Pamoja na ujio wa Symbion, mgao kama kawa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pamoja na ujio wa Symbion, mgao kama kawa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bushbaby, Jun 20, 2011.

 1. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Wana Jf kwa mimi hapa nilipo sijaona changes yoyote iliyoletwa na uwepo wa Symbion Power, umeme ndo umekuwa balaa zaidi... hatukuwahi kukatiwa umeme j'pili ila hii ni mara ya pili wanauchukua asb unarudi usiku... ninavyojua mimi hawa Symbion walishaanza kazi sasa mbona hali haibadiliki na tunawalipa hela nyingi za walipa kodi??? na kuna tetesi ile mitambo ya Tanesco ya Ubungo imezimwa kupisha Symbion, wakuu hii ikoje???
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,448
  Likes Received: 81,648
  Trophy Points: 280
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #FFFFFF"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]yatangaza mgawo mkali
  • Mikoa 18 kuingia gizani, mafuta leo

  na Betty Kangonga
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [/TD]
  [TD="width: 140, bgcolor: #FFFFFF"][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]SHIRIKA la Umeme nchini (TANESCO) limetangaza mgawo mkubwa wa umeme kwa mikoa 18 ambayo inapata umeme kupitia gridi ya taifa.

  Akizungumza katika Televisheni ya Taifa (TBC), Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, William Mhando, alisema mgawo huo umesababishwa na kupungua kwa vina vya maji katika mabwawa ya kuzalishia umeme pamoja na mtambo wa IPTL kuzalisha megawati 10.
  Alisema mtambo wa IPTL ambao una uwezo wa kuzalisha megawati 100 lakini kwa sasa unazalisha megawati 10 kutokana na tatizo la ukosefu wa mafuta.

  "Huko nyuma kulikuwa na mgawo lakini kwa sasa umeongezeka zaidi, maana mikoa yote inayopata umeme kupitia gridi ya taifa pamoja na visiwani Zanzibar watakosa umeme," alisema.
  Mhando alisema kuwa mikakati mbalimbali inafanyika ikiwa ni pamoja na kutafuta mitambo ya dharura ambayo itaanza kufanya kazi kuanzia Julai 31 mwaka huu.
  Alisema TANESCO wamefanya mawasiliano na Wizara ya Fedha na Uchumi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini ili kuangalia namna ya kupata fedha kwa ajili ya kununulia mafuta ya IPTL.

  Alisema kuwa Kampuni ya Symbion iliyonunua mitambo ya Dowans inaendelea taratibu kuzalisha megawati 80 na kadiri siku zinavyokwenda ndivyo inavyoongeza uzalishaji wake ili kufikia uwezo wa kutoa megawati 112.
  "Pia Kampuni ya Aggreko hadi kufikia Agosti mwaka huu nayo itaweza kuzalisha megawati 100, hivyo tunaamini tatizo hilo litapungua," alieleza.

  Alisema kuwa kukamilika kwa mtambo wa kuzalisha umeme uliopo mkoani Mwanza ambao utaweza kutoa megawati 60 hadi 100 nayo inaweza kupunguza tatizo lililopo.
  Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, alisema serikali inaendelea kutafuta suluhisho la tatizo hilo kwa kujenga mtambo wa kuzalisha umeme katika Mkoa wa Mtwara ambao utatoa megawati 300.

  Wakati Mhando akizungumzia hilo, wakazi wa Mkoa wa Ruvuma wamelazimika kukaa gizani kwa saa 16 kutokana na majenereta kukosa mafuta. Ilielezwa kuwa hatua hiyo imetokana na majenereta hayo kukosa mafuta ya kuendeshea hivyo kulazimu viongozi wa shirika hilo katika mkoa huo kuomba msaada kutoka makao makuu.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 3. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #3
  Jun 23, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Sasa nimekubali, tukiitwa a third world ni kweli, tena may be tulitakiwa tuwe fith world. Umeme kimeo!
   
 4. Saeedgenius

  Saeedgenius Member

  #4
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 48
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  atleast Symbions waesimama kwenye ahadi yao wanazalisha umeme bila mizengwe na kitu kikubwa zaidi ni kwamba wanawauzia Tanesco bila hata guarantee. Wawekezaji wa namna hii ndio wanatakiwa nchini kwetu. Hakuna ubabaishaji.
   
 5. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 23, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Mkurugenzi wa Tanesco na katibu mkuu wa wizara ya nishati hawajatoa suluhu endelevu kwenye tatizo la umeme. Jenereta ni suluhu ya dharula.
  Hivi mvua zote hizi mabwawa yasijae maji? Au mabwawa yenyewe hayatunzwi na kusafishwa kwa kuondoa tope na uchafu woote unaotapakaa humo?
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Aaaaah
  yaaani.....mmmmmmmmhhhhh.....uuuuuuuufffffffff.......kaaaaaaaaaaaaa.....ooooooooooossssssshhhhhhh......daaaaaaaaaaahhhhhhhh.....mweeeeeeeeeeeeee.......grrrrrhhhhhhhh.
   
 7. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #7
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Pambaf! and someone tells me eti JK is a maverick!!!!!!!!
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  tatizo bongo ni kwamba tunazani ukishaweka kitu chochote kitajiongoza chenyewe poor administration in tz..
   
 9. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Hizi ahadi za MEGAWATI zimenikera kwa miaka 20 sasa!!!
   
 10. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2011
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,146
  Likes Received: 1,240
  Trophy Points: 280
  Pambavu kabisa, sisi hatuhitaji mahesabu ya megawati, tunataka kuona umeme unawaka. Sijawahi kuona watu mufilisi wa akili kama hawa, pamoja na kutunyonya na bill za umeme kubwa lakini bado wanatugawia umeme, soko la umeme lipo la kumwaga, lakini wapo wapo tu wamekalia ufisadi na miradi ya dharura.
   
 11. Innovator

  Innovator Content Manager Staff Member

  #11
  Jun 23, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 387
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  PUBLIC NOTICE
  (Issued under section 19 of the EWURA Act, Cap. 414 and Section 8 (2) of Electricity Act, Cap. 131)


  NOTICE is hereby served that EWURA has received an application for Electricity Generation Licence from Symbion Power LLC, a company duly incorporated in Tanzania with the particulars set out hereinafter below:

  1.0 Name and Address of the Applicant
  Symbion Power LLC,
  Plot No. 68, Haile Selassie Rd, Msasani
  P.O.BOX 105371
  Dar Es Salaam,
  Tanzania

  2.0 License Particulars:
  (a) Type of License


  Symbion Power LLC has acquired Dowans Natural Gas fired plant installed at Ubungo thus applied for a generation license to operate 112.5 MW available capacity at Ubungo in Dar Es Salaam Region. Electricity generated will be sold to TANESCO under the Power Off Take Agreement of June 2011.

  Generation Facility: Gas to Electricity Generation
  Location: Ubungo, Dar Es Salaam
  Duration: Two Years
  Buyer: Tanzania Electric Supply Company Limited (TANESCO)

  3.0 Details of Shareholder
  Symbion Power Holdings LLC - 100%
  2711 Centerville Rd, Suite 40
  Wilmington, Delware 19808
  United States of America

  Any person who wishes to make any representations or objections with respect to the application should do so in writing to EWURA at the hereunder mentioned address not later than 17:00 hours on the 8th day of July 2011

  Director General
  Energy and Water Utilities Regulatory Authority (EWURA)
  6th Floor, Harbour View Towers
  Samora Avenue/Mission Street
  P.O.BOX 72175, Dar es Salaam
  Facsimile:+255-(022) 2123180
  Email: info@ewura.go.tz
  Website:EWURA - Energy & Water Utilities Regulatory Authority of Tanzania
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Symbion hata megawati 100 hawajafika. Sijui kama na wao watapewa miaka 10 ya kutolipa kodi yoyote. Kwa viongozi wetu wa CCM na SERIKALI yake ili mwanamke aonekane anavutia ni lazima akae au atembee uchi. Ndicho tunachofanya sasa kuwavutia wawekezaji kulingana na nilioyaona na kuyasikia TBC1 kwenye mjadala wa finance bill 2011 jana jioni.
   
 13. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #13
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  double-loss kwa wenye dstv,startimes,etc., umeme uwepo au usiwepo, bili iko palepale!
   
 14. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #14
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Bado tunaendelea na mikataba ya ajabu.....sasa mtu mpaka keshaingia mkataba wa kuuza TANESCO hii notisi ya kuping hadi julai 8 ina nguvu kweli? Mimi sioni manufaa ya hii EWURA
   
 15. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #15
  Jun 23, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Tutaendelea kuzurura sana
   
 16. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #16
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,887
  Likes Received: 6,071
  Trophy Points: 280
  lakini hawa EWURA nao, kwani wametoka wapi!? ...huko walikokuwa hawakuwahi kusikia au kujiuliza maswali haya:
  • kuwa Tanzania kuna kampuni tata inaitwa DOWANS?
  • kwamba DOWNS inaidai serikari ya JK $64m?
  • kuwa mahakama ilizuia kila kitu kinachohusiana na DOWANS kisimamishwe mpaka kesi itakapoisha?
  • kuwa Symbion imenunua mashine za kuzalisha umeme kutoka DOWANS???
  • nk, nk, nk, nk, nk, nk!?
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Formality tu Mzee. Msije mkawashtukia baadae ikawa ni issue.
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  kazi ipo!!!!
   
 19. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #19
  Jun 23, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  PHP:
  Alisema TANESCO wamefanya mawasiliano na Wizara ya Fedha na Uchumi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini ili kuangalia namna ya kupata fedha kwa ajili ya kununulia mafuta ya IPTL

  Hii ni kali jamani!
  Inakuwaje leo hii ndio wanaangalia namna ya kupata fedha, kwani huu ni mradi mpya?...Kwani hakuna utaratibu endelevu wa kupata fedha za mafuta?
  Naamini sasa kuwa SERIKALI YA JK INAPUMUA KWA MASHINE.
  Nchi hii ikabidhiwe kwa mtu anayeiweza.
   
 20. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #20
  Jun 23, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama mafuta(IPTL) yamekwisha ina maana pesa hakuna! Mbona tunalipa umeme kadri tunavyotumia?! (LUKU) Hela wanapeleka wapi mpaka wasinunue mafuta?! Au ndo wanawapa Dowans malipo ya LUKU? Hii serikali ni..(tusi) hv mpaka leo wanajadiri umeme wa dharura? Kama wanategemea mvua idara ya utabiri wa hali ya hewa haiwapi taarifa Tanesco wakajiaanda kujiepusha na hizo dharura?
   
Loading...