Panya wananisumbua

Panya wananisumbua

Wasalaam,
Nimekuwa kwenye vita na panya nyumbani kwangu kwa miezi sasa. Panya hawa wapo wengi kiasi kwamba wakati mwingine unaweza kugongana naye ukiwa unapita kwenye "corridor" nyumbani hasa mida ya usiku.

Ninaomba ushauri jinsi gani ya kuwatokomeza.

NOTE:
.Ninaishi kwenye "appartment" ghorofa ya kwanza - jijini Dar es Salaam
.Jirani zangu hata aliyepo chini yangu (ground floor) hana hiyo kero.
.Nina mtoto mdogo anayetambaa na mwingine wa miaka 3.
.Nimetumia mitego tofautitofauti lakini sijafanikiwa
.Niliwahi kutumia sumu ya kuwakausha wakila - nikaishia kuifagia tu asubuhi maana hawaili.

NAtanguliza shukurani





Tumekuwa tukijitahidi kwa usafi lakini bado wanaendelea kuingia nyumbani usiku. Wanapitia sehemu tofauti tofauti zikiwemo, mlangoni (ukibaki wazi kwa bahati mbaya), madirishani (pakiwa wazi kidogo tu),


Hizo ni Dalili za UTAJIRI waache tu ila Ongeza Bajeti ya Msosi
 
Njia ni rahisi sana nilishawahi kumfundisha mwanajf alifanikiwa karanga zilizokaangwa zisage ziwe laini changanya na cement kidogo pembeni wawekee maji kazi imeisha hawatapata choo utakuwa umetengenezea tofali tumboni mwao hadi kifo chao

mh! Hii yako kali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom