haya utaeza kufanya hivyo?
 
Kulijua Hilo kwamba TISS wengi ni vilaza ni pale walipocheza movie ya kishamba ya utekaji wa MO DEWJI
 
Nauliza tu hakuna mpinzani aliyeko kwenye makaratasi ya malipo ya TISS? Maana hapo juu umesema haiwezi kuajiri wapinzani

Fuatilia sherehe za Ikulu mara nyingi utaona mapicha ya hao watu wa upinzani wanaoulizwa
 
Nimesomaaaaa nikaelewa jambo moja kuu ndio kiini na mjadala wote unaelekea huko
UPINZANI NAO WAKAMATE NCHI
Ni jambo zuri lkn wamejipanga?
1. Chadema wakavurugana Slaa huyoo, Zito naye huyoo akaanzisha chama chake, Cuf wakagawana pasu, na mwingine akakwapuliwa , hili la MISUGUANO halijaisha

2. Likaanza wimbi la kuunga mkono wakaliita ununuzi wa wanasiasa, sisi tulio penbeni tukatambua kumbe WANANUNULIKA hawa uwape nchi.

3. Upinzani wa Always NEGATIVE hata adui wa nchi akitushambulia wanapiga makofi, si Barrick na wenzao wao hata tumekosea mikataba sawa lkn kwanini mna side kwao? Kesi ya mkulima, kila atakayeonyesha kuishughulikia hii nchi msaada atapata kwao,

Tuna bahati 1978 hawakuwepo adui angekunywa supu ya pweza kwa mtogole maana wangeambiwa askari walio front ni mgambo trained kwa wiki wameletwa ni civilian in uniform , wangeambiwa tu tuna ndege 2 zingine mbovu eti kuikomesha serkali kumbe ni kukata shina ukiwa juu ya tawi.

Mimi sio Mzalendo. Ni mpinzani kindakindaki. A.k.a mchomoa betri.
Napenda tuharibikiwe nifurahii
 
Mtoa mada umenifurahisha uliposema tiss imejaa wakina "kamlete"
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Back
Top Bottom