Panya wananisumbua

Panya wananisumbua

KASRI

Member
Joined
May 2, 2009
Posts
93
Reaction score
22
Wasalaam,
Nimekuwa kwenye vita na panya nyumbani kwangu kwa miezi sasa. Panya hawa wapo wengi kiasi kwamba wakati mwingine unaweza kugongana naye ukiwa unapita kwenye "corridor" nyumbani hasa mida ya usiku.

Ninaomba ushauri jinsi gani ya kuwatokomeza.

NOTE:
.Ninaishi kwenye "appartment" ghorofa ya kwanza - jijini Dar es Salaam
.Jirani zangu hata aliyepo chini yangu (ground floor) hana hiyo kero.
.Nina mtoto mdogo anayetambaa na mwingine wa miaka 3.
.Nimetumia mitego tofautitofauti lakini sijafanikiwa
.Niliwahi kutumia sumu ya kuwakausha wakila - nikaishia kuifagia tu asubuhi maana hawaili.

NAtanguliza shukurani





Tumekuwa tukijitahidi kwa usafi lakini bado wanaendelea kuingia nyumbani usiku. Wanapitia sehemu tofauti tofauti zikiwemo, mlangoni (ukibaki wazi kwa bahati mbaya), madirishani (pakiwa wazi kidogo tu),
 
Wasalaam,Nimekuwa kwenye vita na panya nyumbani kwangu kwa miezi sasa. Panya hawa wapo wengi kiasi kwamba wakati mwingine unaweza kugongana naye ukiwa unapita kwenye "corridor" nyumbani hasa mida ya usiku.Ninaomba ushauri jinsi gani ya kuwatokomeza.NOTE:.Ninaishi kwenye "appartment" ghorofa ya kwanza - jijini Dar es Salaam.Jirani zangu hata aliyepo chini yangu (ground floor) hana hiyo kero..Nina mtoto mdogo anayetambaa na mwingine wa miaka 3..Nimetumia mitego tofautitofauti lakini sijafanikiwa.Niliwahi kutumia sumu ya kuwakausha wakila - nikaishia kuifagia tu asubuhi maana hawaili.NAtanguliza shukuraniTumekuwa tukijitahidi kwa usafi lakini bado wanaendelea kuingia nyumbani usiku. Wanapitia sehemu tofauti tofauti zikiwemo, mlangoni (ukibaki wazi kwa bahati mbaya), madirishani (pakiwa wazi kidogo tu),
Fuga paka aka (nyau)
 
mtafute mphilipino aishi hapo kwako kwa muda wa mwezi tu,hiyo kero kwishney
 
Paka pekee ndiye anaweza wasambaratisha jaribu kufuga paka kwa muda wataondoka wote kama si kuliwa ukiweka sumu unaweza wauwa lakini watakuja wengine hasa endapo kuna vyakula wanavipata kirahisi.Lakini kwa kutumia paka hata kama hawatafuni wakisikia kelele za nyauu!! nyauuu!! wataisha wote
 
Hakikisha hawapati chakula chochote hapo ndani na pia ushirikiane na majirani pia wasiache masalia ya chakula watakimbia njaa. Pia paka anaweza kukusaidia sana.
 
Njia ni rahisi sana nilishawahi kumfundisha mwanajf alifanikiwa karanga zilizokaangwa zisage ziwe laini changanya na cement kidogo pembeni wawekee maji kazi imeisha hawatapata choo utakuwa umetengenezea tofali tumboni mwao hadi kifo chao
 
Ha ha ha ha ha hii kali inaweza kuwashulihisho zuri kwa mtu asiyependa kufuga paka.

Njia ni rahisi sana nilishawahi kumfundisha mwanajf alifanikiwa karanga zilizokaangwa zisage ziwe laini changanya na cement kidogo pembeni wawekee maji kazi imeisha hawatapata choo utakuwa umetengenezea tofali tumboni mwao hadi kifo chao
 
Paka ndo suluhisho,
na kama hupendi kufuga paka kwa huku mikoani kuna kidonge fulani kinapatikana kwenye maduka ya madawa ya kilimo kina harufu mbaya sana, cha kufanya unakiweka sehemu wanapopita panya akinusa tu kwaheri harafu cha ajabu panya wenyewe wanaipenda sana harufu ya hiki kidonge !!
 
tafuta kibao kisha waandikie tangazo wahame maana unampango wa kufuga paka...wakisoma wenyewe watakula kona!!!nyau si mchezo...
 
dah komenti zingine bana! Balaa tupu

mkuu ushauri wa kufuga paka naona ni suluhisho ila tu najua kuna watu hawapendo kabisa kumuona, kumsikia licha ya kumfuga mnyama aitwaye paka
 
Panya!! maraisi wa ghetto mi mwenyewe wamenishinda wanakula sofa zangu daily vitabu nguo mpaka fedha sometimes,ki ukweli panya hawana shukrani hata uwape msosi kila siku.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom