Wakati matokeo ya kidato cha nne yaliyotangazwa Januari 15 mwaka huu yakionyesha ufaulu kupanda kwa asilimia 5.19, zaidi ya nusu ya waliofanya mtihani huo wamepata daraja la nne.
Kulingana na takwimu na Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) watahiniwa 221,049 sawa na asilimia 50.74 wamepata daraja la nne, kati yao wasichana ni 126,773 na wavulana 94,276.
Wakati takwimu zikiwa hivyo kwa daraja la nne, jumla ya watahiniwa 61,696 walipata daraja sifuri.
Bila ya serikali kuja na mpango mahususi wa kulisaidia kundi hili kuna hatari ya kila mwaka kuzalisha vijana wengi wasio na shughuri maalumu mitaani, kwa sababu daraja la nne halimuwezeshi mtu kuchaguliwa katika shule ya Serikali.