Papa Francis alikataa Rais wa Philipines kubusu pete yake, achilia mbali unaowaona hawa anaowakatalia wiki hii

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Wiki hii imesambaa picha ya Papa Francis akikwepa kubusiwa pete yake, utaratibu unaofanywa kwa askofu yeyote, achilia mbali Papa.

Kitendo hicho kimejadiliwa na kila aina ya mitandao, kwenye magroup, facebook, twitter na kokote unakoweza kutaja.

Sasa mimi maoni yangu ni nini? Maoni yangu ni kwamba mitandao imejaa wavivu wa kuangalia mambo imejaa wakurupukaji.

Binafsi nimemuona Papa Francis akifanya hivyo kwenye ziara aliyofanya Philipines na alipotelemka kwenye ndege akapokelewa na Rais wa nchi hiyo.

Papa Francis alichofanya ni hikihiki cha kukataa kubusu pete yake.

Rais wa Philipines alimpokea na akampa mkono lakini alipopeleka mdomo kuibusu Papa Francis kwa staili ileile akakwepesha mkono na hivyo Rais huyo akashindwa kuibusu.

Unaweza kuona kitendo hicho kwenye youtube kwenye ziara yake huko Philipines.

Kwenye video inayosambaa hakuna Rais wa nchi ambaye anakwepwa ni wananchi wa kawaida huko Italy kwenye mji unaoitwa Loreto.

Kimsingi ni kwamba Papa wa mwisho kupenda tabia ya kubusiwa pete yake ni Papa Benedict XVI.

Ukiangalia anapompokea Rais Kikwete pale Vatican utaona Jakaya Kikwete alivyojipinda kuibusu pete ya Benedict XVI.

Huyu Papa Francis hapendi sana kitendo hicho ingawa mara moja moja sana hukiruhusu. Staili yake ya kukiataa ni very classic huku akikuchekea na hata mnaoangalia mnaweza msitambue kwamba amekataa.

Kilichotokea juzi ni kwa sababu walimsalimia walikuwa ni kwengi na hivyo kitendo cha kukataa kubusu kikaonekana kwa wingi na aliyesambaza video akaona kama vile amegundua tabia mpya ya Papa Francis.

Ingawa amefanikiwa lengo lake kafanikiwa kwa sababu mitandao imejaa wakurupukaji. Hiyo ndiyo kawaida yake ingawa hajawahi kufafanua ni kwa nini hapendi hivyo.

Iko siku atakutana na Rais wa Tanzania halafu wakurupukaji watatusmbu awiki nzima mitandaoni kwamba kakataa kubusu pete ya Rais wa Tanzania. Tena wanaweza kuunganisha kwamba ni kwa sababu Rais wa Tanzania kagombana na maaskofu kuhusu waraka wa kanisa:D.

Nimetoa mfano wa Rais wa Philipines alivyokataliwa busu lile, hivyo ikitokea hivyo mitandao isikurupuke kama inavyokurupuka juzi.

Wenu Mwana JF
 
Back
Top Bottom