Kama mgao wa umeme umeshaanza mbona hatuambiwi, imekuwa kero sana

Agresive

JF-Expert Member
Feb 18, 2018
889
1,226
Wadau habari ya Weekend,

Hii ni wiki ya pili eneo nilipo kwa sasa suala la umeme kukatika imekuwa ni kila siku lazima ukatike kwa muda wa masaa 4 hadi 7.

Kibaya zaidi wiki hii kuanzia juma4 kila siku umeme unakata saa 1 kamili jioni na unarudi saa kati ya saa 5 hadi 7 usiku.

Mgao wa umeme Tanzania imeshakuwa ni sehemu ya maisha toka uhuru ila tu kununua VX NA V8 ndiyo vipaumbele vya serikal kuliko kuimarisha miudo mbinu.

Hoja yangu ni kuwa Kama kuna mgawo mkali kiasi hiki basi tupewe ratiba ili umeme ukikata tusishangae kuliko kinachoendelea.

Miaka 6 ya Jiwe hatukuona haya ila baada tu ya kuondoka ndiyo vina vya maji vikapungua, mara mitambo haikufanyiwa matengenezo visa haviishi.

Wewe huko uliko hali ikoje?
 
Back
Top Bottom