Papa Francis Adai "Hakuna Paradiso /Mbinguni

Mbingu ni Hali,na siyo mahali

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
Achen masihala Wakuuu, Kwan maandiko yanasema je ?.

Maandiko yanasema, Mara baada ya ujio wapili wa Yesu

Waovu wakishatupwa ziwa la moto.


Mungu, atashuka na Mji wake Yerusalemi ya mbinguni, atashuka nao na kuuleta hapa Duniani.

Na kufanya makazi hapahapa pamoja na wale wateule, watakatifu ambapo wameishinda dhambi.


Hivo Mbinguni ni Mahali halisi kabisa 100%. Sio hali kwamba inafikirika.
 
Sasa kama Mungu hayupo hiyo pepo itatoka wapi?

Pope anawaandaa kisaikolojia mapema ili siku akija na hiyo conclusion msishtuke lazima awaanzie mbali ili angalau muweze bashiri majibu
 
Mbingu IPO spiritually siyo physically
 
Yuko sahihi. Duniani tu ndio mahususi kwa ajili ya kuishi watu na mazingira yanayoendana na viumbe hai.
Ni kweli, ila najiuliza kama ni hivyo hizi sayari zingine 7 tena zingine kubwa kabisa mara nyingi kuliko dunia ni za nini? Kwanini zimekuwepo ilihali hakuna viumbe vingine huko?
 
Uchumi wa Kat tutafika mkuu?

Umemezeshwa Kama yalivyo

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Source please ya ulicho kiandika
 
Huyo yohana ume mjua baada ya kusoma biblia swali linakuja unajuaje biblia kama ni kitabu cha kweli vipi kama nikitabu cha kutunga ili kuweza tu ku shape dunia yan watu wenye Akili walikaa nakuona namna ya kuwaweka watu sawa remember fear is what keep people moving on
 
Hakuna Muabudu siku ya Jumamosi(Msa7too) mwenye akili
ata ukijadiliana nao ni kama digidigi ni 0
 
Hata huyo MUNGU ni Hali,Kama ilivyo pumzi/roho yako iliyopewa 'mahali' pa kuishi(mwili) kisha ukawa physical being

Siku ukifa unarudi kwenye 'hali' yako ya asili ya vile ulivyokuwa zamani kabla hujapelekwa mahali pa kukaa (mwili)

☝️☝️☝️
Ukifanya astral projection ukatoka nje ya mwili /gereza ndy siku utakuja kugundua wewe ni sehemu ya MUNGU (Kama yeye alivyosema na tumfanye mtu Kwa mfano wetu)

Nikuulize swali; watu wa babeli walipojenga mnara ili kumfikia MUNGU hata MUNGU akaona hawa watu wapo serious akaamua kuangusha mnara na kisha akawafanya wasielewane tena Kwa kuongea lugha tofauti tofauti,unadhani huo mnara ulikuwa mrefu kiasi gani Hadi MUNGU kupata hofu juu ya hao jamaa

Au kule kwenye mawingu yanakopita ndege ndy mbinguni ambako watu wa babeli walihenga mnara ili kumfikia MUNGU?

Kukujibu swali lako la 'jerusalemu mpya' biblia inasema hata hao watakaopewa kibali cha kuishi kwenye huo mji watapewa 'mwili mpya'..siyo mwili huu wa duniani ambao roho unaishi ndani yake..tafakari!!
 
Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote, muumba vyote, katungwa na watu tu.

Hayupo katika uhalisia.
 
Mbingu IPO spiritually siyo physically
"Spiritually" maana yake nini?

Au hizi ndizo zile habari za "mwenda poke hajikwai, akijikwaa haanguki, akianguka haumii, akiumia huumia kidogo tu"..

Mwisho unakuta mwendapole kaumia sana, kapigwa daflao na gari kajifia mbali huko, hata bila ya kujikwaa.
 
Basi hao watu walioandika biblia na misahafu ili kuishape dunia kwa kutunga tu zile habari za injili walikua na akili sana coz wemiteka robo tatu ya ulimwengu.
 
Yupo sahihi. Hakuna Jehanamu. Na kama hautendi dhambi kwa kuogopa moto jichunguze ukristo wako. Na pia hakuna hiyo paradiso ya mbinguni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…