Panya wa SUA Wapata Majukumu Bandarini

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), imesema miongoni mwa njia wanazozitumia kudhibiti ujangili na utoroshwaji wa bidhaa zinazotokana na wanyamapori ni kukagua mizigo bandarini kwa kutumia panya wenye mafunzo maalumu kutoka Chuo cha Kilimo Sokoine (SUA).

Kauli hiyo imetolewa na Ofisa Wanyamapori daraja la kwanza wa Tawa, Tryphon Kanon, alipokuwa akitoa mada kwenye semina ya wahariri iliyoandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari wa Mazingira Tanzania (JET), kupitia wa mradi wa Tuhifadhi Maliasil unaofadhiliwa na Shirika la Misaada la Marekani (USAID).

Kanon alisema kukabiliana na ujangili na usafirishaji wa pembe za ndovu na bidhaa nyingine zinazotokana na wanyamapori kunahitaji teknolojia ya kisasa, ndiyo maana kila kukicha wanabuni mbinu mbalimbali za ukaguzi na udhibiti.

"Tunatumia panya waliopewa mafunzo maalumu kukagua mizigo katika bandari zetu, hili tunalifanya kwa kushirikiana na wenzetu wa SUA," alisema.

Kanoni alisema kutokana na udhibiti unaofanywa na Serikali, wahalifu wamebuni mbinu ya kusaga meno hayo na kusafirisha unga, huku wengine wakitengeneza vito vya aina mbalimbali na kuvisafirisha kwenda nje ya nchi.

Hata hivyo, alisema hatua za kudhibiti wjangili zilizochukuliwa na Serikali kuanzia mwaka 2013 hadi 2022 zimesaidia kupunguza idadi ya tembo wanaouawa kila mwaka kutoka 50 hadi 0.

Alisema mwaka 2016 kulikuwa na kesi za ujangili 3,289 lakini mwaka 2023 zimeshuka hadi 1,213 na kati ya hizo 577 zimeshamalizika.​
 
Kama Ukaguzi wa bandari Panya wa Tanzania wanaweza,kwanini Usimamizi wa bandari mnashindwa nyie Watanzania mpaka muwauzie waarabu?
 
Back
Top Bottom