Panya Road wavamia Chamazi

Panya Road wavamia Chamazi

Eti watu wanahimizana kufunga milango,kweli?,hebu jikusanyeni hapo muwafate na kuwafagia pumbavu zao acheni uoga,huku kwetu tumeanza kulinda usiku wakijichanganya tu mbona watawazika!..
 
mkuu, lakini nadhani pia tangu polisi walipoacha kukaa vituoni usiku kundi hili limepata kasi ya kuendelea kuwatesa raia na kuwanyima raha kabisa. serikali inapaswa kufikiria upya uamuzi wake wa kufunga vituo ili polisi wachache waliopo washirikiane na wananchi kutokomeza kundi hili la kigaidi.
Anzisheni Doria za mitaa
 
Chomeni moto hao mbwa,mnawaonea huruma ili iweje?
tatizo wananchi hawana ushirikiano. hata scorpion alifanikiwa kumtoboa mtu macho kwa sababu ya utovu wa ushirikiano miongoni mwa wananchi.
 
Kwan hao pana road hawana wazaz c wanao wakulaumiwa wazaz wao na humhum jf kuna wazaz wanaojua kuwa kijana wake ni panya road c kwamba tuiachie selikar tu tuwakanye watoto wetu
 
Kama taarifa hizi ni za kweli basi naamini vijana Wa kamanda Sirro wako njiani
 
Nadhani pale Chamazi kuna kituo cha polisi. Vipi huna namba zao uwapigie wachukue hatua za haraka? Hilo eneo la Muhimbili hakika ni hatarishi sana. Lipo wazi kwa vile halijajengwa ijapokuwa limezungukwa na makazi ya watu. Nakumbuka pia jirani na hilo eneo kuna Bar nadhani inaitwa Last Card. Mliopo Chamazi mtanisahihisha
Mkuu, ni kweli kabisa wala hujakosea. Hata mimi kuna siku nilipita pale nikaona ule uwazi na giza nene linalotanda pale wakati wa usiku huwachochea panya road kufanya uhalifu wao.
 
Ni kweli. Hili kundi hata sijui limeibukaje wakati Dar ilikuwa imenza kuwa tulivu. Serikali inapaswa kuwapa wananchi mafunzo ya kijeshi na kuwamilikisha silaha kwa ajili ya kujilinda na makundi ya kipuuzi kama hili la Panya Road.
Mafunzo ya nn,itapelekea kuongezeka kwa matukio ya uhalifu.
 
Kwani wanaandamana au wanaiba tuu na kuondoka?
wanaiba, wanachana watu visu, mapanga na viwembe na kisha kuhamia eneo lingine....ni kama kunguru wanavyoshambulia vifaranga.
 
Miaka ya nyuma palikuwepo Na kundi lilifahamika kwa jina la commando yosso,hivi liliishia wapi au ndio hili la panya road ?
 
Nilikuwa sijui, kumbe hata wewe ni mwanaume wa Dar mkuu!!!
mkuu hizi habari nimezipata kutoka Dar, mimi sio mwanaume wa huko...huku kwetu mbwa koko kama hao panya road hawawezi kutia mguu.
 
Mkuu acha masihara uwape wananchi mafunzo ya kijeshi na silaha za kujilindia ili wao wenyewe wageuke waharifu
ili wajilinde. sasa wewe unaona afadhali wabaki hivyo hivyo waendelee kuuwawa na kutobolewa macho na panya road?
 
Back
Top Bottom