Pamoja na ujio wa Symbion, mgao kama kawa!

kwa jinsi madhara haya ya umeme yalivyoniathiri, nashindwa hata kuchangia, nina hasira mno, nasikia mpaka kizunguzungu, siku ya tatu leo ofisi yangu haijafanya kazi, nina tender kibao ofisini kwangu, sijui nifanyaje.
 
Wananchi, tuwaandikieni hao EWURA kupinga kwa nguvu zote kununua umeme wa Symbion, inavyoonekana hao symbion ndio Dowans wenyewe wamekuja kwa jina jingine, wakifanikiwa hili, wale wote waliojihusisha na richmondi na then dowans watakuwa cleared kiujanja ujanja. Can you imagine Dowans walipwe mabilioni, halafu watuzunguuke waende wakapewe tenda nyingine ya kuzalisha umeme kwa jina la Symbion?. Nina wasiwasi kwamba wamarekani wameamua kuingilia kati hii ishu ya Dowans ili kuusaidia utawala wa Mkuu ambao ulianza kupoteza credibility kutokana na ishu ya Dowans, otherwise hii ishu ilikuwa iuyumbishe utawala wake kiasi hata cha kuanguka, sasa si ajabu Wamerakani wameamua kumpiga tafu Mkulu in exchange ya Support kumuondoa Gadafi, ndiyo maana Hillary Clinton alipokuja bongo alitembelea hiyo mitambo ya Symbion ili kuipa clean image!. Na nina wasiwasi pia kwamba Makali ya Mgawo yanafanywa makusudi ili kuwafanya wananchi wakubali solution yoyote itakayoletwa hata kama ni ya Dowans kupitia Symbions, na ili waweze kuivunja TANESCO kiulaini bila watu kupiga kelele. Mvua kibao zilizonyesha itakuwaje mabwawa ya Mtera yasitosheleza maji?, i dont buy it
 
Wanajamvi, leo nimetinga maeneo ya Kimara kumtembelea rafiki, hatujakaa hata nusu saa mara, Ngeleja akaondoka na "Ufalme wake". Mwenyeji wangu akaamua kuwapigia simu Tanesco Kimara nao bila ajizi wakatujuza kwamba ni Mgao. Tukawauliza mbona tumeambiwa kwamba mitambo ya Symbion imewashwa! Jamaa wa Tanesco akatujibu kuwa hawna taarifa hiyo na mgao unaendelea kama kawaida na kwa kuwa haukukatika toka asubuhi hii ndio ratiba yao.

Kama tulishindwa kushangaa bus la lililofungiwa last week la Morobest limepata ajali jana likiwa na abiria, je tutashangazwa na nini tena!
 
Wewe sema umeme hamna nyumbani kwetu Kimara Bonyokwa, unamtebelea rafiki yako usiku? Mijitu mingine bana kwani ukisema unakaa Kimara Bonyokwa ni kosa? Hata kama hakujapimwa
 
Wewe sema umeme hamna nyumbani kwetu Kimara Bonyokwa, unamtebelea rafiki yako usiku? Mijitu mingine bana kwani ukisema unakaa Kimara Bonyokwa ni kosa? Hata kama hakujapimwa
Leo sehemu nyingi za JIJI hazikua na umeme kwa muda mrefu kuliko kawaida yaani kwa kiswahili sanifu Mgao umeongezeka Makali.
 
zile ahadi za ongezeko la megawat za Agreko na Simbion zimeishia wapi? au ndo funika kombe mwanaharam apite?

Nanukuu: "Tunaelewa kutokana mgawo huu, uchumi wa nchi umeyumba, watu wanapoteza ajira hivyo tunalazimika kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha mgawo huu unakwisha kabisa na ifikapo Desemba utakuwa umepungua,” alisema Bw. Ngeleja.

Aliwaomba wananchi kuwa wavumilivu na kumtaka Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bw. William Mhado, kutoa taarifa yanapotokea mabadiliko.

“Kama kuna mabadiliko ya ratiba ya mgawo ni vyema mtoe taarifa kwa umma badala ya kukaa kimya, hili ni tatizo la wote sio nyinyi peke yenu,” alisema Bw. Ngelena na kuongeza kuwa, ahadi ya kupunguza makali ya mgawo aliitoa bungeni kwa kuhakikisha ifikapo Desemba mwaka huu, mitambo yote mitatu itakuwa ikizalisha umeme.

Kwa upande wake, msimamizi wa mtambo wa Symbion Bw. Moses Mwandenga, alisema mtambo huo ambao unatumia gesi na mafuta una uwezo wa kuzalisha megawati 112 za umeme na kuna mitambo minne yenye uwezo wa kuzalisha megawati 20.

“Mtambo huu wa Symbion ambao unazalisha megawati 112 tunauwasha kesho (leo), hivi sasa unazalisha megawati 75,” alisema.

Msimamizi wa miradi hiyo kutoka TANESCO, Bw. Saimon Jirima, alisema mradi wa Jacobsen ambao unasimamiwa na Bw. Marrkko Rapo, ulitarajiwa kukamilika Juni 2012 lakini kutokana na dharura iliyopo, mradi huo unatarajiwa kukamilika kabla ya kipindi hicho.

Alisema mradi huo wenye mashine tatu zenye uwezo wa kuzalisha megawati 35 kila moja, tayari umeanza kufungwa vifaa ambapo mtambo wa Aggreko, una mashine 63 zilizokamika katika kituo cha Ubungo badala ya 50 zilizokuwa kwenye mkataba wa makubaliako.

“Vituo viko viwili, kimoja Ubungo na kingine Tegeta, kila kimoja kinatakiwa kuwa na mashine 50 lakini wameleta na mashine za ziada ili kuziba pengo kama litatokea tatizo,” alisema Bw. Jirima.

Hata hivyo, Bw. Mhando alisema hadi sasa kuna megawati 570 za umeme ambazo zinazalishwa nchi nzima na bado jitihada zinaendelea kufanyika ili kupunguza kero iliyopo ambapo mitambo hiyo inatarajiwa kuanza kuzalisha umeme mwezi huu.

imekula kwetu wakuu, Watanzania tumekuwa wapole sana........
 
Mgao kwisha Tanzania ni kituko cha kuwekwa kwenye Guiness book of records. I'm ready to bet my head the Ngeleja statement won't be true !
 
Ngeleja aliposema mgao wa umeme kuwa historia alimaanisha mgao huu uliopo ni wa kihistoria na hakumaanisha kumaliza mgao. Kweli huu mgao ni wa kihistoria haujawahi kutokea popote duniani.
 
Back
Top Bottom