'PARK AT YOUR OWN RISK' ni wizi mtupu

Lukansola

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
5,435
1,597
Wakubwa shikamoo wadogo marahaba,
Bila shaka wengi wetu kama sio wote tumeona hivi vibao vyenye maandishi ya 'Park at your own risk' kwemnye, maeneo mbalimbali kama mabenki, mahoteli, nk. sehemu hizi pamoja na kuwa na tahadhali hii huwa pia kuna walinzi, kwa maoni yangu huu ni ******, kwani wale walinzi sasa kazi yao ni nini. naombeni maoni yenu kuhusu hili. Mada inaeleweka nisichukue muda wenu kwa maneno mengi
Karibuni sana.
 
Wanakimbia gharama iwapo kutatokea uharibu au wizi.

wajinga ndo waliwao
mfano pale mlimani city ukimisplace kikadi chao ama kama hukukichukua kwa bahati mbaya au kwa kutokujua bas tabu tupu wanataka ulipe fine ya 10,000 sasa kama hawalindi gari yangu au vilivyomo kwa nini wadai,kama ni wezi si wanaweza kutengeneza kadi kama zao maana hazina security mark yoyote na kutumia?
maana ukiingia hakuna matching ya namba ya gari yako na serial number ya kadi sasa vya nini?
 
nyie wa huko ughaibuni hebu tuambieni mambo haya yako huko?
 
Hiyo clause haina nguvu kisheria kabisa.kama gari ikpata tatizo la kuibiwa,au kupata madhara yoyote na kama occupier wa eneo husika amaechangia tatizo hilo basi wewe hapo unafungua kesi na atakuwa liable accordingly,exemption cluase kama hizo ni urembo tu.soma law of torts by catherine itakusaidia pia.soma occupiers liability pia soma law of contract katika exemption cluase itakusaidia pia.ni maoni yangu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom